Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256

Sasa nimeamini kuwa dini ni kwaajili ya maskini na waoga tu.

Mpaka leo hakuna mwanadamu au kitu chochote ikiwemo Mungu alitethibitisha kuwa Mungu yupo.

Kila mtu atakuthibitishia kwa maandiko ambayo yameandikwa kwa mkono wa mtu.

Ukiondoa maandiko hakuna mtu wa dini kukuthibitishia uwepo halisi wa Mungu.

Waislamu kwa kitabu chao watakuthibutishia uwepo wake, Wahindu, Wabudha, Waktisto n.k watakuthibutishia uwepo wa Mungu kwa maandiko na hadithi tu ila hawataweza kukuthibitishia kwa njia nyingine ya reality.

Kwa taabu wanazopata watu duniani ni kama nature ndio inatawala.

Haiwezekani Mungu ambaye wanasema aliupenda ulimwengu aruhusu vita, ubakaji, kuchinjana, kudhulumiana, ufukara, njaa n.k huku hivyo vitu ni vidogo kwake angevikomesha ndani ya sekunde.

Je, Mungu kazidiwa utu na upendo na mwanadamu?

Hii amani na hali ya maendeleo tunayoiona ni fikra na utu wa binadamu kwa ulimwengu.

Binadamu anaunda mabaraza ya kitaifa kupambana na majanga mbalimbali, pasipo na haya mabaraza Dunia isingekalika kabisa kwa idadi hii ya watu ilivyo kwa sasa.

Illusion ndizo zinatawala watu ndio maana kila dini na dhehebu wanajiona kuwa wako sahihi na wana ushahidi kuwa dhehebu lao ndilo sahihi mbele za Mungu na wao tu ndio wataingia mbinguni au peponi.
 
Bora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Hata ukiamini Mungu yupo mbona haikuzuii kufanya mambo yoyote unayotaka!???
Binadam aliyekamilika anapaswa kuishi kwa ustaarab flan na utaratibu hata kama haamini Mungu.

Haya sasa umeamua kutoamin, inakusaidia nini??au inakuongezea nini ambacho hukua na fursa kuki parsue...Ulipokua ukiamin, ni kitu gan ulikua unapungukiwa??

Una unaishi kwa kukariri??
 
Kwahiyo wewe unaamini kwasababu ya woga tu na si reality?
 
Back
Top Bottom