Nimegundua rasmi kumbe shetani ni binadamu wala si pepo kama wengi tulivyokaririshwa

Nimegundua rasmi kumbe shetani ni binadamu wala si pepo kama wengi tulivyokaririshwa

Shetani nae huwa anachat na utalielewa hilo ukisoma post zake ndani ya hoja za wachangiaji.
 
Hapo kwenye progress sijaelewa

Na mwili ni zawadi au roho ndo zawadi?
Mwili (body) ni zawadi......

Kumbuka zawadi ni kitu special unachopewa, sio kila mtu anacho.

Roho kwa muktadha huu sio zawadi sababu kwenye maisha kabla hatujaja hapa duniani (Pre Earth life) tulikua tuko na roho.....

Tulikua kiroho kule,kwa lugha rahisi tulikua na roho bila mwili....

Kumbuka hata kwenye movies wanajitahidi ku portray roho ....unakuta wanaonesha mtu amelala akafa alafu kama kivuli kinatoka kwenye mwili.

So roho inaweza kuwa portrayed kama frame ya mwonekano wako bila mwili.

Na ndo tulivyokua kule mbinguni kabla hatujaja duniani,wote tulikua tuna mwonekano huu tulio nao lakini hatakua na mwili.

Kuna siri kubwa ya kuwa na mwili huu (phyisical body), hata YESU KRISTO ilibidi nae aje apate mwili huu wa kibinadamu ili aweze ku progress ( kwenda mbele,kupanda daraja la utukufu).

Kifupi lucifer na malaika wenzake waliadhibiwa kwa kutokupewa mwili huu wa nyama na mifupa tulio nao...mpaka leo wako kwenye form ya roho chafu,ndo hawa wanaitwa marhuani, maimuna, hizi ndo roho za uzinzi,wizi,etc ni roho zote zinazoingia ndani ya wanadamu, zipo zinazunguka zunguka kutafuta miili ya kuingia maana hawakupewa privilege ya kupata mwili.

Kama unakumbuka kuna tukio kwenye Bible kama wewe ni mkrito,kuna mtu alikua ana mapepo na hizi roho chafu....alipomuona YESU KRISTO zile roho zikaomba ruhusa zikasema "Turuhusu tutoke ndani ya huyu mtu tukaingie kwa wale nguruwe " (Marko 5:1-20)

Ukiwa na mwili huu wa nyama na mifupa, na uki complay sheria za Muumba basi unaweza kufuzu ukapata Mwili usiokufa...ambao YESU KRISTO na watakatifu wengine wanao....

Mwili wa milele,mwili usiokufa wala kuumwa......(UZIMA WA MILELE).

Nitaendelea kama kutakua na swali.
 
Nimekuwa nikitafta namna ya kumhoji shetani!

Lakini rasimi kafunguka! Kasema kwamba baadhi ya mambo mengi binadamu tunamsingizia shetani!

Mfano:

  • Anayekufunga kwa hira ni Binadamu mwenzako tena kutwa yupo kanisani
  • Anayewanyima haki binadam wenzake ni binadamu huyuhuyu aliyeapa kwa katiba
  • Anaekuwangia usiku ni binadamu anaetumia wanyama kama paka n.k
  • Anaekugongea mkeo/ mmeo ni binadamu kama wewe
  • Anarkuzungusha kukupatia huduma kwenye ofisi ya Umma ni binadamu mwenye moyo na damu
  • Huko hospital anaemtelekeza mgonjwa wako ni huyo binadamu
  • Anaekuombea njaa ni binadamu shetani yeye anasema ni mtu wa bata
  • Anaekunyima Uhuru wa habari ni binadamu kama wewe
  • Mabaya yote tunayoyaona yanatoka kwa binadamu wenzetu wenye moyo na damu n.k
Shetani anasisitiza, Kama ilivyo KISU kwenye kesi za mauaji, Mwenye makosa siyo kisu bali Ni BINADAMU!

Laiti kama KISU kikitumika sawasawa hakina MADHARA!

Ndivyo ilivyo kwa Shetani! Anasema hana shida na mtu! Bali ni sisi wenyewe Binadamu HATUJIELEWI!

Shetani anasema yeye Hapendi SHIDA! Yeye ni kama Nyundo ya FATUMA! ni maamuzi ya BINADAM kujengea au kubomolea!

