Nimegundua mapenzi hayanitaki, ngoja nifanye mambo mengine tu

Nina miaka 34 sasa nikiwa mama wa watoto 3, hakika sina budi kukubali kuwa mapenzi hayanitaki tena hayanipendi kabisaa, japo niliyapenda na kuyapa thamani katika maisha ila nimeangua sina budi kuyaacha rasmi kuanzia leo.

Historia yangu kwa ufupi,

Mpenzi wa kwanza.

Huyu alinionesha mapenzi ambayo hakika sijawahi kupata, alikuwa mkweli mpole, na mwenye mapenzi ya dhati kwangu, nami nilimpenda sana sana katikati ya penzi zito tukapata mtoto 1 kwa bahati mbaya mpenzi wangu Mungu akampenda zaidi akafariki dunia nikabaki na mtoto.

Ndiyo penzi pekee ambalo sina historia mbaya nalo, penzi hili lilidumu kwa miaka 5 na lilikuwa bado tamu ila ndo ivyo ilibidi nikubali kuwa hayupo na nisonge mbele.

Kimbembe kinaanza.

Mpenzi wa pili

Tulikutana katika mazingira ya kutafuta maisha tukaanza kuwa marafiki baadaye tukawa wapenzi, mapenzi yakaendelea japo tulikuwa na migogoro ya hapa na pale ila tunaongea tunasawazisha maisha yanaendelea.

Kushtuka nina ujauzito, nikamwambia nina ujauzito akasema sasa itakuwa aibu kubwa sana (kipindi hiko yeye alikuwa anasali kanisa fulani na mimi akanikaribisha tusali wote na alikuwa ni mtumishi kanisani hapo) akasema suluhisho ni kufunga ndoa ya haraka.

Tukaongea na wazazi, ndoa ya haraka ikapangwa, akaambiwa atoe Mahari 1,000,000 mimi nikapambana kuwaambia hii ndoa ni ya haraka hasa kuzingatia hali yangu tukichelewa tumbo litakuwa kubwa hivyo kwa sasa uwezo wake labda atoe 200000 tu, na harusi yenyewe ni ya bila sherehe.

Wazazi wakakubali, akaambiwa atoe laki mbili kumbe hana yeye akasema laki basi ikabidi wazazi wapokee tu maana ndoa ishaanza kutangazwa, harusi ikafungwa bila sherehe.

Baada ya ndoa, ilikuwa ni migogoro kama tunaigiza sinema ndani, yaani ni ugomvi kila kikucha kila siku tunasuluhisha kesi, tukipatana na siku 3 zilizobaki ugomvi, na magomvi yenyewe hata hayama maana ni ya kijinga tu hata aibu kumwambia mtu kuwa hiki ndio cha nzo cha magomvi yetu.

Ikawa kama muujiza tukafanikiwa kutulia kama mwaka nikabeba mimba nyingine nikajifungua mtoto wa 3, tukaanza kulea mtoto mchanga amani tunacheka.

Mara vita ikaanza tukarudi kugombana, hatuelewani mara siku niko kwenye kazi zangu natumiwa sms KUANZIA LEO MIMI SIO MUME WAKO TENA, nataka kumuoa Fulani( huyu dada alikua mchepuko wake) na aliwahi kuwa saabu ya mpasuko wa ndoa yetu kwa sehemu kubwa.

Nikapaniki nikarudi nyumbani nalia kama nimefiwa, basi aliporudi akanambia chukua nguo zako sepa, nikasema siondoki, kipigo nilichopigwa sitasahau nusu anitoe uhai.

Nikaondoka, nikaenda kwa ndugu, akaitwa hakuja, kupigiwa simu akasimamia uamuzi wake kuwa ndio kaamua kuniacha, nikaomba watoto akanipa nikaanza kuishi na watoto peke yetu na hata sijui alipo maana aliamua kuhama na simu kabadili namba.

Baada ya mwaka 1 nikampata mpenzi 3

Maisha ya mapenzi yakaanza penzi likachanua mpaka nikaona angalau dunia ni nzuri penzi likawa tamu, tukapanga mipango ya kuishi wote, na yeye ndio alioanzisha jambo hilo wala sikumwambia kuhusu kuishi wote.

Baada tu ya kukubali kuwa tuanze kuishi wote akaanza kuwa busy hanitafuti iwe kwa simu au sms, ukipiga simu hapokei, sms hajibu, unaweza tuma sms ya kumsalimia asubuhi ikajibiwa usiku, ukipiga simu anaka, au hapokei hata siku 3 na akipokea anakwambia nisubiri kidogo nitakupigia ndio imetoka hadi kesho upige tena, ukimuuliza kama kuna tatizo anajibu hamna, ukimuuliza kama kakuchoka anajibu hapana ila kazi nyingi.

