Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Ufute usite siku ya hukumu ya haki ipo pale pale. Kama hakuna Mumgu nani husababisha kifo na wafu roho zao zimekwenda wapi?
Roho ni nini?
Haya kuku hana roho?, kama anakufa basi tuseme ana roho, je, akifa roho yake Inaenda wapi?
 
Bora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Hata ukiamini Mungu yupo mbona haikuzuii kufanya mambo yoyote unayotaka!???
Binadam aliyekamilika anapaswa kuishi kwa ustaarab flan na utaratibu hata kama haamini Mungu.

Haya sasa umeamua kutoamin, inakusaidia nini??au inakuongezea nini ambacho hukua na fursa kuki parsue...Ulipokua ukiamin, ni kitu gan ulikua unapungukiwa??

Una unaishi kwa kukariri??
Kuamini kuwa yupo ni kufuata maelekezo yake kinyume na hapo huna tofauti na asiyeamini.Hata shetani anaamini Mungu yupo. Kutenda mema tu sio kigezo cha kwenda mbinguni.Kigezo cha kwenda mbinguni ni kuamini kuwa Yesu amesulubiwa na kufa kwa ajili ya dhambi zako ili wewe uhesabiwe haki na Mungu kupitia Yesu Kristu.Hii ndo condition pekee ya kuingia mbinguni na sio matendo mema tu.
 
Hilo swali nitalijibu kwa swali.
Huyo Mungu aliumbwa na nani?
Au wazo la kujiumba alipewa na nani?
Mungu hakuumbwa,hakuwa na mwanzo wala hana mwisho.Yeye ndo alimuumba time hivyo hawezi kufungwa na muda,yeye ndo aliumba matter (maada) hawezi kuwa sehemu ya matter (maada) maana kabla hapajawa na maada yeye alikuwepo na yeye ndo aliumba space na vyote vilivyomo.

Nikuulize wewe sasa,kama hakuna Mungu kila kilichopo ulimwenguni kimetoka wapi?
 
Hao wanasayansi walioanzisha neno nature na jinsi inavyofanya kazi watu wa dini mliwaua sana baada ya kuwashinda kwa hoja, lakini ndio wanaotengeneza simu na kutumia mawimbi kurusha mawasiliano sasa unakomenti kwa raha zako, home umeweka tv ya mwanasayansi ambaye kazi yake inathibitika kila leo
Science inaongoza na laws of nature(materialism) ambazo ziliwekwa na Mungu,hakuna laws pasipo na lawmaker...there must be one. Thinking inaongozwa na three laws of logic,if there is laws of logic who made them?
 
Kuamini kuwa yupo ni kufuata maelekezo yake kinyume na hapo huna tofauti na asiyeamini.Hata shetani anaamini Mungu yupo. Kutenda mema tu sio kigezo cha kwenda mbinguni.Kigezo cha kwenda mbinguni ni kuamini kuwa Yesu amesulubiwa na kufa kwa ajili ya dhambi zako ili wewe uhesabiwe haki na Mungu kupitia Yesu Kristu.Hii ndo condition pekee ya kuingia mbinguni na sio matendo mema tu.
Mambo ya kwenda mbinguni ni mengine kabisaa.
Si kila mtu ana mpango wa kwenda huko japo ana amini Mungu
 
Back
Top Bottom