Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

πŸ˜‚πŸ˜‚ Kwa niliyoyapitia mbona nimeshika adabu na vifungu havinipigi chenga sasa hivi..tofauti na zamani huko ...Mungu azidi kutupigania maana dunia hii mmhh
Halafu ukute kuna mtu eti anatamani arogwe, duh! Si dhani mtu mwenye akili timamu anaweza kusema hivyo!
 
Hio ni sauti ya nyanyo kusota mkuu, yani hawa wase nge huwa natamani kama ningekuwa na bainokolaz niweze kuwaspot na kuwaharibia.

Mie huwa napata hali ya msisimko haswa. Yani nywele husisimka na vipele vya baridi hutokea mwili mzima imefikia stage sizimagi taa usiku. Nikistuka naanza kupiga maombi hadi napitiwa tena na usingizi.
 
kwa hiyo wanaosoma bible ndio hawadhuriki na wachawi?fanya research yako vizuri
Wapi nimesema hivyo? Mantiki ya kusoma Bible na kusali ni kijiondoa kwenye channel za kishetani na kuja kwa Mungu. Unajua mpaka ufanyiwe hivyo hivyo vimbwanga, kimsingi unakuwa umekanyaga waya wa ufalme wa giza, sasa kazi ya agents zake ni rahisi tu ya kuwasha switi tu, unanasa!
 
Sasa kama unajua wanawarithisha why unasema uchawi haupo? Acha kutania watu hapa mkuu.
Kuwarithisha Imani ya kichawi ni kawaida kwa waafrika lakini si uhalisia.

Uchawi ni IMANI, na Imani ni kuamini kitu ambacho yamkini hakipo lakini unaweza kuamini tu huzuiwi na unaweza kuwarithisha kizazi kizazi Imani hiyo hata kama haina uhalisia

Ni sawa na habari ya kusema Mwanamke anambemenda mtoto pale atakapofanya mapenzi na Mwanaume asiye Mume wake kipindi ananyonyesha, Waafrika wanaamini habari ya kubemenda lakini kiuhakisia na kisayansi(ambayo ni uhalisia) hakuna kitu kama hicho.

Sijui kama umeelewa.
 
Dar karibia makabila yote yapo hapo lazima kila mtu aonyeshe ufundi wake [emoji23]

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Dah yani Dar sie ambao hatuko mlengo wa kushoto wala kulia tunanyanyasika sana yani.
Sometimes unatembea koridoni unaingia toilet usiku. Mlangoni unapopita unaskia msisimko wa ajabu.
 
Dah yaani mimi kwa jinsi nilivyowachoka hadi natamani nipande connection za wataalamu kutoka mozambique,nigeria,congo waje kuangamiza hawa washenzi
 
Ila acha woga, mtegemee sana Mungu. Kuna mdada mmoja pia aliwahi kufanyiwa hivyo vimbwanga kama vyako, aliugua sana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…