Kama nilivyosema hapo juu, Njia zinazotumika kufikia subconscious mind ni meditation, mindfulness,therapy na ndoto,
ila hii ya ndoto haitumiki sana maana ndoto huja randomly na hazina formula. Watu wameshindwa kuzicontrol na kuchagua waote kuhusu nini.. wameshindwa kuzielewa na kisayansi imechukuliwa ndoto ni kama makapi ya processes za kazi za ubongo zisizo na maana yoyote.
Mimi nimegundua mbinu rahisi ya kucrack hizi ndoto ili kuuelekeza ubongo ukuambie nini kupitia ndoto.
Njia ya kupitia ndoto.
Kwasababu subconscious mind ni kubwa sana na huwezi kuifikia yote, kwenye hii njia ya ndoto unachofanya ni kutarget unataka ufikie jambo gani ndani ya akili Yako.
Fikiria tu kwenye ufahamu wako wa kawaida, je unaweza kuvifikiria vitu vyote unavyovijua kwa wakati mmoja? Yani kuanzia kumbukumbu zako zote unazokumbuka,hisia,maarifa,ujuzi,Imani zako zote??
Jibu obviously ni hapana Kwasababu unaweza kufikiria jambo moja tu kwa wakati mmoja, na mambo unayoyajua ni mengi sana Yani kama wazo moja ni tone basi ufahamu wako wote ni Kama bahati ya Pacific.
Sasa kama ufahamu wa kawaida (wenye 5%) ni mkubwa Hivyo, vipi kuhusu huu ulio chini ya fahamu? Ambao ni zaidi ya 95% ya akili Yako?
Hivyo hauwezi kuifikia wote lakini unaweza kuchagua parts unazotaka kuzifikia (kama unavyochagua jambo la kufikiri au kukumbuka katika ufahamu wa kawaida) kupitia ndoto.
Pia unaweza kutoa au kuingia vitu kwenye subconscious mind Yako. Kutoa ni Ile kuextract information unazotaka kujua kwa kuuliza maswali, na kuweka ni kama unataka ubadilishe ufahamu wako wa kawaida kupitia subconscious mind Yako.
Tumia hizi steps.
*Vifaa ni simu yenye charge na earphones tu
1. Chagua topic au kitu unachotaka kuifikia kwenye subconscious mind Yako. Mfano, nataka kutoa kitu (kujua ni mwanamke gani alinifaa kuliko wote niliodate nao?)
2. Rekodi voice note fupi (isizidi sekunde 20) ukielezea au kuuliza topic uliyochagua kwa kujitaja taja jina. Mfano (February, Kati ya Jeni na Aisha ni yupi anakufaa? Wewe February, Ni Binti Aisha? Au ni Jeni? February umesikia? Ni Jeni au Aisha?)
Hakikisha unaongea slowly polepole kwa sauti ya upole. Halafu ongea huku unarudia rudia maneno.
ila Isizidi sekunde 20-30.
3. Weka hiyo voice note iwe inaplay kwa kujirudia rudia (loop) halafu weka earphones masikioni kisha lala vizuri kwenye mto kwa pozi ambalo hazitotoka usiku.
4.Ukifanya Hivyo lazima utaota ndoto kuhusu hayo maneno uliyorekodi. Ikumbuke hiyo ndoto uamkapo, ifikirie mara mbili maana hiyo ndoto huja na majibu ya kitu ulichosikiliza usingizini.
Leo ni siku ya 4 nafanya hivi kwa topics mbalimbali, nimegundua vingi sana kuhusu maisha yangu. Nitatoa ushuhuda baadae
Natumai wapo mtakaojaribu, msisahau kuleta mrejesho. Asanteni.
Subconscious
Superconscious...
Hizo level mbili ni za kibabe.
Umejaribu na kueleza jinsi ya ku direct ndoto ambazo zenye asili ya ku play back mambo yenye mjumuisho wa siku nzima. Ambazo based on inputs za siku husika au zile zilipita.
