Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mumgu awabarikiView attachment 2408768
Habari kubwa leo ni ajali ya ndege ya Precision iliyotumbukiwa ziwani Viktoria huko Bukoba...
Pamoja na kuguswa na tukio hili na maumivu tuliyo nayo kwa kupoteza ndugu zetu..tuwe wakweli, unasifia watu ambao wanaweza kuongeza tatizo lililotokea..ajali zinapotokea ni muhimu sana kuelekeza watu wakae mbali na tukio hadi pale watu wenye ujuzi...
Mara nyingi..Mkuu ulishawahi kupata ajali
Ushauri wa kiboya sana, kwa hiyo wavuvi wangesubiri uokozi kwa kusubiria wataalam na vifaa toka GGM na kagera sugar?Pamoja na kuguswa na tukio hili na maumivu tuliyo nayo kwa kupoteza ndugu zetu..tuwe wakweli, unasifia watu ambao wanaweza kuongeza tatizo lililotokea.....
Ajali gani unaongelea..ajali zinafanana? Ajali ya Lori ya mafuta petrol imeanguka na mafuta yanamwagika ni sawa na ajali ya costa imeanguka..wewe unaona zinalingana?Uliokolewa na madaktari?!
Mtaalamu wetu ukiwa kazini...Pamoja na kuguswa na tukio hili na maumivu tuliyo nayo kwa kupoteza ndugu zetu..tuwe wakweli, unasifia watu ambao wanaweza kuongeza tatizo lililotokea..ajali zinapotokea ni muhimu sana kuelekeza watu wakae mbali na tukio hadi pale watu wenye ujuzi...
Hapa inazungumziwa ajali ya ndege ya leo bukoba.... Ushauri wako ndo huo?Ajali gani unaongelea..ajali zinafanana? Ajali ya Lori ya mafuta petrol imeanguka na mafuta yanamwagika ni sawa na ajali ya costa imeanguka..wewe unaona zinalingana? Kutoa usaidizi kwa chombo na majeruhi kunafanana? Ndio maana nimesema watu wapime kiwango cha kutoa msaada kutokana na mazingira ya ajali.
Huelewi chochote bora kukaa kimya..hata ndege ilivyoundwa haiwezi kuzama kama inavyoonekana ikiwa tu milango itabaki imefungwa, kinachoonekana ndege yote imefunikwa na maji kasoro upande wa nyuma, nini kimesababisha ifunikwe na maji?Ushauri wa kiboya sana, kwa hiyo wavuvi wangesubiri uokozi kwa kusubiria wataalam na vifaa toka GGM na kagera sugar?
Kuna mtu angenusurika?
Je tuna team gani ya uokozi?
Tanzania ni yatima wenyewe wanahudumiana wazazi na viongozi ni wafu kiutendaji
Unataka kusema mlango ulifunguliwa na wavuvi??Huelewi chochote bora kukaa kimya..hata ndege ilivyoundwa haiwezi kuzama kama inavyoonekana ikiwa tu milango itabaki imefungwa, kinachoonekana ndege yote imefunikwa na maji kasoro upande wa nyuma, nini kimesababisha ifunikwe na maji?
Nimetoa mfano wa mv bukoba waliosababisha meli izame na idadi kubwa ya watu ni wale waliwahi kutoboa upande mmoja bila kujua madhara yatakayotokea..au wewe hata kama unaokoa mtu mmoja ni sawa halafu 20 wanakufa bado utasema umesaidia? Mambo ya kusema utamaduni kusaidiana yana mahali pale si kila tukio lazima usaidie pima pia msaada unaoutoa unaweza kuongeza madhara..Mtaalamu wetu ukiwa kazini...
Mkuu yaani unamaanisha hata wale wavuvi pale wamefanya MAKOSA kuwaokoa wale watu 26? Je wangekaa kusubiri wapewe maelekezo na wataalamu hata hao 26 wangeokolewa?
Ajali yoyote ikitokea popote iwe ya gari, ndege au meli ilimradi iwe eneo lenye kufikiwa na jamii fulani ya watu basi kwa tamaduni zetu zenye upendo huwaga si rahisi kutoshiriki katika uokozi wowote ule endapo Kuna uwezekano.
Hizi Siasa za sijuie mifupa utapata dislocation sijui waokoaji wanaweza sababisha madhara mengine nadhani ni vitu minor Sana kikubwa kinachoangaliwa ni msaada...
Imagine leo waliopanda ndege wameokolewa na wavuvi Tena wanaotumia vifaa vya ki local Kama mtumbwi ya makasia huku ndege yenyewe ikivutwa na kamba ya manila na haohao watu haohao ambao si wataalamu na hawakusubiri maelekezo ya kitaalamu.
Haya uliyoandika ungemwandikia niliyekuwa namjibuHa
Hapa inazungumziwa ajali ya ndege ya leo bukoba.... Ushauri wako ndo huo?
Wataalam watasema kama wavuvi ndio waliofungua milango, mimi sijui aliyefungua milango, abiria au wavuvi..Unataka kusema mlango ulifunguliwa na wavuvi??
Kuzama kwa ndege kulisababishwa na hewa iliyokuwa ikiingia ndani ya ndege kupitia mbele ambako ndege ilijipigiza...hata ule mlango wa nyuma usingefunguliwa bado ndege ingezama tu kwakuwa teyari maji yalianza kuingia kupitia mbele.Huelewi chochote bora kukaa kimya..hata ndege ilivyoundwa haiwezi kuzama kama inavyoonekana ikiwa tu milango itabaki imefungwa, kinachoonekana ndege yote imefunikwa na maji kasoro upande wa nyuma, nini kimesababisha ifunikwe na maji?
Pamoja na kuguswa na tukio hili na maumivu tuliyo nayo kwa kupoteza ndugu zetu..tuwe wakweli, unasifia watu ambao wanaweza kuongeza tatizo lililotokea..ajali zinapotokea ni muhimu sana kuelekeza watu wakae mbali na tukio hadi pale watu wenye ujuzi,
uwezo na utaalamu wafike eneo la tukio kwa ajili ya uokozi, ajali ya mv bukoba ilipotokea waliosababisha meli izame ni watu ambao wala hawana utaalam wowote wa uokozi waliamua kuitoboa meli upande wa juu hewa ikaingia ndani within 20 minutes meli ikazama chini, wataalam walisema kama meli isingetobolewa kulikuwa na uwezekano wa meli kuelea hata siku mbili..lakini lipo jambo jingine,
ukiacha kazi zingine za uokozi kuna namna hata vile majeruhi wanastahili kubebwa, mfano mtu amepata dislocation ya uti wa mgongo then watu wasiojua namna ya kumbeba wanammbeba, hata kama damage ya mgongo ilikuwa inaweza kutibika waliombeba kwa sababu hawajui majeruhi abebwe namna gani wataongeza tatizo pengine la kumfanya majeruhi asipate tiba ya kumponyesha.
Tusaidiane kutoa elimu kwa watu wanaokuwa karibu na ajali inapotokea wapime kiwango cha usaidizi wanachoweza kutoa ili wasiongeze madhara zaidi ya chombo au madhara kwa majeruhi, vinginevyo wakae pembeni wasubiri wahusika wa uokoaji wafike.