Ni hayo tu shetani kasema na mm!
Kwani shetani mwenyewe anasemaje?
 
Dhambi nyingi tunzozifanya wanadamu kwa 99% ni sisi wenyewe yaani ziko ndani ya utashi wetu zinatokana na miili yetu.
Dhambi zote zatokana na haya.
1. Miili yetu. ( external factor)
2. Nafsi. Intenally
3. Shetani
Sasa kwenye mwili kuna kuzini, kuabudu sanamu, kutamani, n.k n.k hapo shetani yuko pembeni anakuangalia umchague yeye au Yesu ingawa atajitahidi akushawishi ila mwenye uamuzi ni wewe.

Nafsi. Pia dhambi zake zatokana na kukosa imani, n.k

Sasa kwa shetani ni hatua ya mwisho huko kwingine umekushinda sasa unakutana na hili joka lenyewe. Mfano Yesu alishinda dhambi zote na kikwazo cha mwisho ilikua ni kwa shetani mwenyewe kumjaribu siku 40. Sawa sawa na kwa mitume wengine manabii n. K
 
Mwili (body) ni zawadi......

Kumbuka zawadi ni kitu special unachopewa, sio kila mtu anacho.

Roho kwa muktadha huu sio zawadi sababu kwenye maisha kabla hatujaja hapa duniani (Pre Earth life) tulikua tuko na roho.....

Tulikua kiroho kule,kwa lugha rahisi tulikua na roho bila mwili....

Kumbuka hata kwenye movies wanajitahidi ku portray roho ....unakuta wanaonesha mtu amelala akafa alafu kama kivuli kinatoka kwenye mwili.

So roho inaweza kuwa portrayed kama frame ya mwonekano wako bila mwili.

Na ndo tulivyokua kule mbinguni kabla hatujaja duniani,wote tulikua tuna mwonekano huu tulio nao lakini hatakua na mwili.

Kuna siri kubwa ya kuwa na mwili huu (phyisical body), hata YESU KRISTO ilibidi nae aje apate mwili huu wa kibinadamu ili aweze ku progress ( kwenda mbele,kupanda daraja la utukufu).

Kifupi lucifer na malaika wenzake waliadhibiwa kwa kutokupewa mwili huu wa nyama na mifupa tulio nao...mpaka leo wako kwenye form ya roho chafu,ndo hawa wanaitwa marhuani, maimuna, hizi ndo roho za uzinzi,wizi,etc ni roho zote zinazoingia ndani ya wanadamu, zipo zinazunguka zunguka kutafuta miili ya kuingia maana hawakupewa privilege ya kupata mwili.

Kama unakumbuka kuna tukio kwenye Bible kama wewe ni mkrito,kuna mtu alikua ana mapepo na hizi roho chafu....alipomuona YESU KRISTO zile roho zikaomba ruhusa zikasema "Turuhusu tutoke ndani ya huyu mtu tukaingie kwa wale nguruwe " (Marko 5:1-20)

Ukiwa na mwili huu wa nyama na mifupa, na uki complay sheria za Muumba basi unaweza kufuzu ukapata Mwili usiokufa...ambao YESU KRISTO na watakatifu wengine wanao....

Mwili wa milele,mwili usiokufa wala kuumwa......(UZIMA WA MILELE).

Nitaendelea kama kutakua na swali.
Mkuu uko vizuri asante

Na ukifa unaenda wapi kwa mtazamo wako, maana hakuna aliyekufa akarudi
 
Shetani =ujinga
mwenyeziMungu yupo.mungu mwenyewe
Shetani sio kiumbe halisi
 
Mkuu uko vizuri asante

Na ukifa unaenda wapi kwa mtazamo wako, maana hakuna aliyekufa akarudi
Asante kwa swali....naomba nitoe mtazamo wangu kama ulivyoniuliza na ni ruksa kwa mwingine pia kutoa mtazamo wake upon this matter.

Ni huwakweli huwa tunasema hakuna binadamu aliyekufa akarudi,lakini tunasahau kwamba YESU KRISTO alizaliwa,akaishi kibindamu kama mimi na wewe akafa akapaa na akarudi tena duniani....Well,inawezekana ukawa sio muumini sana wa kuamini biblia.....wala inaweza ikawa sio mtu wa imani imani hence naomba nitoe mtazamo wangu,je mtu akifa anaenda wapi???

