Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Kuna issue imenikuta juzi kati hapa,akaja Mtu akaniambia nihame au nivute masheikh.

Mie nikaamua kumchana tu Huyo anayesemekana ni muhusika, sijui nitasalimika!
Mbona hamsemiii? Kuna ishu, si useme ni issue gani tutathmini kama ndio uchawi huo tujue?
 
kunywa maji ufunge tu kinywa chako..

huu ulimwengu wenye Imani ya Mungu una shetani pia.
Sio lazima, Mimi sijawahi kumwona Mungu face to face ila nilishaeleza kwanini naamini yupo tena kwa mambo yanayoonekana wazi kwa kila mtu

Sitaki kuelezea kwenye mada hii, ile ni independent.
 
Nishafinywa usiku na mtu nisiemuona, nishapigwa makofi na mtu nisiemuona mchana kweupe nyuma ya nyumba yetu nikiwa nimelala kwenye mkeka, na mwisho tushamdaka mchawi usiku hakuganduka ndani pale sebuleni mpaka shangaz yetu mtaalam alivyokuja kumgandua, na nyumba tuliikimbia baada ya shangaz kusema kwamba tumetangaza vita na wachawi baada ya mwenzao kuaibishwa, na pia yeye hiyo vita haiwezi, ilibidi harudi zake bush, na sisi tukahama ili kukwepa mabalaa, leo hii unaniambia nisiamini uchawi kama upo, ngoja yakukute.
 
Mbona hamsemiii? Kuna ishu, si useme ni issue gani tutathmini kama ndio uchawi huo tujue?
Mawanda ya uchawi ni mapana sana; unaweza kukuta hawa jamaa ambao wao kimsingi ikifika mida yao, kwenye vilinge vyao wanapanga maeneo au mitaa ya kuzunguka kurugaruga.

Wengine uchawi uko katika kuua zaidi, kuroga, kukufanya mgonjwa, kukupoteza ama kupumbaza fahamu na akili, kujipatia mali -- katika wizi, ujambazi, utapeli, nk. Hata katika nyanja za mahusiano ya kimapenzi, unakuta mke au mume ama wapenzi wanamfanyia ushirikina. Ni mambo mengi mengi sana.
 
Msingehama aiseee! Hao kuna nguvu ya kupambana nayo, labda kama nanyi mlikuwa mmejiweka kwenye nguvu hizo za giza. Uchawi upo, lakini hupaswi kabisa kuugopa; wewe ndiye unaweza kuuvuta au kuupinga kulingana na uchaguzi wako mbalimbali. Uchawi na ushirikina na hata nguvu za giza kwa ujumla zina anga zake ("superstition culture"), ambapo ukijiweka hapo ama phisically au mentally/psychologically, tegemea kuteswa au kitumikishwa na mashetani.
 
Sio lazima, Mimi sijawahi kumwona Mungu face to face ila nilishaeleza kwanini naamini yupo tena kwa mambo yanayoonekana wazi kwa kila mtu

Sitaki kuelezea kwenye mada hii, ile ni independent.
Actually, Mungu ni invisible. Mashetani nao ni invisible. Wachawi wanapata hiyo nguvu ya invisibility kutoka kwa huyo bosi wao. Ndiyo maana wachawi wanaoonekana au wasionekane. NaPo inategemea na aina ya uchawi wenyewe kuna grades/viwango mbalimbali.
 
kuna issue imenikuta juzi kati hapa,akaja Mtu akaniambia nihame au nivute masheikh..

mie nikaamua kumchana tu Huyo anayesemekana ni muhusika
sijui nitasalimika..!
Unatakiwa uwe na ujasiri wa Kimungu, hapo unashinda au angalau unakuwa katika mikono salama.

NB: Watu watambue kwamba hii kitu hainaga fomula moja. Ina nyanja kibao tu kama ilivyo idadi ya mashetani nadhani. Kwa hiyo usikariri kwamba mbona hivi, mbona vile. Hii nayo ni elimu ya giza kama zilivyo elimu zingine, na zina mtandao mpana.
 
Kutumia nguvu na muda wako kumuelewesha na kumthibitishia mtu kuwa uchawi upo ni upotevu wa muda na nguvu zako.
Kuna wanaosaidika, wapo wanaoweza kuchagua, kwa sababu wazijuazo wenyewe, kuendelea kubishana na ukuta. Lakini hii kitu iko wazi sana. Wala haihitaji ushabiki kama soka.
 
Ukishampa makavu, wala hakufanyi kitu,
Sema. Mimi mtaa niliokuawa nakaa wachawi walikuwa wengi sana hujui yupi ni yup
Hatari sana. Kila mahali mawakala wa uchawi wameenea sana tu. Lakini mtu hatakiwi kuogopa kwa sababu kuna nguvu kubwa zaidi inayopiku na kunyutrolaizi kabisa uchawi, ushirikina, urogaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…