Nimefukuzwa tena kundini

na mimi pia nina swali, je bila ya Kanisa A.Sykes angesoma na kuelimika kama alivyoelimika? Je, elimu yako Mzee Mohamed kuna mchango wowote ule wa Kanisa? Kwa maana nyingine, je, unatambua mchango wa kuja kwa Ukristo na Elimu mliyoipata Tanzania?
 
na mimi pia nina swali, je bila ya Kanisa A.Sykes angesoma na kuelimika kama alivyoelimika? Je, elimu yako Mzee Mohamed kuna mchango wowote ule wa Kanisa? Kwa maana nyingine, je, unatambua mchango wa kuja kwa Ukristo na Elimu mliyoipata Tanzania?
Kijakazi,
Nimeanza madrasa Msikiti wa Ijumaa Moshi, Mtaa wa Chini kwa Maalim Mussa.

Nimeanza darasa la kwanza Lutheran Primary School, Moshi ndani ya kanisa.

Nimesoma Kinondoni Primary School kisha St. Joseph's Convent Dar-es-Salaam.

Kabla la Wamishionari kujenga shule Waislam Pwani ya Afrika ya Mashariki ndiyo walikuwa watu wa kwanza kuelimika katika madrasa wakisomeshwa na zile 3Rs yaani Reading, Writing na Arithmetic wakitumia maandishi ya Kiarabu.

Elimu haikuanza na Wamishionari.
 
na mimi pia nina swali, je bila ya Kanisa A.Sykes angesoma na kuelimika kama alivyoelimika? Je, elimu yako Mzee Mohamed kuna mchango wowote ule wa Kanisa? Kwa maana nyingine, je, unatambua mchango wa kuja kwa Ukristo na Elimu mliyoipata Tanzania?
Hili nalo neno.

Muulize...madrasa ingetosha kuwafungua macho kiasi kile?
 
Hili nalo neno.

Muulize...madrasa ingetosha kuwafungua macho kiasi kile?
Glenn,
Pole sana huna ujuzi wa historia ya elimu.

Hapana haja ya mimi kukujibu hilo ingia Google soma historia ya elimu utaelimika.

Ukiwa uko Dar-es-Salaam nenda Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam soma paper ya Ishumi.

Hii ni paper maarufu kuhusu elimu Tanganyika.
 
Mzee Mohamed Said amejipambanua kuwa ni mwanaharakati wa dini yake.

Huwa najiuliza kuwa ni yeye pekee ndiye anaijui historia ya kweli ya nchi hii?

Kwanini lazima ahusianishe historia na dini?

Kuna kitu kinatia shaka.
 

Lakini swali langu ni kama unatambua mchango wa Kanisa katika kutoa Elimu na kuelimisha jamii yote wote Waislamu na wasio Waislamu, mfano hata Lugha ya Kiswahili grammer karibia yote kama tuijuavyo leo hii Kanisa lina mchango wake, Kiswahili kilikuwa kinaandikwa kiarabu ingawaje Kiswahili siyo Semitic languages bali ni familia ya Bantu languages jambo ambalo limesaidia watu wengi sana ambao ni Wabantu kujifunza Kiswahili kwa urahisi na kuenea nchi nzima, moja ya sababu kuu ni kwamba mwanzoni Kanisa la Tanzania ya leo lilitumia Kiswahili na kutengeneza grammer kama tuijuavyo leo hii, sasa nini maoni yako kuhusu mchango wa Kanisa na Ukristo katika ustawi wa jamii wa nchi yetu kihistoria?
 
Mzee Mohamed Said amejipambanua kuwa ni mwanaharakati wa dini yake.

Huwa najiuliza kuwa ni yeye pekee ndiye anaijui historia ya kweli ya nchi hii?

Kwanini lazima ahusianishe historia na dini?

Kuna kitu kinatia shaka.
Glenn,
Mimi ndiye niliyebahatika kufunguliwa Nyaraka za Sykes na kutokana na nyaraka hizo nikaandika kitabu.

Ndiyo sababu ya mimi kuijua historia hii.

Na ndiyo sababu wengi wameisoma historia hii kutoka kwangu.

Historia hii ina uhusiano mkubwa na harakati za Waislam kupambana na ukoloni.

Ikiwa hupendezewi na ukweli huu hiyo ni bahati mbaya kwako.
 
Kijakazi,
Wamishionari na serikali walihujumu madrasa za Waislam zilizokuwa zikisomesha Waislam kwa kupiga marufuku matumizi ya herufi za Kiarabu na kulazimisha matumizi ya herufi za Kirumi.

Elimu ikawa chini ya shule za wamishionari na serikali na ikatolewa kwa kuwabagua Waislamu.
 
Sio kwamba sipendezwi bali naona unaelemea upande wa dini kuliko uhalisia.

Na ilikuwaje hizo nyaraka upewe wewe peke yako?.

Insonywsha ulikuwa bado kijana, ilikuwaje ukapewa umuhimu huo na si wengine?

Kwa hiyo wewe ndiye mwenye historia ya Tanganyika kwa usahihi?

