Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nisingekukuta kwenye hii mada ningejinyonga, anyway nasimama kinyume na wewe, kuwa haya mambo yapo, bahati yako I ain't the one, wewe ningeshakufanya yangu siku mingi sana, sahii ungekuwa umekaa zako kwa kutulia.!!

Nitengeneze basi mama lao uwasaidie hawa jamaa hapa wanaopiga porojo tu tukiwaambia waturoge wanaanza kutoa sababu sizizo na mashiko.
 
kwa mtu ambaye hayajakukuta ...kama mambo yako yamenyooka...haujichanganyi na waswahili hasa kwenye mambo ya biashara nk....hautaelewa kama haya mambo yapo

Kwahiyo uchawi upo kwenye biashara tu na kwa waswahili? Kwenye nyanja zingine haupo? Wazungu hakuna uchawi?

Kwahiyo uchawi haupo kama mambo yamenyooka ila yakiharibika ndo kuna uchawi?

Mnatumia nini kufikiri? Mbona kama uwezo wenu wakufikiri mdogo sana kuliko tofali. Tukisema wanaoamini hizi story ni wajinga mtasema tunawatukana.
 
Nitengeneze basi mama lao uwasaidie hawa jamaa hapa wanaopiga porojo tu tukiwaambia waturoge wanaanza kutoa sababu sizizo na mashiko.
Haha.
Nasubiri uje nikuchote nyayo.!!
 
Kinachonifanyaga nisiamini haya mambo ndio hiki. Inawezekanaje mtu anauwezo mkubwa wa kuloga lakini ni kapuku hata mlo mmoja ni shida?
Uchawi ni field nyingine kabisa, na upo wa nyanja mbalimbali. Kuna wachawi hawatakiwi kulala kwenye godoro kulingana na masharti yao. Mwingine hatakiwi kabisa asafiri mchana, na kadhalika. Sasa maskini wa namna hiyo wasioweza kuiba benki, unakuta uchawi wao ndiyo limit yake. Na usikute mchawi kama huyo anamfanyia mipango ya kishirikina mtu mwingine na anakuwa tayari mkubwa kabisa. Sasa ukikuta wa aina hiyo, uchawi wao unakuwa umewafunga hivyo -- anakuwa na nguvu fulani lakini hawezi kuitumia zaidi ya hapo. All in all, hizi idara za nguvu na utendaji wa giza ni countless -- ziko za aina nyingi mbalimbali.
 
au utamkuta mganga mashuhuri eti kakamatwa na polisi hana kibali cha kufanyia kazi, sasa hizo nguvu z giza walizonazo sijui ni za kazi gani km si uongo tu
Kifupi, uchawi unaweza kulinganishwa kwa mfano wa mawimbi ya simu -- ili unase lazima mwili wa yule target uwe kama receiver wa hayo mawimbi ya kichawi, ndipo hiyo mishale ya giza inanasa. Ndiyo maana ni hatari kujiweka kwenye "channels" zinakopita nguvu za giza. That's why ukijiweka kwenye mazingira ambapo unaweza kushambuliwa na mashetani. Shetani na uchawi hukunasia kwenye anga zake.
 
Hio challenge uli toa maelezo haya ?

*majina yako matatu

*majina ya baba yako na mama yako

*tarehe yako ya kuzaliwa

*picha yako

Weka haya maelezo au MPE haya maelezo mtu anayetaka kukuloga halafu uje utoe ushuhuda kama lakini utakua hai
Huyo mtu au hao watu si watumie uchawi wao kuzipata hizo taarifa.

Kama wana uwezo wa kupaa kwa ungo mpaka majuu huko na kukatiza anga za watu bila kuwa detected na radar, wanashindwaje kuzipata taarifa zangu?

Wadukue tu hata akaunti yangu moja ya benki na watazipata hizo taarifa.
 
Kwa mantiki hiyo

Kama Mbowe anaipinga CCM yeye ni CCM

Kama Kiranga hakubaliani na habari za uwepo wa Mungu basi yeye ni mcha Mungu.

Tukisema mambo ya uchawi yanaamiwa na wavivu wa kufikiri na kusambazwa na wajinga mnasema tunawatukana. Kuna ujinga zaidi ya huu?
Unaruhusa kuwaza kwa uhuru, lakini huwezi kupinga nguvu za giza kwa akili yako peke yake. Mambo mengi ya Kimungu na nguvu za giza mara nyingi sana hupingana ama huenda kinyume na logic ya kawaida ya mwanadamu, ndiyo maana wengine wanakataa havipo vitu hivyo. You cannot logically reason about the reality of the existence of God and the devil. Huwa zinakinzana na logic ya mwanadamu, kwa sababu ya ufinyu wa mawazo yetu. Imagine hata kwenye "electromagnetic spectrum," range ya miali tunayoweza kubaini kwa macho yetu tu ni ndogo sana -- visible light, basi. Sasa hatujui ni vitu vingi kiasi gani tusivyoweza kujua, na viko countless.
 
Muwe mnasikai tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta.

Nguvu za giza haziwezi kuonekana kwa macho yetu ya kawaida wala kupimwa na vifaa vya kisayansi, Ni sawa na kurekodi ndoto ya mtu uione kwenye video, haiwezekani, hata mtu akirogwa bado ipo gizani ndio mana hata ukienda hospitalini utaambiwa mashine haziwezi kugundua chanzo cha ugonjwa wako

Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.

Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.

Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa

Hapo zamani sijui kama sikuhizi bado vipo, Mashuleni ya porini huko boarding visa vya wanafunzi kukutana na vibwengo ilikuwa ni kawaida sana

Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika.
Ndo ya Duniani, jikaze tu.
 
Kwahiyo uchawi upo kwenye biashara tu na kwa waswahili? Kwenye nyanja zingine haupo? Wazungu hakuna uchawi?

Kwahiyo uchawi haupo kama mambo yamenyooka ila yakiharibika ndo kuna uchawi?

Mnatumia nini kufikiri? Mbona kama uwezo wenu wakufikiri mdogo sana kuliko tofali. Tukisema wanaoamini hizi story ni wajinga mtasema tunawatukana.
Nguvu za giza ziko kila mahali, aisee! Acha kumtukana huyo jamaa, aisee
 
Muwe mnasikai tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta.

Nguvu za giza haziwezi kuonekana kwa macho yetu ya kawaida wala kupimwa na vifaa vya kisayansi, Ni sawa na kurekodi ndoto ya mtu uione kwenye video, haiwezekani, hata mtu akirogwa bado ipo gizani ndio mana hata ukienda hospitalini utaambiwa mashine haziwezi kugundua chanzo cha ugonjwa wako

Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.

Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.

Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa

Hapo zamani sijui kama sikuhizi bado vipo, Mashuleni ya porini huko boarding visa vya wanafunzi kukutana na vibwengo ilikuwa ni kawaida sana

Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika.
Unajuaje huu ni uchawi na hiki ni kitu ambacho sijakijua tu?

Mababu zetu walioishi miaka 140 iliyopita wangeoneshwa TV na internet leo, wangesema uchawi.

Lakini si uchawi, ni sayansi tu ambayo hawakupata kuijua.

Unahakikishaje hicho unachosema ni uchawi si kitu tofauti tu ambacho hukijui?
 
Hapana. Kama hukuweza kutoa hizo taarifa katika hio challenge yako basi challenge yako ni ya kujifurahisha. Hutoi taaarifa sababu umejificha nyuma ya keyboard, anonymously...na zaidi hutoi taarifa sababu una hofu na unaogopa ndio mana umejificha nyuma ya keyboard huku ukijitapa...na zaidi zaidi hakuna aliyekuja kukudai hizo information sababu hauna faida ya kulogwa, ungekua na kitu cha thamani cha kulogewa hapo sawa, watu wanaloga usiku na mchana kupata pesa, ila wenye akili za kimaskini wanalogana ili kumkwamisha mwingine. Anyway hitimisho, challenge yako ni batili
Bullshit.

Hakuna uchawi.
 
Unajuaje huu ni uchawi na hiki ni kitu ambacho sijakijua tu?

Mababu zetu walioishi miaka 140 iliyopita wangeoneshwa TV na internet leo, wangesema uchawi.

Lakini si uchawi, ni sayansi tu ambayo hawakupata kuijua.

Unahakikishaje hicho unachosema ni uchawi si kitu tofauti tu ambacho hukijui?
Mimi huwa nasema kuwa, madai mengi ya uchawi au mtu kurogwa, most likely huwa ni brain disorders.

Kibongo bongo bado tuko nyuma sana kwenye mambo ya ufahamu juu ya hizo brain disorders.

Kuna brain disorder moja inaitwa Alice in Wonderland Syndrome.

Hii mtu akiwanayo bongo, kwa mfano tu, culprit namba moja atakuwa ni ‘uchawi’.

Fungua hiyo link uone AIWS ni nini na dalili zake ziko je. Mambo ya size distortion, perceptual distortion, time distortion

Halafu nambie kama ikimtokea mtu bongo ataenda spitali kwa psychiatrist au ataenda kwa mganga...

Halafu bongo kuna psychiatrists wa kutosha kweli?
 
Kuna mambo ya kushangaza sana, na mengi hatujayajua bado.

Wengi wetu, hata kabla ya uchunguzi, wanapenda kukimbilia kusema ni uchawi.

Ni aina fulani ya uvivu.

Uvivu mbaya sana.

Uvivu wa kufikiri.
 
Kama unaamini Mungu yupo, Shetani naye yupo, na ndiye huyu chanzo cha nguvu za giza
nimekwambia naamini mungu yupo,,,ila shetani jini sijui uchawi hivyo vyote siamini hata dhambi siamini kama kuna dhambi
 
mnaopinga uwepo wa uchawi mnajifurahisha tu na wala hamna lolote, majuzi tu hapa wife alikua na ujauzito wakagombezana na jirani ajili ya watoto, kilichofuata siku za kuzaa zikapitiliza tukienda hospital akipimwa hamna tatizo, mwisho dokta akanishauri yawezekana kafungwa kichawi hivo akanielekeza nikanunue dawa fulani maduka ya asili, nikaileta akakorogewa akainywa baada ya kunywa hakuchukua muda akajifungua bt cha ajabu mtoto alitoka kazingirwa mfuko wa plastic hii ilozuiwa kutumika, kama hayajakukuta ya ulimwengu chunga sana ulimi kuongea usoyajua.
 
Kuna explanations nyingi sana.

Nitaje mbili tu kwa sasa.

1. Wewe muongo, umetunga hadithi. Vinginevyo, thibitisha. Hii ilitakiwa kuwa habari kubwa sana, lakini hatukuisikia popote.

2. Hata kama wewe si muongo, hakuna kitu chochote ulichoelezea kinachothibitisha uchawi. Kumbuka, kuona kitu ambacho hukielewi kimetokeaje hakuthibitishi kitu hicho ni uchawi. Ukikimbukia jusai huu ni uchawi kwa sababu huelewi kitu tu, huo ni uvivu wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom