Nimefukuzwa tena kundini

Bisma...
Kwa umri wenu nyie ni wanangu kwani mimi ni miaka 71 na mjukuu wangu wa kwanza ana miaka 10.
 
Ndo ujue athari ya brainwash inayofanywa kwa wananchi.

Tuwekee hapa historia tutawaeleza wenetu ukweli ili tusiishi kwenye giza la uongo dhidi ya nchu yetu
 
Hili lina mantiki sana mkuu.

Lakini kuoanisha histotia ya uhuru na upumbavu uliowekwa kwenye huu mkataba ni sawa na kulazimisha tembo kulala kitandani.

Tuanzishie huu uzi tutiririke maana vifua vimejaa
 
Hapa watu wanaongelea historia, Bumunda ni wewe unaeharibu mada za watu kwa ujinga uliobebeshwa.
Tayari tumekujua, haya wahi kuna nyama ya ngamia🤣
 
Glenn,
Kwa nini unanilazimisha nikujibu?
Nina umuhimu upi kwako?

Huu ni uwanja huru sote tunajadiliana.
Hatutishani wala kupeana "ultimatum," hapa.

Mzee Mohamed Said
Ikiwa mwandiko wangu umeonyesha hata dalili au viashiria vya kukutisha, ninaomba RADHI SANA KWAKO.

Nia yangu sio kukutisha au kukulazimisha.

Nia yangu nilitaka kujua UTHABITI WA MAHAKAMA YAKO YA NDANI katika kutoa hukumu na haki.

Mwenye mahakama huru ndani yake hajui kupendelea kwa mrengo wake au kwa maslahi yake bali huhukumu sawa na kweli ilivyo.

Nitafurahi nikipata maoni yako huru kuhusu bandari.
Naheshimu mawazo yako

Asante sana
Mungu akubariki sana
Glenn
 
Bisma...
Kwa umri wenu nyie ni wanangu kwani mimi ni miaka 71 na mjukuu wangu wa kwanza ana miaka 10.
Umejitahidi, kwangu wewe ni baba mdogo.
Asante kwa kuwa hapa, kuna wakati unatoa elimu bora kabisa.
 
Mzee Mohamed heshima mbele.

Ningependa umjibu mdau aliyeweka maswali kweye post nambari 15.

Kuhusu historia kuchezewa haijaanza leo , hata enzi hizo mtu akipishana na mchonga alionja joto ya jiwe refer to Kambona na zile nyimbo alizotungiwa baada ya kutimkia UK.

Hadi kesho mimi hstoria nyingi za Tanzania siziamini , zina bias ya kutosha hata mapinduzi ya Zanzibar wanampinduzi halisi hawajapewa heshima stahiki.
 
Glenn,
Unadhani Maaskofu wameelewa?
Msikiti una uhusiano gani na DPW?

Masheikh ni tofauti na Maaskofu hawana uwezo wa kuikaripia serikali wala kumfukuza mtu msikitini wala kufuta dhambi zake.
Kumbe maaskofu wote ni zero kichwani?
Walikurupuka bila kuusoma mkataba?
Masheikh ndio waliuelewa zaidi?

Nyie watu dini imeharibu.
Tunajua fika mnachokitetea nyuma ya mlango wa DPW.

Katika hili tutaambiana bila woga.
Tutawanyooshea kidole bila woga.
Tutawakemea tena na tena.

Nasemaje?
Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.

Zaburi 116:6
 
Kumbe upo vitani huku na hujanishtua wakunyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…