Tujadili kwa amani tu
 
Mmmh hii kauli inaukakasi sana.
Huu ni uanaharakati
 

Lakini Kanisa au Ukristo ulitokea Zanzibar na kuja Bara na ndiko Kanisa Kuu la kwanza lilipojengwa na Zanzibar ilikuwa 99.9% islamic hivyo sidhani kama kulikuwa na ugomvi wowote kati ya Sultani na Kanisa vinginevyo lile Kanisa lisingekuwepo mpaka leo hii kwenye nchi ya Uislamu, hivyo kama kuna chochote ambacho Kanisa lilifanya kilikuwa na baraka za Sultani pamoja na hicho ulichokiita kulazimisha, kote Bagamoyo kuna Kanisa kubwa na hakuna mahali kulikuwa na vita kati ya Kanisa na Sultani kwa uelewa wangu hivyo Sultani aliyetawala Zanzibar aliruhusu kila kitu kwa maoni yangu, siajabu hata Sultani na Wamisionari walielewana zaidi ya sisi Wakristo na Waislamu wa leo.

Kanisa la Kristo Zanzibar, Ukristo ulitokea hapa na kuingia Bara

 
Binafsi naamini kanisa limejaza watu ujinga (mass brain washing) kwa mgongo wa elimu.
 
Binafsi naamini kanisa limejaza watu ujinga (mass brain washing) kwa mgongo wa elimu.

inawezekana uko sahihi labda lkn kulinganisha na nini au mfumo gani? Dunia nzima inafwata mfumo wa Kanisa kwa maana western capitalistic system ni christian bila ya Kanisa kusingekuwepo na mfumo huu wa kiuchumi unaotawala Dunia ya leo, mfumo ambao umerahisisha maisha na ku uplift maisha ya watu klk mfumo wowote ule kuwahi kutokea Duniani, hakuna kipindi ambacho binadamu ana maisha ya nafuu kama leo hapa Dunia thanks to capitalism, hivyo kusema kwamba Kanisa limejaza watu ujinga unaweza kuwa uko sahihi lkn kulinganisha na nini?
 
Mzee wangu usipoelewa utafukuzwa magroup mengi sana.
 
Hapana, siyo dunia nzima, rudi kafanye homework. Mfumo huo tuliletewa wajinga ndiyo waliwao. Hata waliotuletea hawaufati.
 
Glenn,
Hilo la kuelemea mimi siwezi kukuingilia wewe ikiwa unaona hivyo sawa.

Hakika nilikuwa kijana lakini tayari makala zangu zikichapwa na majarida maarufu ya Afrika yaliyokuwa London kama New African na Africa Events.

Kwa nini Nyaraka za Sykes nilipewa mimi hili swali angelijibu marehemu Ally Sykes kama angekuwa hai.

Lakini naamini nyaraka hizi nilifunguliwa mimi kwa sababu kwanza aliniuliza kama naweza kuandika kitabu.

Nikamjibu naweza.

Akanifungulia safe ambayo ilikuwa haijafunguliwa kwa miaka 30.

Hili alilifanya naamini kwa yeye kuniamini mimi kama mwanae kutokana ule uhusiano na ihsani ilyokuwapo baina ya baba yangu na yeye toka udogo wao.

Labda nikueleze kitu.

Nina mswada wa kitabu cha maisha ya Ally Sykes: "Under the Shadow of British Colonialism: The Life of Ally Sykes. "

Hii ni Autobiography mimi na yeye tulikaa kitako akanihadithia maisha yake kuanzia kuzaliwa kwake 1926.

Tulipofika 1942 alipotoroka nyumbani kuijiunga na KAR aende Burma WWII akampigia simu Peter Colmore akamwambia, ,"Namleta Mohamed Said mwanangu nataka umweleze tulivyokutana Nairobi kwenye duka la Assanand Music mweleze urafiki wetu."

Peter Colmore, Peter Colmore, Peter Colmore mtu wa pekee.

Si akili ya kawaida.

Ally Sykes akanijulisha kwa mtu mwingine Jim Bailey kichwa hatari.

Hawa wote kama yeye walikuwa matajiri wakubwa.

Tusimame hapa.

Ukitaka kuwasoma ni nani hawa ingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Fanya name search hapa JF Jukwaa la Historia.
 
Nje ya mada naomba nikuulize hivi nini sababu ya kutokuwepo uraia pacha?.

1 Bibi yangu alikuwa na passport ya British na alipo zalipo zaliwa( kabla ya kuwa Tanzania)

2 Jee ni ulikuwa uoga wa Nyerere kwa Kambona na Abdul-rahman Babu?.

3 Uoga wa ccm kutokutaka challenge na wasomi wenye raia pacha watakao wafunua macho wananchi walio lala?.

4 Kuilinda Tanzania kutoka kwa raia wageni kutokumiliki rasilimali ya nchi?.(mbuga,madini na wawekezaji wa hisa wengi ni wageni kwa sasa)

5 Mtanzania aki nyanganywa uraia wa kupewa na kurudishwa kwao Tanzania jee atapokelewa kama nani?.
 
Glenn,
Unadhani Maaskofu wameelewa?
Msikiti una uhusiano gani na DPW?

Masheikh ni tofauti na Maaskofu hawana uwezo wa kuikaripia serikali wala kumfukuza mtu msikitini wala kufuta dhambi zake.
Mashehe darasa la pili B wanajiona waarabu kisa wanaongea kiarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…