Nimeibiwa takribani laki 5 na Binti wa duka langu jipya ndani ya miezi miwili. Nichukue uamuzi gani?

sasa muambie mtoa mada ajitambue analeta mahaba kweny biashara
Mimi kipindi naanza kuweka vijana wauze nilipata hasara nilikuwa naona aibu hata kuwauliza mbona kuna hasara ila kuna ndugu yangu akanambia ukiwa na huruma na utu utafunga biashara yako sasa hivi ni mwendo wa roho ngumu zaidi ya jiwe
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, kwangu nimeona ni uduanzi tu, nataka nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Nimepata wazo kwamba afanye kazi miezi minne hapa kila siku awe anachukua elf 2 tu hakuna mshahara.

Mnaweza kunipa mawazo mbadala ama ya ziada wakuu niweze kudeal nae vizuri.
Mkuu shemeji kwani yuko bize kiasi gani asiweze kudhibiti mauzo?

Kama umeingiwa na moyo wa huruma kwa huyo kibaka, basi wife amzungukie kila muda kumkagua na kuhamisha cash na kumbakizia kidogo tu za chenji.

Ila uelewe kuwa huyo anavoendelea kukaa hapo ndivyo anavyoweza kupanga mbinu chafu na za kukuumiza wewe zaidi.

Siku moja waweza kukuta kahamisha duka zima na yeye kapotea, hivyo hafai kuendelea kuhudumia huo mradi maana hana woga na hana malengo ya maisha, ni mharibifu na mwizi.

Wapo watu wema na waadilifu kuweza kumuweka hapo na akaendesha vizuri.

Wakati unatafuta mtu sahihi, afanye kazi chini ya uangalizi usioisha na ukijaaliwa kupata mhudumu mwingine mapema, mhamishie nyumbani kufanya kazi za house girl kumalizia deni hilo la loss, kisha mtimue.
 
kuna msemo unasema bora shetani unaemjua kuliko malaika usiemfahamuu...!! Nakwambi huyu binti ni bora kuliko huyo mpya atakaekuja.
Unataka mwenzio afilisike mkuu tatizo ya Hawa wafanyakazi ukisha mgundua kama ni mwizi hapo kamwe hatakuwa mzuri tena kwanza anajua mda wowote anatolewa kwa hiyo ama akupige tena pakubwa zaidi ya mara ya kwanza ili atakapo ondoka awe na pesa .
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, kwangu nimeona ni uduanzi tu, nataka nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Nimepata wazo kwamba afanye kazi miezi minne hapa kila siku awe anachukua elf 2 tu hakuna mshahara.

Mnaweza kunipa mawazo mbadala ama ya ziada wakuu niweze kudeal nae vizuri.
Kula jicho Kisha fukuza, vinginevyo itaendelea kula hasara
 
Mkuu shemeji kwani yuko bize kiasi gani asiweze kudhibiti mauzo?

Kama umeingiwa na moyo wa huruma kwa huyo kibaka, basi wife amzungukie kila muda kumkagua na kuhamisha cash na kumbakizia kidogo tu za chenji.

Ila uelewe kuwa huyo anavoendelea kukaa hapo ndivyo anavyoweza kupanga mbinu chafu na za kukuumiza wewe zaidi.

Siku moja waweza kukuta kahamisha duka zima na yeye kapotea, hivyo hafai kuendelea kuhudumia huo mradi maana hana woga na hana malengo ya maisha, ni mharibifu na mwizi.
Wapo watu wema na waadilifu kuweza kumuweka hapo.
Wakati unatafuta mtu sahihi, afanye kazi chini ya uangalizi na ukijaaliwa kupata mhudumu mwingine mapema, mhamishie nyumbani kufanya kazi za house girl kumalizia deni hilo la loss, kisha mtimue.
Post za watakatifu wa jf
 
Asante kwa kuniunga mkono.
Amkate mshahara kidogo kidogo na amfundishe kuwa makini...atakuwa bora sana
Hakuna mfanyakazi wa hivyo mkuu yaani huyo anaenda kubuni mbinu ya kupiga asigundulike tena.
 
Na anaweza akaleta stock yake akawa anauza kimyakimya bila kukuibia huku biashara yako ikizidi kudorora
Kwa point yako hiyo tu, wewe ni mjuzi na mtaalamu wa uendeshaji wa biashara za maduka.
 
Hakuna mfanyakazi wa hivyo mkuu yaani huyo anaenda kubuni mbinu ya kupiga asigundulike tena.
Nuzu
Wewe ni binti makini lkn hapa sikuungi mkono.

Watu wengi wanatia hasara sio kwa kuiba bali kukosa uzoefu na umakini.
Kuingiza hasara dukani ni sekunde tu.

Huenda hajaiba isipokuwa kukosa umakini, apewe nafasi na asimamiwe
 
Back
Top Bottom