Nimegundua mapenzi hayanitaki, ngoja nifanye mambo mengine tu

Nimegundua mapenzi hayanitaki, ngoja nifanye mambo mengine tu

Nina miaka 34 sasa nikiwa mama wa watoto 3, hakika sina budi kukubali kuwa mapenzi hayanitaki tena hayanipendi kabisaa, japo niliyapenda na kuyapa thamani katika maisha ila nimeangua sina budi kuyaacha rasmi kuanzia leo.

Historia yangu kwa ufupi,

Mpenzi wa kwanza.

Huyu alinionesha mapenzi ambayo hakika sijawahi kupata, alikuwa mkweli mpole, na mwenye mapenzi ya dhati kwangu, nami nilimpenda sana sana katikati ya penzi zito tukapata mtoto 1 kwa bahati mbaya mpenzi wangu Mungu akampenda zaidi akafariki dunia nikabaki na mtoto.

Ndiyo penzi pekee ambalo sina historia mbaya nalo, penzi hili lilidumu kwa miaka 5 na lilikuwa bado tamu ila ndo ivyo ilibidi nikubali kuwa hayupo na nisonge mbele.

Kimbembe kinaanza.

Mpenzi wa pili


Tulikutana katika mazingira ya kutafuta maisha tukaanza kuwa marafiki baadaye tukawa wapenzi, mapenzi yakaendelea japo tulikuwa na migogoro ya hapa na pale ila tunaongea tunasawazisha maisha yanaendelea.

Kushtuka nina ujauzito, nikamwambia nina ujauzito akasema sasa itakuwa aibu kubwa sana (kipindi hiko yeye alikuwa anasali kanisa fulani na mimi akanikaribisha tusali wote na alikuwa ni mtumishi kanisani hapo) akasema suluhisho ni kufunga ndoa ya haraka.

Tukaongea na wazazi, ndoa ya haraka ikapangwa, akaambiwa atoe Mahari 1,000,000 mimi nikapambana kuwaambia hii ndoa ni ya haraka hasa kuzingatia hali yangu tukichelewa tumbo litakuwa kubwa hivyo kwa sasa uwezo wake labda atoe 200000 tu, na harusi yenyewe ni ya bila sherehe.

Wazazi wakakubali, akaambiwa atoe laki mbili kumbe hana yeye akasema laki basi ikabidi wazazi wapokee tu maana ndoa ishaanza kutangazwa, harusi ikafungwa bila sherehe.

Baada ya ndoa, ilikuwa ni migogoro kama tunaigiza sinema ndani, yaani ni ugomvi kila kikucha kila siku tunasuluhisha kesi, tukipatana na siku 3 zilizobaki ugomvi, na magomvi yenyewe hata hayama maana ni ya kijinga tu hata aibu kumwambia mtu kuwa hiki ndio cha nzo cha magomvi yetu.

Ikawa kama muujiza tukafanikiwa kutulia kama mwaka nikabeba mimba nyingine nikajifungua mtoto wa 3, tukaanza kulea mtoto mchanga amani tunacheka.

Mara vita ikaanza tukarudi kugombana, hatuelewani mara siku niko kwenye kazi zangu natumiwa sms KUANZIA LEO MIMI SIO MUME WAKO TENA, nataka kumuoa Fulani( huyu dada alikua mchepuko wake) na aliwahi kuwa saabu ya mpasuko wa ndoa yetu kwa sehemu kubwa.

Nikapaniki nikarudi nyumbani nalia kama nimefiwa, basi aliporudi akanambia chukua nguo zako sepa, nikasema siondoki, kipigo nilichopigwa sitasahau nusu anitoe uhai.

Nikaondoka, nikaenda kwa ndugu, akaitwa hakuja, kupigiwa simu akasimamia uamuzi wake kuwa ndio kaamua kuniacha, nikaomba watoto akanipa nikaanza kuishi na watoto peke yetu na hata sijui alipo maana aliamua kuhama na simu kabadili namba.

