Nimegundua mpenzi wangu aliwahi kutoa mimba akiwa chuo

Nimegundua mpenzi wangu aliwahi kutoa mimba akiwa chuo

Mimba ikitungwa ndo kiumbe hai huzaliwa. Yai la kike na mbegu za kiume zikikutana ndo kiumbe hai kinazaliwa......

Hili swali lako halina tofauti na mtu aliyekuwa anaviringisha tairi la gari akaanguka akasema kapata ajali ya gari.
Huu uzi nyie ma last born hauwahusu kabisa
 
Daima mkuki huwa mtamu kwa nguruwe lakini kwa binadamu huwa mchungu sana. Ungehesabu ulizini na wasichana mara ngapi kabla ya kuoa na kisha ukaimagine kila ulipozini ulisababisha mimba na zilitolewa, basi ungekuwa mnyenyekevu kwa kutambua ni kwa kiasi gani umekuwa mharibifu na mdhambi pengine kuliko hata huyo mdada aliyetoa mimba 2! Pathetic men. Ubinafsi ndio dhambi yenu kuu!!
Wewe Ni mpumbavu Sana unatetea ujinga,we ni feminist,pyschologically we ni mwanamke jeuri.
 
Umefanya maamuzi mapema mno. Issue ya kutoa mimba kwa wanachuo sio jambo la kushangaza mpaka uamue kuvunja uchumba. Maisha ya chuoni kwa wanawake ni harsh sana. Kama hukuwa na ugomvi wowote mwingine naye bi afsi naona umefanya mamuzi mabaya.
[emoji28][emoji28]aiseee we kijana Yani mtu ashatoa MIMBA then nn unataka kunegotiate nayee, Tena katoa MIMBA akiwa naye kwa mahusiano.

Mkuu ni kweli hata sie wanamme tunamakosa ila CHEATING sio jambo dogo na kutoa MIMBA ndo mbaya kabisaa, kama angekuwa mstaarabu angekuambia huo uovu then we ndo ujue kama unamsamehe au vipi, Sasa kaficha then umejua,

Je ni MIMBA ngapi ambazo katoa na kasita kukuambia??
 
Mm nikiwa mbeya 2018 nilimpa bint wa knyakyusa mimba nilimuambia asitoe kwan mm nitalea na nitakuoa akagoma akalia kbsa kuwa itakuwa vigumu yey kubak na hyo mimba kwan wazaz wak Ni wa Kali hvy tukaenda kwa dokta kuflash alikuja. Kuolewa lkn mpk leo ajapata mtot nikikumbuka maneno yangu huwa anawasawas Sana na hata hvyo bwana aliyemuoa alimkuta na mtot jamaa Ana mzengenya sana amekosa amani Sana
 
Acha kutetea upuuzi, na kashamuacha sasa unaamuaje? Ukichukia kufa!
Mtaacha sana wanawake, ila Hilo ni jambo la kawaida hata aliyekuleta ukute alishatoa nyingi tu wewe hujui, hafu hata masturbation ni dhambi ya uuaji, soma biblia uone, hata hao wake zenu wa ndoa ndio vinara kwa kuchoropoa mkigombana mara kwa mara, acheni kujiona malaika nyie
 
Sasa mimi siwataki hao 'wengi', nataka wachache wasiotoa mimba, na nitawapata kwa gharama yoyote.

Mistake ni kwako na si kwangu. Kifupi ndio nishamuacha sasa, unaamuaje? Ikikuuma na ufe!
Wengine hutoa hata hawasemi na hutakaa ujue, so hata ndoani atatoa tu hata single mother wanaoamua kuzaa before hutoa nyingi tu mzee. So hili swala haliongelewi ila 99% washafanya kimya kimya na wewe unajifariji tu moyoni
 
Huyo mnamhukumu kwa kuwa amekuwa mkweli na muwazi. Unajuaje huyo mpya akayekuja kumuoa yeye ametoa mimba ngapi? Ukitafuta mwanamke malaika wa kuoa, dunia hii hutaoa kabisa. Alikosea kama wengine na bado anaweza kuwa mke mzuri tu!
Mdogo wangu acha kusikiliza ushauri soft huu,huyo kamalicheat usimfukuze tu mshushie na kipigo kikali
 
Mkuu hivi hizi p2 hazina madhara kweri kwa wadada huko mbeleni?
P2 zinafanya kazi kwa kukwangua mji wa mimba ili lile yai lililorutubishwa lisipate pa kujishika. Na hivyo mimb inashindwa kuishi.
Ukizitumia mara kwa mara baadae unakuwa na mji wa wimba wenye kuta legevu zisizo imara kuishikilia mimba.

