Nimeibiwa takribani laki 5 na Binti wa duka langu jipya ndani ya miezi miwili. Nichukue uamuzi gani?

sasa muambie mtoa mada ajitambue analeta mahaba kweny biashara
Mimi kipindi naanza kuweka vijana wauze nilipata hasara nilikuwa naona aibu hata kuwauliza mbona kuna hasara ila kuna ndugu yangu akanambia ukiwa na huruma na utu utafunga biashara yako sasa hivi ni mwendo wa roho ngumu zaidi ya jiwe
 
Umemtengeneza huyo dada kuwa mwizi, biashara hazifanywi hivyo, kwa biashara ya duka kila siku hesabu lazima ifungwe na hela ziondoke.

huyo hana biashara anatuhadaa tu. yani mtu anafanya biashara anaweka hela humohumo
 
Mkuu shemeji kwani yuko bize kiasi gani asiweze kudhibiti mauzo?

Kama umeingiwa na moyo wa huruma kwa huyo kibaka, basi wife amzungukie kila muda kumkagua na kuhamisha cash na kumbakizia kidogo tu za chenji.

Ila uelewe kuwa huyo anavoendelea kukaa hapo ndivyo anavyoweza kupanga mbinu chafu na za kukuumiza wewe zaidi.

Siku moja waweza kukuta kahamisha duka zima na yeye kapotea, hivyo hafai kuendelea kuhudumia huo mradi maana hana woga na hana malengo ya maisha, ni mharibifu na mwizi.

Wapo watu wema na waadilifu kuweza kumuweka hapo na akaendesha vizuri.

Wakati unatafuta mtu sahihi, afanye kazi chini ya uangalizi usioisha na ukijaaliwa kupata mhudumu mwingine mapema, mhamishie nyumbani kufanya kazi za house girl kumalizia deni hilo la loss, kisha mtimue.
 
kuna msemo unasema bora shetani unaemjua kuliko malaika usiemfahamuu...!! Nakwambi huyu binti ni bora kuliko huyo mpya atakaekuja.
Unataka mwenzio afilisike mkuu tatizo ya Hawa wafanyakazi ukisha mgundua kama ni mwizi hapo kamwe hatakuwa mzuri tena kwanza anajua mda wowote anatolewa kwa hiyo ama akupige tena pakubwa zaidi ya mara ya kwanza ili atakapo ondoka awe na pesa .
 
Kula jicho Kisha fukuza, vinginevyo itaendelea kula hasara
 
Post za watakatifu wa jf
 
Asante kwa kuniunga mkono.
Amkate mshahara kidogo kidogo na amfundishe kuwa makini...atakuwa bora sana
Hakuna mfanyakazi wa hivyo mkuu yaani huyo anaenda kubuni mbinu ya kupiga asigundulike tena.
 
Na anaweza akaleta stock yake akawa anauza kimyakimya bila kukuibia huku biashara yako ikizidi kudorora
Kwa point yako hiyo tu, wewe ni mjuzi na mtaalamu wa uendeshaji wa biashara za maduka.
 
Hakuna mfanyakazi wa hivyo mkuu yaani huyo anaenda kubuni mbinu ya kupiga asigundulike tena.
Nuzu
Wewe ni binti makini lkn hapa sikuungi mkono.

Watu wengi wanatia hasara sio kwa kuiba bali kukosa uzoefu na umakini.
Kuingiza hasara dukani ni sekunde tu.

Huenda hajaiba isipokuwa kukosa umakini, apewe nafasi na asimamiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…