Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Kwa mamlaka ya Yesu natamka nguvu ikushikie.Na utakuwa MTU wa kwanza Ulipo kuona Ukuu wa Mungu.Tubu Leo mambo yako yote yatakuwa sawa futa kauli chafu
Mikwara hii, thibitisha kwanza kama MUNGU yupo.
 
Mungu kakuumba na utashi unaokuwezesha uchague unavhotaka. Ila anakushauri umsikilize Yeye maana atakupa jawabu bora kwa kila utakalouliza. Lakini mwanadamu unajifanya akili nyingi kisa tu umeumbwa kwa sura na mfano wake. Ukipata matokeo ya uchaguzi wako unarudi kulalamika kuwa Mungu hayupo.

Mungu sio dikteta. Unayoyaona duniani ni matokeo ya ukaidi wa mwanadamu. Onjeni mpate kujua ya kuwa Bwana yu mwema. Ndugu nakukuombea ukutane na Bwana kwa njia ya kipekee hakika utaishi kuelezea matendo makuu ya Mungu.

#Mwanadamu alianguka
#Yesu alikamilisha
#Biblia ni Neno la Mungu
Maelezo matupu hakuna hata picha halisia ya kuambatanisha kwamba MUNGU yupo? Leta evidence wazi isiyo na makando kando
 
Unaanza kunikwepa? Thibitisha kwanza uwepo wa MUNGU kwa ushahidi ulio hai.
Mimi sikukwepi ila hua napenda mtu niende nae taratibu mpaka aelewe. Umekubali kuwa majini wapo. Na huko juu nimeona unamwambia mtu kuwa alete picha ya Mungu. Kupitia kwenye uwepo wa majini utaelewa tu. Umekubali kuwa majini yapo je unaweza kuniambia majini wana maumbile gani?
 
Kipi hasa ambacho unataka nifanye ili ndio iwe uthibitisho wa kuwepo Mungu?
Unachoona kinafaa
Thibitisha,
Sisi tunakuthibitishia hayupo kwa maandishi tu. Hatuwezi kukuonyesha au kumeleta au kumwambia afanye hili au lile kwakuwa hayupo.
Wewe unayesema yupo thibitisha
 
Unachoona kinafaa
Thibitisha,
Sisi tunakuthibitishia hayupo kwa maandishi tu. Hatuwezi kukuonyesha au kumeleta au kumwambia afanye hili au lile kwakuwa hayupo.
Wewe unayesema yupo thibitisha
Mimi nataka wewe unayetaka uthibitishiwe ndio uniambie ni kitu gani nifanye ambacho kitakuwa ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu? Maana ni nyie ndio ambao mnasema hakuna Mungu na hakuna uthibitisho hivyo ni vyema ukaeleza ambacho kifanyike ili iwe ndio uthibitisho wa uwepo wa Mungu.

Kuhusu ninyie hamjaambiwa mthibitishe kisichokuwepo bali mnaambiwa mthibitishe kutokuwepo kwa hicho mnachodai kuwa hakipo,mtofautishe kusema kitu fulani hakipo na uhakika wa kutokuwepo hicho kitu.
 
Daaaahhh ngoma ngumu.
Hivi kati ya watu 2 ambao mmoja anasema humu ndani hakuna mtu na mwingine anasema humu ndani kuna mtu, ni yupi atapaswa kuthibitisha kauli yake mara watakapoingia humo ndani?
 
Daaaahhh ngoma ngumu.
Hivi kati ya watu 2 ambao mmoja anasema humu ndani hakuna mtu na mwingine anasema humu ndani kuna mtu, ni yupi atapaswa kuthibitisha kauli yake mara watakapoingia humo ndani?
Wote wanasema(wanadai) hivyo wote wanapaswa kuthibitisha madai yao. Kusema tu kuna mtu hakufanyi huyo mtu kuwepo na kusema tu hakuna mtu hakufanyi huyo mtu asiwepo.

Niambie ni kipi unahitaji nifanye ili iwe uthibitisho wa kuwepo Mungu? Mimi naamini uwepo wa Mungu ila wewe unataka uthibitisho.
 
Save your energy for better things. Huyo kachagua upande tayari. Si kwa sababu ya ushahidi au kitu chochote. Wengi hupenda kuogelea kwenye maisha ya dhambi na wakikubali Mungu yupo itawalazimu kuyaacha hayo maisha. Hii kitu hawaitaki so only solution ni kujaribu kujiaminisha kuwa hakuna Mungu na kwa kuwa nafsi zao zinawasuta wanakuja huku nje kutafuta angalau consolation kuwa ah kumbe siko peke yangu.

Hakuna idadi ya ushahidi inamsaidia mtu wa aina hii kwa sababu shida yake sio ushahidi. Kwa hiyo tunza nguvu zako katumie kufanya kitu bora. Acha wafu wazikane kwa kutiana moyo. Ipo siku watajua ukweli na hawatahitaji kubishana na mtu kwa sababu hakutakuwa na mtu wa kubishana naye na watajua kwa hakika kama Mungu yupo au hayupo!
Nashukuru kaka
 
Wote wanasema(wanadai) hivyo wote wanapaswa kuthibitisha madai yao. Kusema tu kuna mtu hakufanyi huyo mtu kuwepo na kusema tu hakuna mtu hakufanyi huyo mtu asiwepo.

Niambie ni kipi unahitaji nifanye ili iwe uthibitisho wa kuwepo Mungu? Mimi naamini uwepo wa Mungu ila wewe unataka uthibitisho.
fanya chochote ilimradi uthibitishe tu, nakumpa uwanja mpana
 
Ufute usite siku ya hukumu ya haki ipo pale pale. Kama hakuna Mumgu nani husababisha kifo na wafu roho zao zimekwenda wapi?
 
Kuhusu machafuko na maradhi yanayozidi kuikumba dunia hilo sio kosa la MUNGU.Ni kosa la mwanaadamu mwenyewe kukataa na kubadili sheria ya MUNGU.Ndiyo maana laana inaitafuna dunia(ISAYA 24:1-5)
 
Back
Top Bottom