Nimeibiwa simu na mwizi ametoa pesa tiGO Pesa!

Nimeibiwa simu na mwizi ametoa pesa tiGO Pesa!

Yes unakuta aliweka namba au kupiga picha kitambulisho cha NIDA akaweka kwenye simu. Mwizi akipata taarifa zako ni rahisi akiingia kwenye MENU ya Tigo pesa kule kwenye kubadili password watamuuliza aweke namba ya NIDA akiweka hiyo wanaifyatua.

Nb; alipoibiwa pale pale angetafuta mtu baki mwenye tigo wapige simu huduma kwa wateja Waifunge laini.
Niligundua sina simu baada ya muda kama saa moja
 
Kuna baadhi ya nchi ni Kosa kisheria kutokuweka Number za siri kwenye simu yako na Simcard..kabla ya kulaumu tigo,why laini yako haina PIN??usalama unaanza na wewe...tofauti na kuibiwa ipo siku laini yako itatumika vibaya.
Kuna wabongo wanakwambia mimi ni mwaminifu siwezi kuweka ma PIN na password kila mahali.Yaan akili zao zinawaza hapa karibu tu hawajui kua simu yako inaweza kutumika vibaya ikiangukia kwa muhalifu.Kuna shemej yangu alikwapuliwa simu,simu ilikua nyeupe haina kipengele chochote cha usalama.lijamaa lilifanya kama yake lilikua linajibu hadi meseji za watu.linaingia kwenye magroup ya whatsap linachat ujinga na matusi alafu linaleft.lilifanya ujinga alafu likapotea jumla.sasa lingefanya uhalifu mkubwa ingekua kimbembe.
 
Amerenew line yako akaeka namba za siri upya mana mawakala wa mtaani wana process ya ukimtajia namba anakupatia nida yako
 
Amerenew line yako akaeka namba za siri upya mana mawakala wa mtaani wana process ya ukimtajia namba anakupatia nida yako
Sasa tigo watawajibika. Pesa nimeweka kwao sasa zimeibiwa wananiambia niende kuripoti polisi. Usalama wa pesa zangu ulikuwa mikononi mwa nani?? Huko polisi nilishapeleka loss report tatu hakuna hata moja ilipatikana!!
Swali kwako unarenew vipi laini bila dole gumba
 
Watanzania Wana tabia ya kuweka simple password
Anaweka mwaka wa kuzaliwa au anaweka no rahisi mf 1000 au 2000
Mwizi hapati shida
 
Amerenew line yako akaeka namba za siri upya mana mawakala wa mtaani wana process ya ukimtajia namba anakupatia nida yako
Wakala Hana access ya kurudisha line Bila dole gumba
Huyu aliweka password ya tigopesa rahisi mwizi akajaribu mara mbili tu akaipatia akatoa mzigo
 
Nimeibiwa simu yenye line ya Tigo na nilipoenda kuchukua line mpya naangia salio la pesa nakuta hakuna kitu! Kwenye statement inaonekana mwizi ametoa pesa mara tatu. Hii inawezekana vipi mtu hajui password yangu atoe pesa??
Pole sana
 
Pole sana
Nimewapigia Tigo makao makuu nimewaambia pesa nimeweka kwao. Usalama wa pesa zangu uko mikononi mwao. Ninachotaka ni pesa zangu zirudi siyo kuniambia nikaripoti polisi. Mimi sikuweka pesa polisi. Wao kama banker wawajibike
 
Back
Top Bottom