Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia


Ni kweli mkuu lakini kuna siasa ambayo ndiyo fimbo kuu sikuhizi kwa kisingizio cha democracy wanayotumia mabeberu wa dunia; haihitaji haraka kuna mambo ya msingi yanafanyika kwanza kabla ya kufikia huko.

Ukiiona Zim aliko comrade mwenzetu si kuwa hakuwa anajitambua kuna kamba wanazotumia wenzetu kukuvuta mpaka wanakufikisha kwenye corner ambayo utakuwa laughing stock na ndipo hutumia crafted democracy kukuondoa...tupo imara na kunasehemu tunaelekea ambapo dunia itatambua hata nchi za weusi ziliwekwa kwenye dunia hii na Mungu ambaye hugawa vipawa bila upendeleo...nimesema na narudia tena hii yetu bado haijaonekana duniani na wakubwa wanaulizana ilikuaje hata wakafanikiwa mpaka sasa?
 
EPA ni Mkataba mmoja. Mibovu mingine nayo iekwe. Hata hivyo EPA mkataba ndio ulikuwa unakwenda kuwekwa sahihi, haujakamilika bado. Naona tunachanganya mada. Huu mkataba ndio ungesainiwa kwa mara ya kwanza.
Maana yangu ni kwamba Tanzania tupo vizuri kwenye mambo ya mikataba kuliko nchi zingine za Afrika Mashariki hadi tuwe viongozi wa kuongoza mkataba huo? Maana kuwa kiongozi unajua/unaweza kuliko wenzako.
 
maana yangu ni kwamba Tanzania tupo vizuri kwenye mambo ya mikataba kuliko nchi zingine za Afrika Mashariki hadi tuwe viongozi wa kuongoza mkataba huo? Maana kuwa kiongozi unajua/unaweza kuliko wenzako.
Wapiga dili akina Lowasa toka waondoke serikalini mikataba mibovu imepungua sana...Lowasa alitutia hasara sana kwenye mkataba wa RICHMOND.
 
Wachache sana watakuelewa mkuu, hii nchi tumechagua ujinga kuwa sehemu ya maisha yetu. No wonder tuliowatuma hawakufanya hata huu utafiti kidogo. Sisi tunatakiwa kujijenga na kufanya vizuri sana kwenye potential zetu hasa kilimo, madini na rasilimali za asili kama gesi na mafuta yakija. Kamwe hatutakuja kushindana na Ulaya kutengeneza magari sana sana walete matawi ya viwanda vyao. Wasomi wetu hawajui hata vitu vidogo kabisa
 

Upo sahihi sana mkuu, kwenye biashara za kimataifa nchi huwa hazishandani kuzalisha kila kitu bali unazalisha kile ambacho kitakufanya uwe na ''competitive advantage''.
Bado ukizalisha unahitaji mahali pa kwenda kuuza hizo bidhaa.
 
Ni vema kufanya hivyo lakini ifike mahala tubadilishe sheria zetu zinazo ongoza michakato ya mikataba yetu ili mikataba hiyo inakuwa wazi na Wananchi wanapewa furusa ya kuijadili ili waweze kunufaika nayo.
Jokakuu: hata sisi kupewa fursa kujua ni sehemu ya kutatua tatizo. Kwa vyovyote ikiwa majadiliano yalikamilika tangu 2014 hakukuwa na sababu ya kuanza kupima tena. Lakini kama wengine hawakujua na sasa wanataka kujua, pengine hii ni nusu shari, na ni bora kuchukua maamuzi baada ya kujua kuliko bila uhakika. Hii ni changamoto kwa uendeshaji nchi kwa usiri.
 
Wewe Joka unauliza
swali la kampeni. Mambo ya ingekuwa mimi ilikuwa mwaka jana. Sasa yupo mtu tunapima kulingana na maelekezo yake. Tunaweza kukataa ama kuridhia bila kuingiza kampeni...
 
