Pamoja na kuguswa na tukio hili na maumivu tuliyo nayo kwa kupoteza ndugu zetu..tuwe wakweli, unasifia watu ambao wanaweza kuongeza tatizo lililotokea..ajali zinapotokea ni muhimu sana kuelekeza watu wakae mbali na tukio hadi pale watu wenye ujuzi,
uwezo na utaalamu wafike eneo la tukio kwa ajili ya uokozi, ajali ya mv bukoba ilipotokea waliosababisha meli izame ni watu ambao wala hawana utaalam wowote wa uokozi waliamua kuitoboa meli upande wa juu hewa ikaingia ndani within 20 minutes meli ikazama chini, wataalam walisema kama meli isingetobolewa kulikuwa na uwezekano wa meli kuelea hata siku mbili..lakini lipo jambo jingine,
ukiacha kazi zingine za uokozi kuna namna hata vile majeruhi wanastahili kubebwa, mfano mtu amepata dislocation ya uti wa mgongo then watu wasiojua namna ya kumbeba wanammbeba, hata kama damage ya mgongo ilikuwa inaweza kutibika waliombeba kwa sababu hawajui majeruhi abebwe namna gani wataongeza tatizo pengine la kumfanya majeruhi asipate tiba ya kumponyesha.
Tusaidiane kutoa elimu kwa watu wanaokuwa karibu na ajali inapotokea wapime kiwango cha usaidizi wanachoweza kutoa ili wasiongeze madhara zaidi ya chombo au madhara kwa majeruhi, vinginevyo wakae pembeni wasubiri wahusika wa uokoaji wafike.