Baada ya mwaka 1 nikampata mpenzi 3

Maisha ya mapenzi yakaanza penzi likachanua mpaka nikaona angalau dunia ni nzuri penzi likawa tamu, tukapanga mipango ya kuishi wote, na yeye ndio alioanzisha jambo hilo wala sikumwambia kuhusu kuishi wote.

Baada tu ya kukubali kuwa tuanze kuishi wote akaanza kuwa busy hanitafuti iwe kwa simu au sms, ukipiga simu hapokei, sms hajibu, unaweza tuma sms ya kumsalimia asubuhi ikajibiwa usiku, ukipiga simu anaka, au hapokei hata siku 3 na akipokea anakwambia nisubiri kidogo nitakupigia ndio imetoka hadi kesho upige tena, ukimuuliza kama kuna tatizo anajibu hamna, ukimuuliza kama kakuchoka anajibu hapana ila kazi nyingi.

Ukimwambia tuoanane anakubali ikikaribia muda anasema kapata dharura iwe kesho, nk, mwezi sasa yuko ivyo na hatujaonana japo sio mbali. Nimejiongeza kuwa kashaniacha ila kashindwa kusema kuwa kaniacha.

Sasa mapenzi naona niwaachie wengine mimi nipambane na malezi ya wanangu tu.
Mmmh sasa wewe unakubali kuzalishwa tu na kila unaekutana nae, lazima wadau waingie mitini

Lea tu mamaa.
 
Pole sana dear. Achana na habari ya kupata mume au mtu utakaeishi nae lea watoto wako. Wanaume wengi wataogopa kuanzisha maisha na wewe kwa kua yna watoto kadhaa tayari.
 
Inawezekana wewe mwanamke una mapungufu ambayo mwenyewe huyaoni kama ni mapungufu.

Kwanza unapenda lawama/kulalamika/kusononeka kwa vitu visivyo na msingi.

Pili, inawezekana ni aina ya wale wanawake ruba/ving'ang'anizi muda wote unataka uwe na mume kwapani. Hutaki kumpa mume muda wa kufanya kazi zake.

Tatu, unaishi katika wakati uliopita pindi unapopata mpenzi mpya, una demand awe kama mpenzi wako wa kwanza. Akufanyie mambo ambayo ulikuwa ukifanyiwa kabla ya kuwa na mtoto/watoto.

Unaweza kuwa na miaka 34 au hata 40 na bado ukawa hujapevuka kifikra
 
Dah dada yangu ukweli mchungu ila kwa watoto 3 kusema kirahisi utapata mume wa kuishi naye,nikutahadhalishe unawezajikuta umekuwa chombo cha burudani.

sisi wanaume tuna ufala mwingi sana linapokuja swala la kuchukua utelezi,tunaweza ahidi chochote tu.
 
Halafu mwanangu wewe kauzu sana ujue[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hebu subiri kwanza, hivi nawe upo kwenye lile kundi la walioamua kutuchukia?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hebu subiri kwanza, hivi nawe upo kwenye lile kundi la walioamua kutuchukia?
Mwanamke ni mama
Mwanamke ni dada
Mwanamke ni binti
Mwanamke ni mchumba
Mwanamke ni mke.

Mimi nawapenda sana wanawake.
Ninawaheshimu sana wanawake.

Lakini haiondoi ukweli kuwa kuna wanawake hatari kuliko hatari yenyewe
Espy Atoto
 
Mwanamke ni mama
Mwanamke ni dada
Mwanamke ni binti
Mwanamke ni mchumba
Mwanamke ni mke.

Mimi nawapenda sana wanawake.
Ninawaheshimu sana wanawake.

Lakini haiondoi ukweli kuwa kuna wanawake hatari kuliko hatari yenyewe
Espy Atoto
Ooooh!! Hapo sawa.

Hata nyie ni hatari rafiki, si unaona hadi mdada wa watu kayaaga mashindano!! Unafikiri mchezo!! Sema tu huwa tunawahiana, ukiwahiwa ndio basi tena.

Ila daah tumeifanya dunia kuwa ya ajabu ajabu sana.
 
Ooooh!! Hapo sawa.

