NIMEGUNDUA: Mtoto wa Kitanzania hawezi akanyooka kimaadili kwa kumuhutubia tu kwa maneno

NIMEGUNDUA: Mtoto wa Kitanzania hawezi akanyooka kimaadili kwa kumuhutubia tu kwa maneno

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Nina watoto wangu wawili mmoja ana umri miaka 17 mwengine miaka 15. Watoto hawa nimekua nikitumia nguvu nyingi sana kuzungumza nao, kuwa karibu nao na kuwaelekeza katika maadili sahihi na tabia njema za maisha bila mafanikio yeyote. Wananisikiliza kwa makini lakini baada ya hapo ni kama vile hatujaongea kitu.

Sasa bwana wiki iliyopita nikajaribu kubadilisha mbinu, nilitumia lugha kali ya kuwatikisa kidogo pamoja na bakora na matokeo chanya nimeanza kuyaona tena makubwa tu.

Hakika nawashauri wazazi wenzangu haya mambo ya kuzungumza na watoto ni mambo ya wazungu sio uku kwetu. Uku Tanzania, ni kuwagombeza na kuchapa tu ndo jambo lako litaweza heshimiwa!!!
 
Ni kweli kiboko kina fix baadhi tu ya mambo, lakini yapo mengi sana haiwezi kufix au kumbadilisha mtu.

Na ndio maana Neno linasema.

" Kama kenge aweza kubadili rangi ya ngozi yake, ndipo na nyie mlio zohea kutenda maovu mtaweza kujibadili na kuacha"
 
Sio watoto tu Tanzania hii ukiwa mstaarabu kuanzia kazini na mtaani utapata shida sana na mambo kukugomea ila ukiwa mkali mambo yataenda, na hata kazini ukiwa boss ukawa fair watakuharibia kazi dawa ni kuwa na roho mbaya watu watakuheshimu.
In short bongo watu ni ka punda hawaendi bila mjeledi
 
Hapo "kazini" nakuelewa sana
 
Shida ni kwamba umechelewa sana, mtoto analelewa kuanzia miaka 0-5/6 baada ya hapo hakuna kitu unaweza kufanya kumbadilisha.

Inaelekea kulingana na maelezo yako wewe ni Psychopath na wazazi au mzazi mmoja ni psychpath na ulilelewa kikatili pia ndio maana una ukatili na hauna huruma hata kwa damu yako mwenyewe.

Unapaswa utambue mtoto siyo mali yako ni binadamu mwenye haki sawa na wewe, ukilielewa hilo labda ukichaa wako utapona/pungua!
 
Sio watoto tu Tanzania hii ukiwa mstaarabu kuanzia kazini na mtaani utapata shida sana na mambo kukugomea ila ukiwa mkali mambo yataenda, na hata kazini ukiwa boss ukawa fair watakuharibia kazi dawa ni kuwa na roho mbaya watu watakuheshimu.
In short bongo watu ni ka punda hawaendi bila mjeledi

ujumbe huu uwafikie watanzania wote...

Mtanzania utamuweza tu kwa fimbo, tofautu na hapo watakuonea sana aisee..
Tanzania hata ukitaka ufanikiwe kwenye biashara zako kuwa katiri kwa wafanyakazi wako, Tanzania ukitaka kufanikiwa kazini kama bosi kuwa na roho mbaya kazi zitaenda...
 
Yes watanzania tumezoea shida na shuruba, ukiwa fair utanyewa Hadi mdomoni huku ukiharibikiwa mambo yako
 
"Imefika wakati tuondoe viboko mashuleni"
😂😂😂Kama vile nawaona walimu wanavyoniangalia
 
Mmenikumbusha Bi. Mkubwa Mama Karim, aieee ukifanya kosa bora uende ukalale polisi.
Bibi mkubwa alikuwa ananipiga kinoma sio kwamba alinionea, hapana kuna makosa nilikuwa natafanya huku nikujua kabisa hili ni kosa.
Mzee wangu alikuwa hana noma, ili Mama Karim akikiwasha ndio balaa hata akina Donnie Yen, Jet Lee sijui akina John Cena wakasome.
Bi mkubwa alikuwa anapiga sio mchezo, yaani mpaka leo nimekuwa mtoto mwema.

R.I.P Mama
 
Yes watanzania tumezoea shida na shuruba, ukiwa fair utanyewa Hadi mdomoni huku ukiharibikiwa mambo yako
Sio tu kazin hata kwenye mahusiano usipokuwa mkali na msimamoo wa kiumeni na roho ngumuuuu utanyewa mdomoni
 
Back
Top Bottom