Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nakumbuka alichanganyikiwa kabisa pale tulipokua kwenye gìza tororo tuna breathe fire kama madragon..kumbe watu tunapuliza mafuta ya taa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Angewarushia mawe kudadeki mngekimbia kama hamna akili nzuri [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],
 
Shetani ana watu wake. Na Mungu anawatu wake. End.
 
Mbona hiyo inafanyika sana tu, aisee! Watu wamshukuru sana Mungu anazuia mambo mengi mabaya ya giza. Vinginevyo ingekuwa mwendo wa kutibuana kwenda mbele.
 
Ngonjera tu hizi..hakuna uchawii
 
Unatakiwa ushike biblia na vifungu vyake [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] iki umjue yesu vizuri
😂😂 Kwa niliyoyapitia mbona nimeshika adabu na vifungu havinipigi chenga sasa hivi..tofauti na zamani huko ...Mungu azidi kutupigania maana dunia hii mmhh
 
Huwezi kuupinga uchawi kwa akili ya binadamu tu. Lazima Mungu ahusishwe, vinginevyo hujipendi. Pili, kuna wachawi maskini na matajiri, watu wa kila aina. Uchawi hautegemea hali ya maisha ya mtu. Hiyo ni nguvu ambayo watu wanaiazima kutoka kwa mfalme wa giza mwenyewe -- Iblisi. Kuhusu "risasi kuwa maji," angalia pia upande wa pili waliokuwa wakipambana nao wamejiandaaje.
 
Wanakuwa washatimba yani..Mie hio hali hunikuta nikiwa Dar. Yani Daslamu ina wachawi kinoma aisee. Kukur kakara za mabati usiku ni kama kazi.
kumbe tuko wengi tunaoathirika na hvyo vitu aisee.
Yaani kila siku saa nane kamili lazima nishtuke halafu baadae unaanza kusikia vitu kama mchanga vinarushwa juu ya bati au vitu kama shanga vinatupwa kwenye sakafu ndani.
Au unasikia nyayo za mtu zinatembea lakini hafiki anakokwenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…