Nimegugo dalili zote UKIMWI, ninazo

Nimegugo dalili zote UKIMWI, ninazo

Niliamka saa kumi usiku baada ya kuona hizi wiki mbili naumwa Kila siku kichwa, nahara, kitambi chote kwishaaa mkanda nimetoboa matundu sita mpya mpaka sasa.

Nikaona kabisa huu ni UKIMWI, kuchukua simu nikaingia gugo nikaandika dalili za ukimwi. Nimesoma naona zote ninazo mpaka kijipu upande wa paja karibu na korodani ninayo wanaita groin nodes.

Wakuu kupima naogopa Vibaya mno, nakumbuka mwaka 2010 niliwahi kupata mkanda wa jeshi naona hili Tena limekuja. Hii ngoma nimekuwa na stress Sana hata kazini kwenda nahisi uvivu.

Muda wote kichwa na misuli inauma nahisi kuchokaaa.
Kama si wanzuki ni lile Jani lile
 
Aliyekwambia kwamba ukikutwa na maambuzi ya VVU/UKIMWI ndiyo mwisho wa Dunia nani?

Usisite kutimiza ndoto zako za Kifamilia na ndoto zako binafsi Kwa hofu ya Kuwa na maambukizi.

Wapo watu Wana hayo maambukizi Mwaka wa 25 huu bado wanadunda.

Muhimu uzingatie taratibu zote za Afya ikiwemo Kula mlo Kamili/Kufanya mazoezi/ kupata muda wa kupumzika.

Acha kutumika sana(Usiwe unafanya sana Ngono hata kama na Mkeo), nimeona watu wengi walio na maambukizi kupenda kufanya ngono mara Kwa mara Kwa Lengo eti la "Tufe wengi" na hawapendi kabisa Matumizi ya Condom.

Kufa tutakufa tu uwe Mzima wa Afya tele ama Mgonjwa lazima Siku yako ikifika lazima utalamba udongo.

Tuendelee kujinyenyekeza Kwa Muumba wetu, tukiendelea kuishi Kwa kumpendeza yeye.

Wahi hospitali ukatambue Afya yako na Uanze tiba sasa.

Tanzania bila maambukizi mapya inawezekana, Chukua hatua 💪
 
Ulipata Mkanda wa jeshi au uligoogle pia na wenyewe? nenda kapima achana na Google. Ulipopata Mkanda wa jeshi ulitibiwaje na ulitibiwa wapi? Ninaamini kama uliambiwa Hospitali kuwa una mkanda wa Jeshi basi lazIma walikupima
Bora kupima mkuu ukajua afya yako mm nilipatwa na woga km huo nika geogle pia lkn badae nikaona bora nipime tuu na nimeshapim zaid ya mara 4 ktk miez 3 na nimeambiw imetosha namshkur mungu pia
 
Aliyekwambia kwamba ukikutwa na maambuzi ya VVU/UKIMWI ndiyo mwisho wa Dunia nani?

Usisite kutimiza ndoto zako za Kifamilia na ndoto zako binafsi Kwa hofu ya Kuwa na maambukizi.

Wapo watu Wana hayo maambukizi Mwaka wa 25 huu bado wanadunda.

Muhimu uzingatie taratibu zote za Afya ikiwemo Kula mlo Kamili/Kufanya mazoezi/ kupata muda wa kupumzika.

Acha kutumika sana(Usiwe unafanya sana Ngono hata kama na Mkeo), nimeona watu wengi walio na maambukizi kupenda kufanya ngono mara Kwa mara Kwa Lengo eti la "Tufe wengi" na hawapendi kabisa Matumizi ya Condom.

Kufa tutakufa tu uwe Mzima wa Afya tele ama Mgonjwa lazima Siku yako ikifika lazima utalamba udongo.

Tuendelee kujinyenyekeza Kwa Muumba wetu, tukiendelea kuishi Kwa kumpendeza yeye.

Wahi hospitali ukatambue Afya yako na Uanze tiba sasa.

Tanzania bila maambukizi mapya inawezekana, Chukua hatua 💪
Mkuu Asante Sana, naomba unifundishe njia ya kupokea matokeo nakuamua kukubali kama yamekuja mabaya
 
Bora kupima mkuu ukajua afya yako mm nilipatwa na woga km huo nika geogle pia lkn badae nikaona bora nipime tuu na nimeshapim zaid ya mara 4 ktk miez 3 na nimeambiw imetosha namshkur mungu pia
Mkuu nipe njia ya kupata ujasiri ili nipime
 
Mkuu Asante Sana, naomba unifundishe njia ya kupokea matokeo nakuamua kukubali kama yamekuja mabaya
Nenda ukapime kwenye Vituo vya Afya ambapo kazi ya kutoa Ushauri kabla na baada ya kupima, ni Jukumu la mtaalamu ambaye amesomea zaidi ya miaka 2 kufanya kazi hiyo.

Kwangu nitakupa maneno ya faraja kutoka kwenye vitabu vya Imani tu;

Naanza na neno hili kutoka Kitabu cha Ufunuo 21:4

Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”.
 
Back
Top Bottom