Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Mbona mkoloni alituchapa viboko na kutubuluza tulishindwa nini kumroga?
 
Hujaweka justification yoyote ya uchawi

Habari ya taifa kutokuwa na hatimiliki ya uchawi umeitoa wapi? Nani kasema hayo?

Umesema Mwanadamu anatumika kama chambo tu, sasa nijibu maswali yangu kinagaubaga ili tuendelee na mada

Uchawi ni nini?

Mchawi ni nani?
 
Uchawi unategemeana na mazingira; kwa wenye elimu kuna uchawi sawa na levels za waelimika; kwa watu wajinga na wasio na elimu pia kuna uchawi unaokubaliana na kiwango na uwezo wa maarifa, imani na fikra zao.
Mmeanza kukizana wenyewe.

Uchawi ni nini?
Mchawi ni nani?

Unakwepa sana hayo maswali mawili, au umeleta mada ya jambo usilolijua.
 
Nadhani hatubishani.

Uchawi ni nguvu za giza (kwa kifupi), ni uwezo zaidi ya ule wa kawaida wa kibinadamu.
 
Kwani wachawi wote wanaroga watoto wao?

Mbona huwa wanawarithisha?
Uchawi haunaga mlango mmoja aisee! Lengo la uchawi ama nguvu za giza ni kuvuruga kabisa mfumo wa dunia, kuwachanganya wanadamu, na kuwaangamiza. Sasa mbinu zinatofautiana. Watoto wanaweza kurithishwa uchawi, au kurushiwa uchawi na jamaa zao. Wanaweza pia kutolewa kafara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…