Kuna sombdy humu aliwahi pia kuongelea jinsi ya kuziongoza ndoto zako. Ila hizi ndoto zipo za aina nyingi kulingana na Source.
1. Work of mind. Ambapo kila information unayo iona na kuisikia ,hata kama ilikuwa miaka saba iliyopita. Our brain inaweza ikahifadhi kitu hata utachi kion kwa mara moja tu kikakaaaa. Sema jinsi ya kuki retrieve ndio maarifa ya conscious yamekwama. Wapo wanao weza na ndio tunaona wana kumbukumbu au geniuses. Ila wapo wanaoamin wana shida ya memory basi wanausemesha ubongo kuwa hii taarifa ipuuze weka ktk recycle bin. Sasa ndoto za Work of the mind unaweza kuziongoza kila hisi kabisa kwa method ya kucheza na input.
2. Ndoto za asili ya kiroho kabisaaa. Purely spiritual. Tukumbuke sisi ni roho tulio vaa miili. Na kuna roho zingine like Angels walio umbwa na kuwa assigned kabisa kufanya task zetu,kutusaidia na kutu tumikia. Usipo wapa task ya kufanya wanaboreka.
So unapo ingia ktk deep thinking, kitacho gusa hisia zako za ndani kabisa, moyoni mwako, hapo unaingia ktk masafa ya kiroho. Deep thinking wengine wanaipata kwa Chanting ( Maneno ya kurudia rudia). Wengine maneno ya kuambiwa, kama Hivyo recording zako unazo zitumia, ni kama chanting. Ambapo una activate masafa ya Rohoni na unaingia ktk actions.
Mimi nikitafakari jambo sana, nikionyesha concern basi nnapata majibu haraka sana tena kama ktk ndoto au thoughts za muda huo huo. Na kuna muda unaweza pata matokeo,ambayo unashindwa kujua hizi mbinu nimejifunza wapi. Hata Déjà Vu zinatokea humo.
Tunapolala roho zetu zina jimwaya ktk natural state yake ya haina mpaka wa muda, mazingira nk. Ukiruhusu itaweza kukuonyesha mengi inayo observe, kuanzia yaliyo tokea zamani, wanayo fanya watu muda huoo au hata kuweka ushirika na roho zingine ( Viumbe vingine vya rohon na kuja kulink na Conscious yako).
Ukifanya kila siku utakuwa unaishi ktk conscious sana, na mengine latest ya rohon ambayo roho yako inataka ku fetch utakuwa unayakosa. Mbali na recordings pia unaweza kufanya yafuatayo
1. Jiulize maswali wewe, binafsi kuhusu mambo yako, wewe ni nani, nini nataka, jambo gani ni muhim sana kwangu ktk majira haya, watu gani niwatoe etc Onyesha concern ktk hayo maswli connect vyema utapata majibu.
2. Tumia peni na karatasi. Mimina nafsi yako, sema yale unawishi, tafakari kama karatasi, kama unaona mind yako inatawanyika ukiwa unafikiria hewani hewani.
3. Unaweza omba msaada kwa MUNGU,muombe akufunilie kitu fulani, ongea kama unavyoongea na rafiki Yako. Ukiamini kuwa yupo Pembe yako, yaaani vyovyote vile lakni ukiamini kuwa yuko anakusikia na ukiomba tegemea anafanya.
NOTE
*Usiwe mtu wa kuchezea Simu nusu saa kabla ya kulala.
* Asubuhi usikurupuke kutoka kitandani, tulia hapo until consciousness yako ichukue ya ndotoni, otherwise Fwaaaaa yameenda.
*Usikurupuke kuchezea simu wkt wa kuamka, amka. Nenda jiandae, vaa. On your way out ndio unaweza chezea simu ( sio ngumu ukitaka).
* Usiamshwa na alarm ya simu,anza ku practice kujiambia nataka kuamka saaa fulani utaamka.