THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Mikataba mibovu kama ule wa RICHMOND ilikuwa kipindi cha JK kwa sababu alizungukwa na wapiga dili.Yaani nchi zingine ziifuate Tanzania wakati Tanzania inaongoza kwa kuingia mikataba mibovu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mikataba mibovu kama ule wa RICHMOND ilikuwa kipindi cha JK kwa sababu alizungukwa na wapiga dili.Yaani nchi zingine ziifuate Tanzania wakati Tanzania inaongoza kwa kuingia mikataba mibovu?
Anna Mghwira,
Ni kweli kwa hili namuunga mkono Magufuli japo sikubaliani na mambo yake mengi. Sasa kwenye hili inabidi atumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha anapitia mikataba mingine nchi iliyoingia huko nyuma ili kuona kama ina faida kwa nchi au ilisainiwa na 10%.
Kwa mara ya kwanza nimeona nchi yetu ikisimama kidete dhidi ya mikataba inayotengenezwa ulaya huku ikivalishwa vazi la nia njema.
Sasa tuhakikishe tunapinga mikataba hii lakini tuhakikishe tunajitahidi kujikwamua na hali hii ya kutegemea bidhaa toka nje kwani ninavyojua kuna uwezekano wa nchi hizi za Ulaya kuanza kutupa wakati mgumu.
Maana yangu ni kwamba Tanzania tupo vizuri kwenye mambo ya mikataba kuliko nchi zingine za Afrika Mashariki hadi tuwe viongozi wa kuongoza mkataba huo? Maana kuwa kiongozi unajua/unaweza kuliko wenzako.EPA ni Mkataba mmoja. Mibovu mingine nayo iekwe. Hata hivyo EPA mkataba ndio ulikuwa unakwenda kuwekwa sahihi, haujakamilika bado. Naona tunachanganya mada. Huu mkataba ndio ungesainiwa kwa mara ya kwanza.
Wapiga dili akina Lowasa toka waondoke serikalini mikataba mibovu imepungua sana...Lowasa alitutia hasara sana kwenye mkataba wa RICHMOND.maana yangu ni kwamba Tanzania tupo vizuri kwenye mambo ya mikataba kuliko nchi zingine za Afrika Mashariki hadi tuwe viongozi wa kuongoza mkataba huo? Maana kuwa kiongozi unajua/unaweza kuliko wenzako.
Wachache sana watakuelewa mkuu, hii nchi tumechagua ujinga kuwa sehemu ya maisha yetu. No wonder tuliowatuma hawakufanya hata huu utafiti kidogo. Sisi tunatakiwa kujijenga na kufanya vizuri sana kwenye potential zetu hasa kilimo, madini na rasilimali za asili kama gesi na mafuta yakija. Kamwe hatutakuja kushindana na Ulaya kutengeneza magari sana sana walete matawi ya viwanda vyao. Wasomi wetu hawajui hata vitu vidogo kabisaMwaka 2014 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisaini makubaliano na European Union, wataalamu wa uchumi wa nchi hii hawakutoka na kueleza nini faida au hata kama kuna hasara katika makubaliano hayo.
Hapa ndipo elimu zetu na vyeti vinapopoteza maana, maana anavyoongea mtaalam wa uchumi na biashara na anavyoongea mtu asiye na weredi kwenye maeno haya ni kama sawa tu, wote wanabuni?
Niliwahi kumuuliza afisa mmoja wa serikali anaelewa nini kuhusu EPA? Hakuwa na majibu zaidi ya kutoa hisia zake na mambo aliyoyasikia kwenye magazeti.
Sasa kama maafisa kama hawa ndio wanamshauri rais katika mambo ya kiuchumi bado tuna safari ndefu.
Nisiingie kwenye maamuzi yaliyofanyika hivi karibuni lakini embu tujiulize maswali machache
1. Unaweza kuepuka kufanya biashara na European Union?
2. Wangapi wetu tumesoma makubaliano ya awali kati EAC na EU yaliyofanyika miaka miwili iliyopita? soma hapa http://trade.ec.europa.eu/doclib/docs/2015/october/tradoc_153845.compressed.pdf
3. Bidhaa/ biashara kutoka East African Community kwenda nchi za Umoja wa Ulaya ni kahawa, maua, chai, kahawa, samaki na mbogamboga - Hii ni exports, je nchi yetu ni shindani katika kuzalisha mazao hayo ukilinganisha na nchi nyingine za Africa Mashariki?
