Nimeibiwa takribani laki 5 na Binti wa duka langu jipya ndani ya miezi miwili. Nichukue uamuzi gani?

Kama yuko tayari, usimwambie Mama yake kama alivyoomba, aendelee kufanya kazi kwa ufuatiliaji wa karibu, mlipe nusu mshahara mpaka deni lilipwe.
Aambiwe aliyemtafuta ili alipe
 
mzee hivi unafanya biashara au umeajiriwa? na kama una biashara nahisi ni ndogo tu, ww uinvest zaidi ya 20 million ya kusotea na mkopo mtu anakuiibia almost half a million unasema umoe second chance????

Tabia haichi Asili.

Mtu akiiba hapaswi kupewa nafasi nyingine,

Huwa tunaweka mpya anakaa miezi 6 anakuja mwingine,kabla hajazoea mazingira anaondolewa.

Huo ushauri wako ni batili.Na usithubutu kuufata siku ukifungua biashara ya mamillioni
rikiboy an pointi nzito, ukimfukuza ni sawa na kumsamehe, pesa inakuwa imeenda hio.

Nimeona point yake ina make sense maana kwa sasa nishamjua hivyo atatumia nguvu kubwa sana kurudisha imani yake ya kuwa mwaminifu.

Ntachofanya ntabadili utaratibu kidogo, ntakuwa namkata elf 50 kila mwezi, mshahara utakuwa elf 50 na allowance kama kawaida.
 
Endelea hvyohvyo sawa?
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, kwangu nimeona ni uduanzi tu, nataka nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Nimepata wazo kwamba afanye kazi miezi minne hapa kila siku awe anachukua elf 2 tu hakuna mshahara.

Mnaweza kunipa mawazo mbadala ama ya ziada wakuu niweze kudeal nae vizuri.
Pole sana mkuu duka mpe mkeo
 
mzee hivi unafanya biashara au umeajiriwa? na kama una biashara nahisi ni ndogo tu, ww uinvest zaidi ya 20 million ya kusotea na mkopo mtu anakuiibia almost half a million unasema umoe second chance????

Tabia haichi Asili.

Mtu akiiba hapaswi kupewa nafasi nyingine,

Huwa tunaweka mpya anakaa miezi 6 anakuja mwingine,kabla hajazoea mazingira anaondolewa.

Huo ushauri wako ni batili.Na usithubutu kuufata siku ukifungua biashara ya mamillioni
Mimi sasa hivi nimechukua hiyo nikiona Mfanyakazi ana anza mazoea na kuna dalili ya upigaji namuondoa haraka,nikigundua kuna wizi umetokea police inamhusu sicheki na kima.
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, kwangu nimeona ni uduanzi tu, nataka nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Nimepata wazo kwamba afanye kazi miezi minne hapa kila siku awe anachukua elf 2 tu hakuna mshahara.

Mnaweza kunipa mawazo mbadala ama ya ziada wakuu niweze kudeal nae vizuri.

Umemtengeneza huyo dada kuwa mwizi, biashara hazifanywi hivyo, kwa biashara ya duka kila siku hesabu lazima ifungwe na hela ziondoke.
 
Wahindi ukiwaibiaa lazima uwekwe ndani na ndugu zako wachangie ile hela ya loss ndo utoke.

Labda akusamehe.

Hela za haramu hazina uchungu, iwe kaaiiba madili utapeli na kadhalika.

ndo mana anaibiwa laki 5 anachekacheka na kuomba ushauri.

Mimi nimesota sana na maisha afu mtu aniibia kweny biashara aiseee, Aroooo
Sitaki ujinga weka ndani au Fukuza kabisa siku hiyohiyo

HALAFU MTOA MADA NI ZUZU YANI UNAKUTA SHOTI 147,000 ETU ANASUBIRI AIIBIWE MILLION 1 AJE ALALAMIKE

KUNA WATU WA HOVYOOO
Asante sana mkuu..

Kuna Boss mmoja ali ibiwa kidogo kidogo store kuja kupiga hesabu 60m

Alicho SEMA nanukuu,

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
 
Kwa mshahara wa sh 6000 per day ni haki yako kuibiwa...Tanzania tulitakiwa tuwe na mfumo wa kulipana kwa masaa ambayo mtu amefanya kazi...kiwango cha chini kingekuwa sh 2000 kwa saa
 
SASA wewe unafikiri ni adhabu gani nyingine inaweza mfaa zaidi ya hiyo Kwa mfano !?

Kesha kuchapa!....na wewe ni kumchapa nao! Maana uwezo wa kulipa hana! Zaidi ya kukupa hicho cha maungoni!

Kuchapa kuchapana tu.... Ndo kusemaaaa!? tunasema ngoma draw!
Wazo bandia
 
Back
Top Bottom