Abuhunna
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 409
- 233
Wewe ni muislam km ulivyo jitambulisha mwenyewe, na sherehe husika ni ya kikristo, inakuhusu nini kuhudhuria ibada za imani za watu wengine, hapo tayari umeukosea uislam na kuna hatari kwa myenendo yako hiyo inaweza kuwa unajiita muslam kumbe siku nyingi umeshatoka ndani ya uislam bila kujijua, muislam hana ruhusa ya kuingia katika ibada za imani nyengine hapo tayari anakuwa amekufuru, na waliokufukuza katika ibada yao walikua sahihi sana, tena wamekusaidia.Tukisema ni ubaguzi nitakuwa nimekosea? Kuna kasumba huku mkoa ninao ishi kuna ubaguzi ambao ndugu zangu wa upande wa pili yaani wakristo wanaufanya siandiki kwa ubaya wala ugomvi na mtu fulani kusema ukweli wakristo wa huku au sijui kote wapo hivyo wana ubaguzi sana iweje mimi nialikwe kwenye kipaimara na kupewa kadi kabisa ila nimefika tu ukumbini nimefukuzwa kuuliza sababu ni nini eti naambiwa mimi ni muislamu siruhusiwi kuhudhuria sherehe za wakristo eeeeh! Nimejiuliza sana maswali kwanini ndugu zangu hawa ni wabaguzi sana?