Kibiashara inaweza kuonekana tunachelewa, lakini pengine bora kuchelewa kiusahihi kuliko kubahatisha
 
Hang'over ya uchaguzi bado inawaathiri wengi ndio maana hawataki kuyaangalia mambo kiuhalisia,kama yalivyo na kutafakari kwa uamuzi sahihi...ni kama watu wanataka serikali ifanye uamuzi wa hovyo bila kupima ili wapata cha kuzungumza...bila kujua kuwa waathirika ni wananchim wote.Uendeshaji wa serikali una changamoto kubwa sana.
Wewe Joka unauliza

swali la kampeni. Mambo ya ingekuwa mimi ilikuwa mwaka jana. Sasa yupo mtu tunapima kulingana na maelekezo yake. Tunaweza kukataa ama kuridhia bila kuingiza kampeni...
 
Zungu Pule: Soma vizuri post yangu utajua sikusema nimehudhuria mkutano wa wakuu wa nchi..wanachama...hilo ukijibiwa hutahitaji kuuliza mengine
 
Sioni kama tuna la kujisifu katika hili. Kama kwa miaka yote tangu kulipoanzishwa mazungumzo ya mkataba wa EPA tumeshindwa kujua kama kuna faida au hakuna faida, tutaweza kutambua hilo kwa hii miezi michache kati ya sasa na mwakani? Inaonekana sisi hatujua tunataka nini au hatutaki nini.
 
Zungu Pule: Somavizuri post yangu utajua sikusema nimehudhuria mkutano wa wakuu wa nchi..wanachama...hilo ukijibiwa hutahitaji kuuliza mengine

Nadhani kama Taifa tuna tatizo kubwa la kufanya maamuzi. Hata biblia husema ni hatari mwanadamu unapokuwa si moto si baridi. Watanzania hatueleweki, tunashindwa kufanya maamuzi. Kwa karibia miaka 10 kumekuwa na mazungumzo ya mkataba wa EPA, mpaka leo hatujui kama una faida au hauna faida. Nilidhani kwa sasa ilitakiwa tuwe na nafasi ya kusema kuwa mkataba huu au una faida ili usainiwe, au hauna faida, na hivyo tutamke kuwa hatutasaini. Kutokuusaini nako bado inaonekana ni kioja maana mkataba huo haukuletwa bali ulikuwa ukijadiliwa na wawakilishi toka pande zote mbili EU na EAC.

Kama mkataba huo ulikuwa unaandaliwa na pande mbili kwa majadiliano, kama kuna mambo yanayohitaji marekebisho, nina imani kulikuwa na nafasi ya kuyajadili. Kama tunaona ulikuwa hauna maana kwa nini tulipoteza muda huo wote kwa kitu ambacho tunajua hakina faida kwa watu wetu? Kwani tulilazimishwa?
 
Pongezi gani anastahili ? Kama hauna vya kuuza kwenye nchi za watu utauza nini ? Kilimo kimekufa,viwanda vya kuchakata malighafi stadi hauna,una maneno tu vya kuuza hauna!
Nani katufikisha hapa!
 
Mpaka sasa tunazaidi ya 50yrs Tangu tupate UHURU bado tunasema hatuwezi kushindana hebu niambie unadhani kama Taifa ..tupate muda gani ndio tuweze
 
Asante sana Mama Anna Mghwira,
  • Je ni faida zipi wao wameainisha kuwa tutapata kama Taifa, na kama Kanda ya EA
  • Je, kwakitendo cha mataifa mawili kusaini na mengine kukata kunatuweka katika nafasi gani kama nchi kwa upande mmoja na kama Jumuiya kwa upande mwingine
  • Ni mambo gani kama taifa tungependekeza yawepo kwenye mkataba ili kuridhia kuusaini
 
Haya ni baadhi ya mambo ya kuainisha, kufafanuliwa na wataalam wa uchumi na wa biashara z kimataifa. Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…