Muwe mnasikai tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta.
Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.
Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.
Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa
Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika.