Nimeibiwa milioni 5 Stendi ya Mabasi ya Magufuli

Omopa

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2022
Posts
335
Reaction score
1,466
Sijui ni karma au ni nini mpaka sasa wala sijui nifanyeje daaah nashindwa sijui nifanyeje wakuu na hapa ninapoandika navuja machozi nipo kwenye gari langu nimepaki nalia mwenyewe wakuu.

Nilifika na gari langu dogo aina ya Toyota crown athelete(namba za usajili kapuni) nilikuwa namsindikiza wife alikuwa anaelekea kondoa huko kwao kusalimia na pesa niliziweka kwenye briefcase yangu sasa nikashuka na wife kwenda kumsindikiza kwenye gari ABM coach la Dodoma nikasahau kufunga mlango wa gari aisee lahaula kurudi nikakuta mlango upo wazi briefcase yangu haipo na kila kila kitu hakipo na halafu ukizingatia hizo pesa ni za mapato ofisini nilikuwa napeleka ofisi za halmashauri x😩😩😩😩😩

Wakuu naombeni kama kuna mtu ataiona please mnicheki Pm tafadhali wakuu.

Nafwa nitafungwa mie😫😫😫
 
Hufungwi.

Hivi Stand kubwa kama Magufuli haina cameras?

Bila shaka wanayo. Nenda wakuangalizie. Pengine wanaweza wasitambulike ila ikakuhakikishia usalama wako.

Ila ulichokifanya ni uzembe wa hali ya juu.

Uza crown lipa pesa za ofisi.
 
Una laki tano tukamroge huyo mwivi?
 
Yaani hata ungefunga mlango jamaa wangevunja iwapo wangejua zipo huko ndani ya gari sembuse wewe hata mlango hukufunga? Mambo mengine mnatakaga kuwalaumu wezi bure tu.

Kwanini hukushuka na hilo brifkesi lako mkuu, kwani lina kilo ngapi hilo?

Wala usilie kwa kuibiwa hela, lia kwa wewe kuzaliwa mbwiga na fala
 
Kumbe nyie ndiyo mnafuga wezi.
 
Hufungwi.

Hivi Stand kubwa kama Magufuli haina cameras?

Bila shaka wanayo. Nenda wakuangalizie. Pengine wanaweza wasitambulike ila ikakuhakikishia usalama wako.

Ila ulichokifanya ni uzembe wa hali ya juu.

Uza crown lipa pesa za ofisi.
M 7 ipo kwenye mfuko wa shati hapa aje fasta na mimi nitembelee matako 4
 
Pole ndugu. Ni mistake tu kupitiwa kupo auna aja ya kulia ndugu pambana ulipe tu mana Hilo lishakua deni ndugu sawa yake ni kulipa na sio kulia
 
Pole Sana, Mungu akupe nguvu utapata zingine

 


huyuu anavituko sanaa.
 
Pole mkuu mradi wamekuachia simu rizki ya mtu ipo kwa mtu!
 

Pole sana sheikh
 
Lengo ni kututangazia kwamba umenunua gari na kwamba ulikuwa na 5m.

Unasahauje kufunga mlango wa gari likiwa na hela ndani.

Hata hivyo hongera kwa kununua gari.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…