Ukimwambia tuoanane anakubali ikikaribia muda anasema kapata dharura iwe kesho, nk, mwezi sasa yuko ivyo na hatujaonana japo sio mbali. Nimejiongeza kuwa kashaniacha ila kashindwa kusema kuwa kaniacha.

Sasa mapenzi naona niwaachie wengine mimi nipambane na malezi ya wanangu tu.

Ukiwa na pesa na uko bze na maisha yako trust me wanaume watakuhangaikia wenyewe
 
Inavyoonekana hiyo ndoa na huyo jamaa ulifosi wewe yeye hakuwa tayari ,
Sasa Angalia imekula kwako.

Aliposema
Mahali ana laki 2 badala ya milioni hadi kufika laki 1 hapo alikuwa anaonesha namna muelewe kuwa hayuko tayari na nyie mkafosi , haya sasa!
 
Sasa hivi atakae kutaka na huo wegazi (ulezi) wa watoto hao nani tena ?!

Labda iwapo uko na financial freedom kwa Mpenzi wa kupeana Furaha na raha utapata lakini kutegemea vinginevyo sizani !

Halafu sasa wengine wana neema na nguvu ya Mungu hawarogeki au ukute nao huwa wanajihangaikia mara kwa mara kucheki status akikuta umemroga anaona inatafuta kuja kumuua anakuacha mazima!
 
Ungekuwa huna watoto tungesema uendelee kutafuta new bae, mi naona ufocus kwenye kulea watoto wako wanakuhitaji kuliko hao beach boys within the process utampata mtu sahihi Wala hautotumia nguvu nyingi. All in all poleee my dear!!!!
 
Wewe unayatafuta mapenzi ili iweje?
Binafsi huwa ni kunyandua tu sina sababu kuubwa ya kuyapapalikia mapenzi zaidi ya hiyo tu.
Hivyo hayanitesi kwasababu mbusus ni nyingi mno, na ninaweza kuamua wala nisinyandue kwa muda fulani.

Sasa wewe unaingia penzini kwa kutaka kunyanduliwa au kupata faraja.?
Kama ni minyanduo mapenzi hayatakutesa sana ila kama unataka mpenzi wako ndo akupe furaha, akujali, akutreat kama malkia hapo ushafeli.
 
Ndoa ya pili ilikuwa ya haraka sababu ya mimba, actually isingeweza kuwa strong kutokana na sababu yenyw iliyowafanya muoane, japo zipo za aina hiyo zilizodumu, ni bahati hutokea.

Wa tatu amekimbia majukum nahisi, watoto wa tatu! ni ngumu Sana hasa kama alikuwa kijana mwenzio, jumlisha ulivokubali kwa haraka suala la kuishi pamoja!!, (Akili mtu wangu)

NB
Miaka 34 wanaume watatu!!? CV ya maana sana
 
Pole sana, sali sana Mungu atakupa wa kufanana na wewe… all the best..
 
  • Thanks
Reactions: THT
Watakuja kusema mzimu wa mpenzi wako wakwanza bado unawivu nawewe..[emoji1787]

Pole japo sio sana maana hatujajua waliokuacha walikuwa wanakutana na nini
Nahisi mi ujinga wao huyu dads angekuwa na tatizo wasingekuwa wanamtundika mimba.
 
Huyo jamaa wa 3 kuna mawili:

Huenda alikuwa anatesti mitambo kuhusu kuishi wote akaona imetick ghafla mno kastuka kuwa anapigwa.

Au ni kweli amedhamiria kuishi na wewe hivyo ameanza kukupima uvumilivu wako na reactions zako anapokuwa hakuzingatii.

Note:
Most women make no effort to keep their relationships healthy when the evil strikes , mara nyingi huendekeza lawama tu na kulalamika.
Huyo wa tatu aliona mzigo kulea watoto wa wenzake.
 
Sidhani kwa sababu sijawahi mpa jukumu la kununua chochote, cha wanangu na sehemu kubwa najihudumia na nahudumia wanangu katika hali ya ugumu ila najitahidi misimtegee mtu katika maisha yangu.

Kwake nilikuwa nahitaji faraja tu basi huduma zake alikwa anatoa mwenyewe kwa kupenda na si kumlazimisha afanye kitu kwa watoto.
 
Imekuchukuwa mda gani kujua kuwa mapenz hayakukubali?pole hujachelewa wanaume hawafanani, achana na wamba kwaya njoo kwa ma sheikh
 
Nina miaka 34 sasa nikiwa mama wa watoto 3, hakika sina budi kukubali kuwa mapenzi hayanitaki tena hayanipendi kabisaa, japo niliyapenda na kuyapa thamani katika maisha ila nimeangua sina budi kuyaacha rasmi kuanzia leo.

Historia yangu kwa ufupi,

Mpenzi wa kwanza.

Huyu alinionesha mapenzi ambayo hakika sijawahi kupata, alikuwa mkweli mpole, na mwenye mapenzi ya dhati kwangu, nami nilimpenda sana sana katikati ya penzi zito tukapata mtoto 1 kwa bahati mbaya mpenzi wangu Mungu akampenda zaidi akafariki dunia nikabaki na mtoto.