Mtu akifa,mwili wake unaachana na roho....tunasemama roho inatoka.

Ndo nikatoa mfano hapo juu kwamba movies nyingi wanajaribu kuonesha hii...kuna kivuli kinatoka kinaacha mwili .

So roho inatoka inaacha mwili,so tuliobaki duniani tunabaki na mwili ,tunaenda kuuweka kaburini ukaoze huko.

Roho haifi, roho ikitoka inaenda sehemu iitwayo "ulimwengu wa roho",sio mbinguni kama wengi wanadhaniavyo.

Ulimwengu wa roho (spirit world),upo hapa hapa duniani...YES! ,upo hapa hapa duniani lakini hatuwezi kuuona kwa maaana ya kwamba hatujaruhusiwa kuuona only zile roho zilizotangulia ndo zinaonana .....

Hapa nakubaliana na waislamu na watu wengine huwa wanaamini roho ya marehemu inakua bado iko nyumbani kwake ama eneo alilokua anaishi...na huwa wanasema ana uwezo wa kuona watu wakilia na waliokuja msibani lakini hana uwezo wa kuongea nao.

Kuna movies nyingi pia zime portray hii kitu kuna moja siikumbuki jina kuna sehemu wanaonesha watu waliokufa wakiwa kwenye ulimwengu wao pamoja na walio hai...alafu yule aliyekufa akataka aongee na walio hai lakini kuna mlinzi wa kule ulimwengu wa roho akamwambia "it is forbidden for the living to speak with the dead"

Ngoja ntatafuta jina la hiyo movie.

So kifupi kuna kitu kiitwacho ulimwengu wa roho (Spirit World [emoji289])ambao roho za waliokufa zipo kwenye ulimwengu huo na kuna mambo mengi yanaendelea kwenye ulimwengu wao huo.

Kwa sisi Wakristo tunaamini baada ya YESU KRISTO kufa pale msalabani ,watu walikuja wakashusha mwili msalabani,wakaupeleka kaburini alafu roho ya mwamba ikatoka ikaenda ulimwengu wa roho kuhubiria zile roho ,
naomba ninukuu hii verse toka kwenye biblia 1 Petro 3:18-20 "

"Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu.
Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho; na kwa maisha yake ya kiroho [ alikwenda kuwahubiria wale roho waliokuwa kifungoni.] Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina'

Na tunajua pasi na shaka Alihubiria hizi roho wa siku 3.......

Baadae alivyomaliza Roho yake ikarudi ndani ya ule mwili kule kaburini na kukawa na tukio la ufufuko.

Ndo mana wakristo wengi wanaamini kwenye kufufuka siku ya tatu...

Note:Hizi siku tatu YESU hakwenda mbinguni, alikua kwenye ulimwengu wa roho akihubiria roho zilizopo huko.

Na kwa uthibitisho kwamba hakwenda mbinguni bali alikua ulimwengu wa roho akichapa kazi angalia alivyomjibu magdalena pale kaburini,

Naomba ninukuu, Yohana 20:17

Yesu akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”

So kifupi mtu akifa Roho inaenda ulimwengu wa roho,na mpaka sasa kwenye ulimwengu wa roho kuna roho nyingi sana zipo zikisubiri ile siku zirhusiwe zirudi kwenye miili yao kule makaburini ili ziweze kufufuka na kupata hukumu.,kifupi zinasubiri parapanda ambayo ndugu zetu waislamu huwa wanasema "siku ya kiama",

Na kwa kiuhalisia,haujawahi kusikia stories mtu anaonana na baba ake au mama ake aliyekyfa siku nyingi ndotoni au wakati mwingine anamuona kakaa kwenye kochi pale kwao,au wakati mwingine unajikwaa njiani bila kuona kilichokugusa.

Wakati mwingine hizi roho huwa zinaruhusiwa na MOLA kuja kuonana na wapendwa wao au kuwapa maelekezo muhimu.

Ila zipo na tuko nazo hapa hapa duniani ,hatuzioni maana hatujafunguliwa macho kuonana nazo.

Nitaendelea kama kutakua na swali.
 
Back
Top Bottom