Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

Thank you mkuu kwa kuja hapa maoni yako ni muhimu sana
 
Lakini hata lile somo lako la Ongeza Thamani nililichukua mkuu
 
Nitajie hata PM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha uliishia kuzivaa mwenyewe,,,,,, me nilifuga kuku ila kwakupenda kula nyama yakuku nilijikuta nimewatafuna wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana Rebecca
 
Kabla ya kusema umeingiza 1,092,600 ni vizuri ukatenga mshahara wako wa miezi mitatu iliokaa dukani. Laki 900,000 kuzalisha 1,092,600 kwa miezi mitatu siyo haba ila hujatuambia hiyo 1,092,600 umepataje?

Maana faida unatakiwa uchukua bidhaa zote zilizopo dukani +cash + madeni unayodai nje - zile unazodaiwa wewe mfano hiyo TZS 800,000
 
Mkuu kwa mtaji wangu bado sijaanza kujilipa SASA SIJUI NAKOSEA AU LAH
 
Maana faida unatakiwa uchukua bidhaa zote zilizopo dukani +cash + madeni unayodai nje - zile unazodaiwa wewe mfano hiyo TZS 800,000
Upande wa Cash huwezi kunikuta Nina cash labda kama nimebahatika kuuza siku husika pesa yote nitakayouza naiagiza mzigo so hata hiyo Faida NAIONA KWENYE DAFTAR LANGU TU
 
Mkuu kwa mtaji wangu bado sijaanza kujilipa SASA SIJUI NAKOSEA AU LAH
Unaishije kama full time uko dukani? Namna pekee ya kuwa na nidhamu kwenye biashara yako ni kujipangia kiwango cha kuchukua kulingana na ukubwa wa biashara yako.

Mwaka 2005 niliacha kazi ya mshahara wa TZS 1,500,000 nikafungua biashara yangu; nilianza kujilipa TZS 150,000 kwa mwezi; ikaja laki 300,000 baadaye 1,000,000 na sasa nina mshahara wa kunitosha kusomesha vijana wangu shule zenye majina
 
Upande wa Cash huwezi kunikuta Nina cash labda kama nimebahatika kuuza siku husika pesa yote nitakayouza naiagiza mzigo so hata hiyo Faida NAIONA KWENYE DAFTAR LANGU TU
Fanya stock ujui bidhaa zilizopo dukani kwa bei ya kununulia zina thamani gani. Hiyo ya kwenye daftari ni "CASH PROFIT"
 
Biashsra gani unafanya
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…