Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Giza kwa giza uponyaji wake ni wa muda mfupi, giza na mwanga ndiyo dawa pekee
 
Hapo uliposema mpanagi mmoja ndiyo alikua anafuatiliwa hukaweka bayana babu yake alivyokuja akafanyaje sasa
 
Kuna mtumishi wa Mungu mmoja namjua ni rafiki yangu sana sana, kuna eneo nilimpatia aweke makazi alikutana na vimbwanga sio mchezo, alikua anasikia sauti na vishindo nje ya nyumba, na ilifika mahala walikua wanatokea na watu live yani live jicho kwa jicho lakini hakuacha kuomba
 
Hizo ni imani tu na wenge lenu usiku

Hakuna kitu kama hicho (uchawi) uyo mtoto aliyekuwa kipofu, kiziwi nk apelekwe hospitali utapewa chanzo na nini kifanyike
Hayajakukuta siku yakikukuta ndio utaelewa waafrika ni watu wa namna gani
 
kuna jamaa mmoja jirani yetu alikua na kacheo fulani uko mkoani Mara sijui alifanyaga kitu gani ila alilogwa alikuaga anakunya mawe yamoto walihangaika sana bila tiba mpaka walipofilisika nayeye akafa ndo niliamini uchawi upo
 
Sisi wenyewe tulishamfanyia baba mdogo vimbwanga ili ahame alipokua anaishi kinyume na sheria mpka leo anaamini ni uchawii na huwezi mbadilisha....kumbe wajuba tulitupia mashuka meupe na nukuchezea akili yake tu
 
Chadema na ACT wanalialia kila siku wanonewa na CCM
Kwanini kwa miaka yote CHADEMA CUF na ACT wasitafute wachawi na wakawatumia kuwaroga vingozi wakubwa wote wa CCM wakafa
Na wakati huo huo CCM nao kwanini wasiwaroge viingozi wakubwa wa CHAADEMA CUF ACT ambao wamekuwa wasumbufu na badala yake wanawaua kwa risasi na kuwateka kama vile Lissu au Ben 8
Swali kama uchawi una nguvu na upo kwanini mtamia njia ngumu kama hizo
 
Sasa wewe MUHA una chale mpaka za unyolo unategemea watakugusaje. Wakati wanakuona untouchable.
Siyo untouchable; ukijisajili unakuwa mwanachama wao, na wanakutumia kwenye misheni na mikakati yao ya giza. Usitegemee Shetani akawa na uadui na agents zake. Hawa wanakuwa na uhasama na wale wanaowapinga -- watu wale ambao wako chini ya UFALME WA NURU.
 
Mwambie kwanini watu hawajaenda Lwangwa kupiga kampeni, unajua hao wanapinga wanakuwa ni mawakala tena wachawi wakubwa wanapumbaza ili watu wasijue siri zao, wenyewe ni waturutumbi wakubwa kabisa

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Hahahah kuna maeneo yamoto sana, huko kuna kamati za hali ya juu katika ufalme wa giza😂😂😂
 
Umeongea point kubwa sana wengi wanaosema kuna uchawi wanakuwa wameathirika kiakili
Mm siwezi kuogopa kitu ambacho kwnza hakipo na hakina nguvu mpk ukiogope au kikutie hofu ndio kifanye kazi huoni hapo ni psychological disoder na wala sio uchawi
Haupaswi kuugopa uchawi kwa vyovyote vile, kwa sababu hata ukiuogopa huwezi kuudhibiti kwa hofu yako. Hofu na woga vinamfanya mtu awe vulnerable zaidi. Hii ni njia ambayo wengi huitumia kukutisha ili utafute ulinzi kwenye himaya yao ya giza. Hakuna eneo lolote la mwili wa mwanadamu asikoweza kushambulia Iblisi. Anashambulia akili, nafsi ya ndani ya roho na hisia, na mwili. Na anafanya kirahisi na kiustadi mkubwa, ukiwa mbishi huwezi kudhani ni nguvu ya giza. Kumkana Shetani kwa akili tu ni kazi bure.
 
Nafunga mjadala uchawi ni imani kama vile uislam au ukristo au budha hivyo haimanishi uchawi una nguvu hapana hizo ni imani
Na imani maana yake kuamini jambo ambalo huna uhakika kama lipo na la kweli that's why wachawi wengi hawafanikiwi kama wanaamini uchawi una nguvunguvu kwawasitumie kupata mafanikio
Uchawi huambatana na Hallucination na Delusion mojawapo ya dalili za shuzophrnia na ili uchawi upate kukupata lazima uwe na hofu kuwa uchawi upo na una nguvu na unaweza kukidhuru
Na endapo usipo kubali kuwa uchawi haupo na akili yako ikawa resist uchawi hauwezi fanya kazi
Hitimisho uchawi ni imani kama vile imani nyingine wala huitaji kuogopa mm nakuja na bastola halafu wewe njoo na uchawi wako halafu tuone nani atakuwa mshindi rejea yaliyotokea vita vya maji maji
Watu walikufa wengi wakiamini uchawi upo wakipigwa risasi wanakufa wakiamini wakisema maji eti risasi zigeuke maji La Haula ni ujinga wa kiwango cha juu
 
Ila yote kwa yote Jamani..ombeni msiwe na mchawi kwenye familia au ndugu wa karibu either wa baba au mama na awe amewaweka kwenye target yake..Jamani..Tushukuru tu nguvu za Mungu zipo.
Mtajuta maisha yote watu wanakuwa wanawaona hamjielewi kumbe kuna mtu kawaweka target, usiombe haya, ukimjua Mungu ndiyo utajua vita hii si yakitoto

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Safi umejibu vzr soma post yangu ya mwisho hapo chini kuhusu yaliotokea vita vya maji maji
 
Uchawi haupo that's why hata wewe huujui
Kama unaujua uchawi naomba unieleweshe uchawi ni nini?
Na nikiuona nitaujuaje?
Ni kama upepo, hauonekani kwa macho, ila athari zake ni wazi kabisa, na zinatambulika. Ndiyo maana uchawi ni nguvu za giza. Imagine mtu anaweza kuhamishwa ndani anakolala, akabebwa kishirikina na kulazwa nje, asubuhi akiamka yuko nje, na milango alikuwa amefunga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…