4. Bidhaa kutoka EU kuja EAC ni mashine na mitambo, vifaa vya viwandani na ujenzi, magari na vifaa vya tiba na madawa - Je kwenye njozi yetu ya kuwa na uchumi wa viwanda hatuhitaji EPA? Au tutatumia zana za mawe?
Note: Kilimo kinachangia asilimia 24.5 ya GDP
Viwanda na ujenzi asilimia 22.2
Haya ni maeneo ambayo wataalamu wa uchumi wa serikali hii wangeweka focus yao hapo, na kupima kama EPA itakuwa na faida kwa upande wetu.
Nimetimiza wajibu wangu wa kuchangia kwa mustakabali mwema kwa taifa letu.
Wachache sana watakuelewa mkuu, hii nchi tumechagua ujinga kuwa sehemu ya maisha yetu. No wonder tuliowatuma hawakufanya hata huu utafiti kidogo. Sisi tunatakiwa kujijenga na kufanya vizuri sana kwenye potential zetu hasa kilimo, madini na rasilimali za asili kama gesi na mafuta yakija. Kamwe hatutakuja kushindana na Ulaya kutengeneza magari sana sana walete matawi ya viwanda vyao. Wasomi wetu hawajui hata vitu vidogo kabisa
hapo sawa. Sikuji update.Wapiga dili akina Lowasa toka waondoke serikalini mikataba mibovu imepungua sana...Lowasa alitutia hasara sana kwenye mkataba wa RICHMOND.
Anna Mghwira,
..mkataba wa EPA umekuwa negotiated kwa miaka zaidi ya 10.
..mkataba huo ulishakuwa tayari toka mwaka 2014 na EAC ikapewa muda mpaka mwaka huu kusaini mkataba huo.
..sasa wewe ulikuwa MGOMBEA URAISI kwa hiyo suala hili lazima ulipaswa kulifahamu. Kama unafuatilia kampeni za Uraisi za Marekani wagombea wote wanajadili na wana uelewa wa masuala ya trade agreements.
..vilevile wewe ni MWENYEKITI WA CHAMA na chama chenu kina sera zinazohusiana na masuala kama haya.
..sasa naomba kujua msimamo wako, na wa chama chako kuhusu suala hili.
..JE UNGECHAGULIWA KUWA RAISI WETU UNGESAINI MKATABA HUU? AU UNGEUKATAA?
Eric Cartman , chige, @Nguruvi3,MsemajiUkweli ,Geza Ulole
Jokakuu: hata sisi kupewa fursa kujua ni sehemu ya kutatua tatizo. Kwa vyovyote ikiwa majadiliano yalikamilika tangu 2014 hakukuwa na sababu ya kuanza kupima tena. Lakini kama wengine hawakujua na sasa wanataka kujua, pengine hii ni nusu shari, na ni bora kuchukua maamuzi baada ya kujua kuliko bila uhakika. Hii ni changamoto kwa uendeshaji nchi kwa usiri.Ni vema kufanya hivyo lakini ifike mahala tubadilishe sheria zetu zinazo ongoza michakato ya mikataba yetu ili mikataba hiyo inakuwa wazi na Wananchi wanapewa furusa ya kuijadili ili waweze kunufaika nayo.
swali la kampeni. Mambo ya ingekuwa mimi ilikuwa mwaka jana. Sasa yupo mtu tunapima kulingana na maelekezo yake. Tunaweza kukataa ama kuridhia bila kuingiza kampeni...Anna Mghwira,
..mkataba wa EPA umekuwa negotiated kwa miaka zaidi ya 10.
..mkataba huo ulishakuwa tayari toka mwaka 2014 na EAC ikapewa muda mpaka mwaka huu kusaini mkataba huo.
..sasa wewe ulikuwa MGOMBEA URAISI kwa hiyo suala hili lazima ulipaswa kulifahamu. Kama unafuatilia kampeni za Uraisi za Marekani wagombea wote wanajadili na wana uelewa wa masuala ya trade agreements.
