Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Mkuu hapa unabishana na wachawi wenyewe, wcha kupoteza nguvu zako bure.
Hawajijui wakishapikwa kichawi, ni kama mtu aliyenaswa umeme, mpaka umtegue, vinginevyo ndiyo safari ya maporomoko hadi kuzimu.
 
Unabadilisha magoli. Nimekwambia niroge au tafuta mchawi yeyote aniroge kama huwezi sema huwezi sitaki hizo ngonjera zako.
Nisingekukuta kwenye hii mada ningejinyonga, anyway nasimama kinyume na wewe, kuwa haya mambo yapo, bahati yako I ain't the one, wewe ningeshakufanya yangu siku mingi sana, sahii ungekuwa umekaa zako kwa kutulia.!!
 
kuna mwaka fulani, nilifanya field training kwenye moja ya wilaya ya mkoa wa Morogoro, yaani ile siku nafika usiku wake nikapata jaribio moja kutoka kwa hao watu, aisee nashukuru Mungu huwa siingiliki.
 
Ujasiri wa kimungu haufungamani na mambo ya anasa. Unaweza ukaomba nguvu za kimungu ukazipewa ila the moment umetomb@na au kufululiza pombe basi unarudi kwenye mikono ya watesi wako chap na nguvu zinakuwa zimefifia.

Hapo ndipo ugumu ulipo.
One of the best comment kutoka kwako extro ila edit tu hapo PG language, weka tafsida
 
Nimekuwa mbishi sana lakini uchawi upo wakuu.
Tuuite vyovyote lakini upo sana,,, fuatilia ubishi wangu hapa jf kuhusu uwepo wa Mungu na uchawi lskini leo nakiri kabisa hizi mambo zipo sana
 
Ombea usipitie haya majaribu mkuu.
Ah ah mzee kuna neno uchawi hauendi kwa mental..uchawi ni kama matatizo ya akili huwa hereditary au yanarithishwa..kama kwenye ukoo wenu kuna mchawi lazima nawe uwe au urithi mikoba...hawa waliobaki inategemea umejisogeza kiasi gani kwa hawa wachawi,..ndo maana kuna neno utanirogaje hata kitovu changu hujui nlipokizika,,...
 
Kuna wengine wanadanganya wenzao kuwa hawaamini hii kitu haswa viongozi serikalini....utashangaa usiku hawalali, wako mitaani matako wazi kutafuta maalbino ili wakafanye mambo yao wapandishwe vyeo.
 
Nisingekukuta kwenye hii mada ningejinyonga, anyway nasimama kinyume na wewe, kuwa haya mambo yapo, bahati yako I ain't the one, wewe ningeshakufanya yangu siku mingi sana, sahii ungekuwa umekaa zako kwa kutulia.!!
naomba nroge mimi mama///kikubwa uwe na msambwanda tu
 
Hii ya kutest mitambo ipo Sana na hata sehemu ninayo ishi nikiwa mgeni walikuja hasa ukikaa eneo lenye wenyeji wa asili Wana hizi mambo na wanarogana kwa kwenda mbele. Sijui hupata faida gani?
"Sijui hupata faida gani?" Uchawi ama ushetani lengo kuu ni kumtawala mwanadamu na kumtumia for its own ends. Sasa njia inayotumika ndiyo hiyo ya kutisha, kuhofisha ili ujisalimishe kwenye mamlaka ya giza. Ndiyo maana watu watakwambia, Kazindikwe ili usisumbuliwe! Hicho ndicho ushetani unachotafuta -- kumweka kila mtu kwenye mamlaka yao ya giza. Tambua kuna falme mbili kubwa zinahasimiana -- NURU & GIZA!
 
Anayebisha uchawi haupo hajapigwa dhabau la maana ndio maana hajui kitu. Tuzidishe maombi na sala/Dua kuutokomeza huu ushenzi
 
Hayo ya kurithi mikoba siyaamini japo kuna watu imewatokeaga. Ila kwa jamii yetu uchawi ni wa husda tu kuwa mtu utatusua labda watu wanakupiga kipapai.
 
Unadhani maadui wa maguful tundu Lissu wanafurahi kuwaona wazima
Jaribu kumloga Lissu watu mpk wametumia risasi kwanini wasitumie uchawi kumuua au watu wasiompenda magufuli kwanini wasitumie uchawi kumuua
Kwanini uchawi hauna nguvu kiasi hiko na hiyo nguvu ya uchawi ipo katika gani
 
Kuna wengine wanadanganya wenzao kuwa hawaamini hii kitu haswa viongozi serikalini....utashangaa usiku hawalali, wako mitaani matako wazi kutafuta maalbino ili wakafanye mambo yao wapandishwe vyeo.
True. Na wanaweza kufanikiwa utajiri au nafasi, vyeo, lakini cha moto lazima watapata -- and in many different ways.
 
Sidhani umewaza kwa kina aisee! Ukisema uchawi hauna nguvu, kila mtu atakucheka, na ndicho anachotaka Iblisi uamini kwamba Shetani hayupo, au hana nguvu. Make no mistake about it. Kuna nguvu ya Mungu, ipo nguvu ya giza, likewise!!!
 
mzee wangu aliangushwa kwenye jukwaa la siasa, ilibidi tumuwahi, akafanyiwa Dua ndio akatengemaa, la sivyo familia tungekuwa tunaongea mengine hadi sasa
 
Hayo ya kurithi mikoba siyaamini japo kuna watu imewatokeaga. Ila kwa jamii yetu uchawi ni wa husda tu kuwa mtu utatusua labda watu wanakupiga kipapai.
Kuna watu wanarushiwa uchawi, wanarithishwa au kushikishwa uchawi. Kwa mfano, kwenye familia ya kichawi labda mtoto fulani amekataa au imeshindikana kuurithi kama ndiye aliyeteuliwa, anaweza kuuawa, kuharibiwa akili au maisha, au hata kusumbuliwa maisha yake yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…