Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwili (body) ni zawadi......Hapo kwenye progress sijaelewa
Na mwili ni zawadi au roho ndo zawadi?
Kwani shetani mwenyewe anasemaje?Nimekuwa nikitafta namna ya kumhoji shetani!
Lakini rasimi kafunguka! Kasema kwamba baadhi ya mambo mengi binadamu tunamsingizia shetani!
Mfano:
Shetani anasisitiza, Kama ilivyo KISU kwenye kesi za mauaji, Mwenye makosa siyo kisu bali Ni BINADAMU!
- Anayekufunga kwa hira ni Binadamu mwenzako tena kutwa yupo kanisani
- Anayewanyima haki binadam wenzake ni binadamu huyuhuyu aliyeapa kwa katiba
- Anaekuwangia usiku ni binadamu anaetumia wanyama kama paka n.k
- Anaekugongea mkeo/ mmeo ni binadamu kama wewe
- Anarkuzungusha kukupatia huduma kwenye ofisi ya Umma ni binadamu mwenye moyo na damu
- Huko hospital anaemtelekeza mgonjwa wako ni huyo binadamu
- Anaekuombea njaa ni binadamu shetani yeye anasema ni mtu wa bata
- Anaekunyima Uhuru wa habari ni binadamu kama wewe
- Mabaya yote tunayoyaona yanatoka kwa binadamu wenzetu wenye moyo na damu n.k
Laiti kama KISU kikitumika sawasawa hakina MADHARA!
Ndivyo ilivyo kwa Shetani! Anasema hana shida na mtu! Bali ni sisi wenyewe Binadamu HATUJIELEWI!
Shetani anasema yeye Hapendi SHIDA! Yeye ni kama Nyundo ya FATUMA! ni maamuzi ya BINADAM kujengea au kubomolea!
Ni hayo tu shetani kasema na mm!
Mkuu uko vizuri asanteMwili (body) ni zawadi......
Kumbuka zawadi ni kitu special unachopewa, sio kila mtu anacho.
Roho kwa muktadha huu sio zawadi sababu kwenye maisha kabla hatujaja hapa duniani (Pre Earth life) tulikua tuko na roho.....
Tulikua kiroho kule,kwa lugha rahisi tulikua na roho bila mwili....
Kumbuka hata kwenye movies wanajitahidi ku portray roho ....unakuta wanaonesha mtu amelala akafa alafu kama kivuli kinatoka kwenye mwili.
So roho inaweza kuwa portrayed kama frame ya mwonekano wako bila mwili.
Na ndo tulivyokua kule mbinguni kabla hatujaja duniani,wote tulikua tuna mwonekano huu tulio nao lakini hatakua na mwili.
Kuna siri kubwa ya kuwa na mwili huu (phyisical body), hata YESU KRISTO ilibidi nae aje apate mwili huu wa kibinadamu ili aweze ku progress ( kwenda mbele,kupanda daraja la utukufu).
Kifupi lucifer na malaika wenzake waliadhibiwa kwa kutokupewa mwili huu wa nyama na mifupa tulio nao...mpaka leo wako kwenye form ya roho chafu,ndo hawa wanaitwa marhuani, maimuna, hizi ndo roho za uzinzi,wizi,etc ni roho zote zinazoingia ndani ya wanadamu, zipo zinazunguka zunguka kutafuta miili ya kuingia maana hawakupewa privilege ya kupata mwili.
Kama unakumbuka kuna tukio kwenye Bible kama wewe ni mkrito,kuna mtu alikua ana mapepo na hizi roho chafu....alipomuona YESU KRISTO zile roho zikaomba ruhusa zikasema "Turuhusu tutoke ndani ya huyu mtu tukaingie kwa wale nguruwe " (Marko 5:1-20)
Ukiwa na mwili huu wa nyama na mifupa, na uki complay sheria za Muumba basi unaweza kufuzu ukapata Mwili usiokufa...ambao YESU KRISTO na watakatifu wengine wanao....
Mwili wa milele,mwili usiokufa wala kuumwa......(UZIMA WA MILELE).
Nitaendelea kama kutakua na swali.
Asante kwa swali....naomba nitoe mtazamo wangu kama ulivyoniuliza na ni ruksa kwa mwingine pia kutoa mtazamo wake upon this matter.Mkuu uko vizuri asante
Na ukifa unaenda wapi kwa mtazamo wako, maana hakuna aliyekufa akarudi