..vilevile wewe ni MWENYEKITI WA CHAMA na chama chenu kina sera zinazohusiana na masuala kama haya.
..sasa naomba kujua msimamo wako, na wa chama chako kuhusu suala hili.
..JE UNGECHAGULIWA KUWA RAISI WETU UNGESAINI MKATABA HUU? AU UNGEUKATAA?
Eric Cartman , chige, @Nguruvi3,MsemajiUkweli ,Geza Ulole
Kibiashara inaweza kuonekana tunachelewa, lakini pengine bora kuchelewa kiusahihi kuliko kubahatishaMkuu you nailed it...hata huko EU ni mbali kwa vigin land tulionayo inatosha Kabisa kututajirisha kwa kulisha majirani Zetu tu...tatizo hapa ni kutawaliwa na watawala wale wale wenye mawazo na akili zile zile kwa miaka hamsini..
Wananchi wa Kenya nao wanalalamika kuwa watakachouza EU sana sana ni maua na maua yenyewe wanaolima 85% ni kampuni za kigeni..
Lakini serikali haijakataa kusaini nadhani imesitisha kusaini kwa sasa...mpaka baaada ya miezi 3. Kuna mambo mengi ya kuangalia na kupima nadhani...ni jambo jema kukaa na kuutafakari huu mkataba kwanza@Anna
Wewe Joka unauliza
swali la kampeni. Mambo ya ingekuwa mimi ilikuwa mwaka jana. Sasa yupo mtu tunapima kulingana na maelekezo yake. Tunaweza kukataa ama kuridhia bila kuingiza kampeni...
Zungu Pule: Somavizuri post yangu utajua sikusema nimehudhuria mkutano wa wakuu wa nchi..wanachama...hilo ukijibiwa hutahitaji kuuliza mengine
Nani katufikisha hapa!Pongezi gani anastahili ? Kama hauna vya kuuza kwenye nchi za watu utauza nini ? Kilimo kimekufa,viwanda vya kuchakata malighafi stadi hauna,una maneno tu vya kuuza hauna!
Mpaka sasa tunazaidi ya 50yrs Tangu tupate UHURU bado tunasema hatuwezi kushindana hebu niambie unadhani kama Taifa ..tupate muda gani ndio tuwezeNakubaliana nawe hili suala la viwanda sio la kukamilika overnight lakini huu mkataba naona utakuza tu viwanda vya huko ulaya kwa kuwawezesha kuleta bidhaa zao huku with tax exemption, sisi hatuwezi kushindana nao kamwe, tutaishia lada kuuza raw materials halafu wataziprocess kwao na ikiwezekana kuzirejesha huku kama finished products kwa faida maradufu.
Kwa hali hiyo hamna kiwanda hapa nchini kitakachoweza kufunguliwa na kuzalisha bidhaa itakayoshindana na hizo zinazotoka Ulaya tutaishia kuwa dependent on importing goods kutoka nje wakati Rais kwa maono yake anataka sisi tuweze kujihudumia kwa bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe mpaka kufikia hatua ya ku-export kwa wengine.
Hayo ni mawazo yangu japo mimi sija-specialize kwenye maswala ya uchumi wenye ujuzi zaidi wanaweza kunirekebisha au kukubaliana nami.
Asante sana Mama Anna Mghwira,
- Je ni faida zipi wao wameainisha kuwa tutapata kama Taifa, na kama Kanda ya EA
- Je, kwakitendo cha mataifa mawili kusaini na mengine kukata kunatuweka katika nafasi gani kama nchi kwa upande mmoja na kama Jumuiya kwa upande mwingine
- Ni mambo gani kama taifa tungependekeza yawepo kwenye mkataba ili kuridhia kuusaini
Haya ni baadhi ya mambo ya kuainisha, kufafanuliwa na wataalam wa uchumi na wa biashara z kimataifa. Asante.Asante sana Mama Anna Mghwira,
- Je ni faida zipi wao wameainisha kuwa tutapata kama Taifa, na kama Kanda ya EA
- Je, kwakitendo cha mataifa mawili kusaini na mengine kukata kunatuweka katika nafasi gani kama nchi kwa upande mmoja na kama Jumuiya kwa upande mwingine
- Ni mambo gani kama taifa tungependekeza yawepo kwenye mkataba ili kuridhia kuusaini