Hata nyie ni hatari rafiki, si unaona hadi mdada wa watu kayaaga mashindano!! Unafikiri mchezo!! Sema tu huwa tunawahiana, ukiwahiwa ndio basi tena.

Ila daah tumeifanya dunia kuwa ya ajabu ajabu sana.
Uko sahihi ni mimi na wewe ndiye tunaifanya hii tasnia ya mahusiano kuwa chungu au tamu
 
Japo Ni one sided story,
Ila Hapa Kuna vitu unatufichwa,
Kwanini utaji sababu ya ugomvi kila Mara.

"Baada ya ndoa, ilikuwa ni migogoro kama tunaigiza sinema ndani, yaani ni ugomvi kila kikucha kila siku tunasuluhisha kesi, tukipatana na siku 3 zilizobaki ugomvi, na magomvi yenyewe hata hayama maana ni ya kijinga tu hata aibu kumwambia mtu kuwa hiki ndio cha nzo cha magomvi yetu"
 
Ktk story yako umesema Mwanaume wa kwanza mlipendana Sana, mkazaa na bahat mbaya akafariki.
Kisha ndo ukaenda kuolewa na Mwanaume wa pili.

Hapa naweza kuhisi kilichokua kinawagombanisha,
Kwamba Kuna namna ulikua unajikuta umemkosea kwa kauli zako, hasa hasa za kumlinganisha na marehemu baba wa mtoto wako kwa kila analofanya.

Hii Kitu Ni mistake Kubwa Sana mnayofanya single mothers mnapoingia kwenye mahusiano mapya mkiwa bado mlikua mnamapenz na baba wa mtoto.
 
Cha kukusaidia Ingia kwenye Maombi huenda hujapata mtu sahihi muombe Mungu akupe
 
Mtoa mada,
Kuachana na Mapenzi haiwez kua suluhisho.

Umeandika mengi ila sijaona ulipoomba wanaume mliotofautiana nao wakwambie Tatizo lako Ni Nini.

Inaonekana unadominate Sana ugomvi au mjuaji sana kias ya mtu kuona Bora akuache na ujuaji wako, asikueleze mapungufu yako.

Sio kwa Nia mbaya,
Ila UKWELI Ni kwamba single mothers wengi mnashindwa kuendana na mahusiano mapya kwa kuweka Watoto wenu Kama vipaumbele vya mahusiano na kuwalinganisha wapenz wenu na baba Watoto wa wenu.

Hii Kitu inawafelisha Sana,
Na wengi mnakosea Sana ktk hili bila kujijua, ndo maana Unaweza tamka Kitu ukihisi Cha Kawaida. Ila sisi tukakichukulia kwa uzito na kikatukera Sana.

Na ukikirudia rudia kila Mara,
Hupelekea moyo wa mapenz kwako kufa kabisa.
 
Japo Ni one sided story,
Ila Hapa Kuna vitu unatufichwa,
Kwanini utaji sababu ya ugomvi kila Mara.

"Baada ya ndoa, ilikuwa ni migogoro kama tunaigiza sinema ndani, yaani ni ugomvi kila kikucha kila siku tunasuluhisha kesi, tukipatana na siku 3 zilizobaki ugomvi, na magomvi yenyewe hata hayama maana ni ya kijinga tu hata aibu kumwambia mtu kuwa hiki ndio cha nzo cha magomvi yetu"
Ni mgomvi huyu mwanamke...anakiri wazi kuwa walikuwa wanagombania vitu vidogo. Kwa taarifa kwa wanawake wote...mwanaume hapendi mwanamke mgomvi hata siku moja
 
Kushtuka nina ujauzito, nikamwambia nina ujauzito akasema sasa itakuwa aibu kubwa sana (kipindi hiko yeye alikuwa anasali kanisa fulani na mimi akanikaribisha tusali wote na alikuwa ni mtumishi kanisani hapo) akasema suluhisho ni kufunga ndoa ya haraka.
Wakija wenyewe watasema umekashifu imani kumbe mtumishi ndiye amekashifu
 
Back
Top Bottom