Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nakumbuka alichanganyikiwa kabisa pale tulipokua kwenye gìza tororo tuna breathe fire kama madragon..kumbe watu tunapuliza mafuta ya taa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Angewarushia mawe kudadeki mngekimbia kama hamna akili nzuri [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],
 
Muwe mnasikai tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta.

Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.

Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.

Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa

Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika.
Shetani ana watu wake. Na Mungu anawatu wake. End.
 
Chadema na ACT wanalialia kila siku wanonewa na CCM
Kwanini kwa miaka yote CHADEMA CUF na ACT wasitafute wachawi na wakawatumia kuwaroga vingozi wakubwa wote wa CCM wakafa
Na wakati huo huo CCM nao kwanini wasiwaroge viingozi wakubwa wa CHAADEMA CUF ACT ambao wamekuwa wasumbufu na badala yake wanawaua kwa risasi na kuwateka kama vile Lissu au Ben 8
Swali kama uchawi una nguvu na upo kwanini mtamia njia ngumu kama hizo
Mbona hiyo inafanyika sana tu, aisee! Watu wamshukuru sana Mungu anazuia mambo mengi mabaya ya giza. Vinginevyo ingekuwa mwendo wa kutibuana kwenda mbele.
 
Huwa nawaambia watu uchawi wala siyo wa kujaribisha; unaweza kutumika wewe mwenyewe, tena kimzamzaa tu ikiwa hivyo. Ukweli mchungu ni kwamba hiyo kitu za kishirikina na nguvu za giza hazinaga fomula moja. So unaweza tulifanya hivi ama vile, kumbe nguvu ilitumika kupitia utayari wako. Uwezekano huo upo sana tu. Lakini upande wa pili, mtu anaweza akaamini amerogwa, kweli akaugua akafa!
Ngonjera tu hizi..hakuna uchawii
 
Unatakiwa ushike biblia na vifungu vyake [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] iki umjue yesu vizuri
😂😂 Kwa niliyoyapitia mbona nimeshika adabu na vifungu havinipigi chenga sasa hivi..tofauti na zamani huko ...Mungu azidi kutupigania maana dunia hii mmhh
 
Nafunga mjadala uchawi ni imani kama vile uislam au ukristo au budha hivyo haimanishi uchawi una nguvu hapana hizo ni imani
Na imani maana yake kuamini jambo ambalo huna uhakika kama lipo na la kweli that's why wachawi wengi hawafanikiwi kama wanaamini uchawi una nguvunguvu kwawasitumie kupata mafanikio
Uchawi huambatana na Hallucination na Delusion mojawapo ya dalili za shuzophrnia na ili uchawi upate kukupata lazima uwe na hofu kuwa uchawi upo na una nguvu na unaweza kukidhuru
Na endapo usipo kubali kuwa uchawi haupo na akili yako ikawa resist uchawi hauwezi fanya kazi
Hitimisho uchawi ni imani kama vile imani nyingine wala huitaji kuogopa mm nakuja na bastola halafu wewe njoo na uchawi wako halafu tuone nani atakuwa mshindi rejea yaliyotokea vita vya maji maji
Watu walikufa wengi wakiamini uchawi upo wakipigwa risasi wanakufa wakiamini wakisema maji eti risasi zigeuke maji La Haula ni ujinga wa kiwango cha juu
Huwezi kuupinga uchawi kwa akili ya binadamu tu. Lazima Mungu ahusishwe, vinginevyo hujipendi. Pili, kuna wachawi maskini na matajiri, watu wa kila aina. Uchawi hautegemea hali ya maisha ya mtu. Hiyo ni nguvu ambayo watu wanaiazima kutoka kwa mfalme wa giza mwenyewe -- Iblisi. Kuhusu "risasi kuwa maji," angalia pia upande wa pili waliokuwa wakipambana nao wamejiandaaje.
 
Wanakuwa washatimba yani..Mie hio hali hunikuta nikiwa Dar. Yani Daslamu ina wachawi kinoma aisee. Kukur kakara za mabati usiku ni kama kazi.
kumbe tuko wengi tunaoathirika na hvyo vitu aisee.
Yaani kila siku saa nane kamili lazima nishtuke halafu baadae unaanza kusikia vitu kama mchanga vinarushwa juu ya bati au vitu kama shanga vinatupwa kwenye sakafu ndani.
Au unasikia nyayo za mtu zinatembea lakini hafiki anakokwenda
 
Back
Top Bottom