Na hapo ndipo mwanamke anakuwa ameingia kwenye changamoto za kushindwa kuzaa.
Ndio maaana wanawake wengi siku hizi kuzaa ni changamoto kwao.
 
Nimejifunza jambo, Kwamba Wakati Mwingine inabidi utumie lugha ambayo unayezungumza naye atakuelewa Kwa Urahisi. Nafikiri unatatizo Kubwa sana kwenye KUFIKIRIA BILA MIHEMUKO NA LENGO LA KUHUKUMU. Jifunze kutazama mambo Kwa Uhalisia bila kuweka hisia na ubinafsi.Huku Ukiwa unajificha kwenye nadharia hasi ya "UANAUME" .
Moja wewe Una Ujinga wa KUHUKUMU. Mfano unaposema
( wewe huna familia na hujui namna bora ya kuanzisha familia ) tayari umeni hukumu
Hili tatizo nafikiri ni mpaka uende kwa Njia za Mafundisho ya Kiimani ndo utaweza Kuelemika na kuwa HURU.
Pili umeudhiirishia umma namna idea zako kuhusu Ndoa na Malezi zilivyo MBAYA hasa Karne hii ya 21 Kwa kufikiria Kwamba mwanamke unamwoa kwa ajili ya Kuzaa na kukulelea watoto kwa kauli hii ni kama hujui JUKUMU LAKO KWENYE MALEZI kwamba watoto hulelewa na wazazi na sio mzazi. Mfano unaposema
(na kukulelea wanao )
Tatu Hujui unasimama kwenye nini na haya ni madhara ya Kutanguliza hisia, sikuwa mjinga kukuambia ujitazame wewe kwanza kabla ya kujipa mamlaka na mihemuko ya Historia za wengine. Mfano hapa unaposema;

(zingekuwa za huyu kusingekuwa na lawama kosa lingekuwa alitoa mimba so tungeshauri namna ya ku-solve tatizo)
Huu ni Unafiki wa hali ya juu...Kumbe wewe Mimba yako kutolewa ni Swala linalosameheka UMEKUWA KITUKO! mkuu
Nne Wewe Sasa nimegundua Afya ya Akili yako haiko sawa Kwani umeshindwa kutambua mimi nimekuwa nikisimamia nini kutoka mwanzo mpaka sasa Nakukumbusha Tena Msimamo wangu ni Huu WEWE HUNA mamlaka ya KUHUKUMU vinginevyo na wewe matendo yako pia yaanikwe tukupatie nawewe Hukumu yako...Japo ni dhahiri kupitia maneno yako tu HALI YAKO NI MBAYA!
Mwisho Kabisa Sifaa kuu ya Kuwa mwanaume ni Kuweza kumfanya Mwanamke Na Mtoto katika Jamii nzima wawe salama. Bila kujali ni wa nani.
Na Hapa hujui lolote kabisa, Kulingana na haya maneno yako mwenyewe unaposema.................................................sifa za dada zako kwenye post zako mbili hapo juu zisikutoe kwenye rail ya uanaume,mwanaume anayefikiria sawasawa anaweza kukufikiria vibaya........ )
Jifunze KUONGOZANA na Mwanamke na Sio kuwaburuza kwa mawazo ya kishenzi na Kibaguzi huku ukijilinda na kutoruhusu kuonekana kuwa kama binadamu wa kawaida hujakamilika. Hakuna mwanamke Asiyekuwa Mke bora Shida ni kuwa Jamii imejawa na Wanaume ambao vichwa vyao ni vibovu, Wanao fikiria kutembea na Wanawake wengi sana ili mwisho wakaoe Bikra. Kiukweli HUFAI KUWA KIONGOZI! Hata wa maisha yako binafsi...
 
Kutoa mimba ni kujiwekea laana. Tena ametoa mara mbili.. Hiyo laana itamtafuna kizazi hadi kizazi.

Raha ale yeye huko, makombo ampelekee mwana.
Labda Nikuulize Swali....Mimba ni matokeo ya Nini?
Alilala peke yake kisha Asubuhi akajikuta nayo?

Huu mjadala kuna baadhi ya watu mnajiweka eneo la utakatifu kisha mnaweka HUKUMU bila kutazama pande zote.

Uhalisia ni Hivi Mwanaume akikataa Mimba yake hana tofauti na Mwanamke aliyeitoa Kwa sababu wote wanakwepa jukumu la Malezi.
 
Back
Top Bottom