Ndiyo penzi pekee ambalo sina historia mbaya nalo, penzi hili lilidumu kwa miaka 5 na lilikuwa bado tamu ila ndo ivyo ilibidi nikubali kuwa hayupo na nisonge mbele.

Kimbembe kinaanza.

Mpenzi wa pili

Tulikutana katika mazingira ya kutafuta maisha tukaanza kuwa marafiki baadaye tukawa wapenzi, mapenzi yakaendelea japo tulikuwa na migogoro ya hapa na pale ila tunaongea tunasawazisha maisha yanaendelea.

Kushtuka nina ujauzito, nikamwambia nina ujauzito akasema sasa itakuwa aibu kubwa sana (kipindi hiko yeye alikuwa anasali kanisa fulani na mimi akanikaribisha tusali wote na alikuwa ni mtumishi kanisani hapo) akasema suluhisho ni kufunga ndoa ya haraka.

Tukaongea na wazazi, ndoa ya haraka ikapangwa, akaambiwa atoe Mahari 1,000,000 mimi nikapambana kuwaambia hii ndoa ni ya haraka hasa kuzingatia hali yangu tukichelewa tumbo litakuwa kubwa hivyo kwa sasa uwezo wake labda atoe 200000 tu, na harusi yenyewe ni ya bila sherehe.

Wazazi wakakubali, akaambiwa atoe laki mbili kumbe hana yeye akasema laki basi ikabidi wazazi wapokee tu maana ndoa ishaanza kutangazwa, harusi ikafungwa bila sherehe.

Baada ya ndoa, ilikuwa ni migogoro kama tunaigiza sinema ndani, yaani ni ugomvi kila kikucha kila siku tunasuluhisha kesi, tukipatana na siku 3 zilizobaki ugomvi, na magomvi yenyewe hata hayama maana ni ya kijinga tu hata aibu kumwambia mtu kuwa hiki ndio cha nzo cha magomvi yetu.

Ikawa kama muujiza tukafanikiwa kutulia kama mwaka nikabeba mimba nyingine nikajifungua mtoto wa 3, tukaanza kulea mtoto mchanga amani tunacheka.

Mara vita ikaanza tukarudi kugombana, hatuelewani mara siku niko kwenye kazi zangu natumiwa sms KUANZIA LEO MIMI SIO MUME WAKO TENA, nataka kumuoa Fulani( huyu dada alikua mchepuko wake) na aliwahi kuwa saabu ya mpasuko wa ndoa yetu kwa sehemu kubwa.

Nikapaniki nikarudi nyumbani nalia kama nimefiwa, basi aliporudi akanambia chukua nguo zako sepa, nikasema siondoki, kipigo nilichopigwa sitasahau nusu anitoe uhai.

Nikaondoka, nikaenda kwa ndugu, akaitwa hakuja, kupigiwa simu akasimamia uamuzi wake kuwa ndio kaamua kuniacha, nikaomba watoto akanipa nikaanza kuishi na watoto peke yetu na hata sijui alipo maana aliamua kuhama na simu kabadili namba.

Baada ya mwaka 1 nikampata mpenzi 3

Maisha ya mapenzi yakaanza penzi likachanua mpaka nikaona angalau dunia ni nzuri penzi likawa tamu, tukapanga mipango ya kuishi wote, na yeye ndio alioanzisha jambo hilo wala sikumwambia kuhusu kuishi wote.

Baada tu ya kukubali kuwa tuanze kuishi wote akaanza kuwa busy hanitafuti iwe kwa simu au sms, ukipiga simu hapokei, sms hajibu, unaweza tuma sms ya kumsalimia asubuhi ikajibiwa usiku, ukipiga simu anaka, au hapokei hata siku 3 na akipokea anakwambia nisubiri kidogo nitakupigia ndio imetoka hadi kesho upige tena, ukimuuliza kama kuna tatizo anajibu hamna, ukimuuliza kama kakuchoka anajibu hapana ila kazi nyingi.

Ukimwambia tuoanane anakubali ikikaribia muda anasema kapata dharura iwe kesho, nk, mwezi sasa yuko ivyo na hatujaonana japo sio mbali. Nimejiongeza kuwa kashaniacha ila kashindwa kusema kuwa kaniacha.

Sasa mapenzi naona niwaachie wengine mimi nipambane na malezi ya wanangu tu.
Nimejaribu kutafakari tatizo lipo wapi kwa hao wote , bado cjapata picha kamili nikama umewazungumzia madhaifu yao tu yakwako umeyaficha nikisoma uzi wako unaonekana kama wewe nimkamilifu 100% .....je? Nikweli? Eb tusikie na upande wako ili tukushauri vzri au njo PM
 
Back
Top Bottom