Kwanza nikujibu post yako ya 92 tabia ya kutoroka kwenye mada na kuanza kuongelea mtu aliyetoa maoni au hata kutoa lugha isiyo na staha ni kukosa nidhamu binafsi na kuheshimu mawazo ya wengine..hakuna anayekuja kuandika hapa kwa lengo la kubomoa kupitia matukio kama haya tunataka kujenga ili yanayoonekana ni mapungufu yarekebishwe..pili kwa suala la mv bukoba kujua nani alitoboa sidhani ina uzito, sabab sote tunajua meli ilitobolewa ikazama, na hakuna mahali nimesema wavuvi ndio walitoboa, lbd uonyeshe hiyo post, tatu hakuna mahali nimeandika kikosi, kwa anayesoma kwa lengo la kuelewa ataona maana ya kile ninajaribu kujenga na si kubadilisha maneno, nikisema hata polisi mmoja au wawili wakifika kwenye tukio hicho si kikosi..mambo ya kujifunza ni mengi ikiwemo kukubali ukweli kama ulivyo, mara nyingi inapotokea hali km hii wengi wanatetea kile walichofanya watu ni sahihi na serikali imeshindwa kufanya sehemu yake kitu ambacho si kweli wakati mwingine, huko nyuma utamaduni huu wa watu kusaidia matukio ya ajali ulileta malalamiko hasa pale watu wanaowahi kwenye tukio pamoja na kusaidia wengine wanafanya uhalifu, wanasachi mifukoni mwa majeruhi au kuchukua vitu vya majeruhi na hapo ndipo inakuwepo haja ya kusubiri ili angalau wanausalama wafike kwenye tukio ili wasimamie uokozi wa awali, si wote wanaweza kuwa wema kufanya uokozi wengine wanakuwa wamepata nafasi ya kufanya uhalifu pamoja na uokozi..tukio la morogoro ajali ya Lori la mafuta ni mfano wa haya ninayosema. Kutukana watu usiowajua kisa tu wametofautiana na wewe kufikiri ni hulka mbovu kabisa na sijui kwa nini watanzania wengi matusi ndiyo maneno mepesi kusema badala ya kutoa hoja na mifano..tuelimishane kwa staha ili kujenga, that's all.