Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa

Mkuu mwanamke mjamzito mchukulie kama mtoto tu yaan ukiwa nae serious kiasi hicho kwa kila kitu anachofanya basi utatia fora mtaani[emoji16][emoji16][emoji16].Yaan hapo ianbid uwe mpole na mbunifu laasivyo utamuona msumbufu,mvivu,mlalamishi na asiyetosheka.Machemical imbalance kunako mwili wake[emoji4][emoji4][emoji4]
 
Mwanamke akiwa na mimba anakuwa kama kichaa flani.
Sio wote na hii sio kawaida. Ninae dada angu yuko kwenye ndoa enzi na enzi. Akaniambia katu usije ukatumia mimba kama fimbo kwa mwenza wako. Hizi drama watoto wa saiv mnazoziletaga hazifai. Tena mkome.

Mimba ni kiumbe cha Mungu. Na Mungu ni mpenda amani. Kamuumba alieko tumboni, kamuumba aliemuweka humo, kakuumba na wewe uliembeba. Iweje kiumbe cha Mungu kikakufanya uwe na visingizio na drama za kipepo namna hiyo. Kwann umtese mwanaume anaehangaika kukulea, kukulisha kuhakikisha unaishi ukiwa salama bila shida. Tena mara nyingi wanawake wakiwa na ujauzito mwanaume anaongeza sana mapenzi maana anajua mtoto wake yuko njiani.

Sasa wewe ndo utake kuitumia kama fimbo. Hizi drama za sijui nataka hiki nataka kile sitaki hiki ni kwa watu wenye pesa. Kimwanafunzi kiko kijijini na kimepewa mimba kina nguvu ya kuchagua? Mihogo twende, magimbi twende, chochote kinapanda. Sitaki kujiapiza mengi lakin kila mara nataman nitembee kwenye ushauri wake. Mimba isiwe chanzo cha kumtesa mtoto wa mtu maana hata yeye kazaliwa na mwanamke kama mimi. Mimba inatakiwa imtukuze Mungu vilevile maana sisi sote ni mali yake. Upendo, umoja, heshima, upole juu yangu na vijacho wangu. Amen.
 
Dah umetisha Mkuu very positive [emoji122][emoji122][emoji122][emoji120]
 
Tatizo lenu, elimu,pesa na vyeo lakini bado mnashindwa kiowa wanawake wa kuwafaeni, ilibidi muowe huyo beki tatu
 
How mkuu maana mimi sijamlinganisha na mtu nimeongeanae tu kwa wema

Unalinganisha mimba ya mkeo na Za watu wengine

Nimebeba mimba mbili Hakuna hata moja iliyofanana na nyingine

Mimba ya kwanza nilikua nabadilisha tu sehemu za kulala
Nahama kitandani nahamia sofani
Nahamia mkekani, mpaka Giza linaingia
Nikisema hata niende kwenye biashara nalala
Nilishapitishwa mpaka mbagala tokea buguruni nimelala zangu kwenye daladala

Ila ya mwisho nilikua napiga Kazi mpaka mwisho kabisa lakini matukio yangu mzee alihama nyumba

Hivyo sikushauri ulinganishe mimba ya mkeo na za watu wengine

Ongeeni tu wenyewe na Kama hawezi mvumilie Kwani miezi Tisa ni mingi?
 

Inawezekana pia

Mi nakumbuka ilikua nikianza kuwasha moto anasema tu basi mama baadae na simu amekata [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama hakuwa na tabia hio kabla ya ujauzito kuwa mpole Acha hasira,
Cheza na mudi yake weka uanaume pembeni, Ili asimstress mtoto tumboni. Mvumilie akishusha kama sio tabia yake ataacha tu
Kwa kweli uko sahihi. Kila mwanamke hormones zake zina'react' kivyake kwa hivyo lazima awe mstahmilivu. Akishajifungua hali itarudi kama kawaida.
 
Kuna mdada alikuwa mwl.kafundisha Leo kesho yake akaenda kujifungua,alivyopata mimba nyingine miezi 2 tu hawezi chochote,akitembea kidogo miguu yote inavimba Hadi huruma

Ni mimi kabisa Yaani mwili unagoma kabisa kabisa
Plus craving ya Vitu ambavyo nikiwa normal haunilishi hata kwa fimbo[emoji30]

I hate being pregnant sema tu baba chanja ashanisoma anaelewa anasolve kiutu uzima


Mwenye anauza iPhone 14 akuje inbox nimfungie zawadi ya Valentines mtoto wa mama mkwe
 

Sijui ni kwa nini
Yaani utasikia utarudi kwenu na mabag yako[emoji30]

Wanawake tutafute hela
 
Mpeleke kwao bodaboda wakamchakate huko, sikuhizi wanawapenda sana wanawake wenye mimba
 
Nenda naye taratibu ndio mimba ya Kwanza lazima adeke na uvumilivu ndio unatakiwa kwenye ndoa mkuu, nenda naye taratibu huna haja ya kumpeleka kwao.
 
2:Mimba ya kwanza
3:ndio nafahamu mkuu
4: kwani nikosa kuongea na mkewangu tena kwa upendo lakin nalo kosa?
Kwa nini hukuwa na subira?
Ungesubiri urudi nyumbani uongee naye kuliko kupiga simu,ni muhimu kuwa mwanaume.
Ulivyorudi nyumbani kwa nini ukumsemesha?ila ukawa umepanic?
Jitathmini sana,uanaume si lelemama
 
siku ya kujifungua aanze tena kulalamika, mpe nauli aende akapambane na mama ake mbona atafanya tu mazoezi.
 
Wanaume acheni story za kijiweni kua mimba sio ugonjwa niliwahi beba mimba mapigo ya moyo yanaenda kasi balaa miguu na mikono haina nguvu hata kidogo wee asee mimi mjamzito hata aniambie kitu gani naamini, msiwe wajuaji kwa vitu msivyo vijua, lakini nilibeba mimba nyingine nilikua normal kabisa nilipiga kazi mpaka nikawa najishangaa yaani. Mimba hii na ile hutofautiana jamani au huyu na yule.
 
Umekosea namna ulivyomwambia lazima apanick Yani apo amekusikia kama unamwambia we ni mvivu sana wenzio wote wachapa kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…