Ajali zinapotokea zinataka utulivu na subra kidogo ili uokozi ufanyike pasi na kuleta madhara zaidi..papara na haraka haraka mara nyingi zinaongeza madhara.
Ni kweli kwamba kunahitajika utulivu na maarifa wakati wa dharura, lakini jiulize hao wataalam unaosema walikuwa wapi! hadi wavuvi na wananchi wa kawaida wakafika kwanza?
Tunahitaji kuwapongeza wananchi kwa jitihada zao.
Kilichotakiwa ni Wataalam kufika kwanza ili kuwaongoza wananchi, kwa bahati mbaya hawakuwepo.
Ingalikuwa ni ujinga kuwatazama watu wanatapa tapa eti wakisubiriwa wataalam ambao hatujui kama wapo.
Tatizo ni kutokuwa na maandalizi ya dharura na akili zetu Waafrika na sisi Watanzania ni kutojifunza.
Meli ya MV Bukoba ilitosha kutufunza kwamba lazima tuwe na kikosi cha uokoaji 24/7 katika ziwa Victoria.
Bukoba kuna Bandari na kiwanja cha ndege kama ilivyo Mwanza.
Kulitakiwa kuwe na kikosi cha uokozi kikiwa tayari saa 24 kwa wito wa dharura.
Sijui kama kipo na kama kilikuwepo kikowapi hadi wavuvi watangulie!
Gharama za kikosi cha uokoaji ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya V8 zinazozunguka nchini.
Tunawezaje kuwa na Helicopter ya kutangaza sensa lakini hatuna boti ya uokozi wakati wa dharura
Dodoma kila anayesimama anapongeza huduma nzuri za jamii !!
Ni mwendo wa mapambio na kujikomba tu, eti leo tuwalaumu wavuvi kwa kujitoa!
Dodoma hakuna anayefikiri dharura hata siku moja, kila mmoja akikamata kipaza sauti ni kusifia tu.
Kesho utasikia wanatoa rambi rambi, hawa ndio wakuwaambia wakae kimya siyo wavuvi waliojitolea
Ninyi wa Dodoma msitutie kichefu chefu wakati huu wa msiba , msitoe rambi rambi wala msiongelee ajali ya ndege, endeleeni na mapambio na kusifia, mafao yenu yapo salama, tuacheni tuomboleze ndugu zetu!
Haya hayapaswi kutokea miaka 60! Ni aibu sana.
JokaKuu Pascal Mayalla Mag3