Nimeguswa na wale wananchi waliookoa watu ajali ya ndege

Huu ushauri unatuhusu sisi watanzania au nchi za UK na Marekani??

Watu wanaokuwaga wa kwanza kufika eneo la tukio ni wale walio karibu na tukio, achana na hilo kuna maeneo vifaa vya hao wataalamu kama magari ( kama tukio ni la moto).

Unaona mtu chuma limemwangukia kinachotakiwa ni mshirikiane kuliinua mumtoe ama lah mumuache liendelee kumgandamiza mkisubiri wataalamu, nyumba inaungua moto na ndani kuna watu wasioweza kujiokoa na uwezo wa kuwakoa mnao, ila mnasubiri wataalamu waje kuokoa ilhali uwezo huo mnao.

Ingekua tunaweza kujua ajali itatokea wapi huo ushauri wako ungewezekana lakini ajali haifahamiki itatokea wapi, hata kama huna ujuzi yule muhanga utakua umemsaidia sana" sometimes kinachoua sio majeraha ya ajali bali ni hofu/mshtuko/ kukata tamaa ya kusaidiwa so mtu akiona msaada haijalishi wa nani basi nae atajitutumua asife mapema.

Jiografia ya nchi yetu ni ngumu kutegemea wataalamu mkuu, lakini pia ajali zipo za aina nyingi ni ipi ufundishe na ipi uache. Na ndio maana general knowladge huwa inatolewa sometimes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…