Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

Keep up the good work kuna mtaalamu kakushauri vizuri kucompliment biashara yako na izo females utensils kama vikuku,hereni n.k fanya ivo mkuu utafika mbali uje ufungue duka la urembo kabisa
 
Keep up the good work kuna mtaalamu kakushauri vizuri kucompliment biashara yako na izo females utensils kama vikuku,hereni n.k fanya ivo mkuu utafika mbali uje ufungue duka la urembo kabisa
Asante mkuu
 
Mkuu kwa biashara uliyoifanya kwa siku 90 tu imekupa return hio? Usiiache,kwani kawaida biashara ambayo haikupi hasara ni biashara nzuri sana. Uwekezaji wako na return unayoipata ni sawasawa. Unaendelea vizuri.
 
Ku-net positive ni kitu kizuri, ila still faida hiyo ni ndogo, 333K kwa mwezi haitoshi kuishi popote pale.
Ila kabla ya yote hayo jiulize maswali haya kwanza

1. Je biashara inapanda au inashuka? yaani mwezi wa kwanza hadi sasa mauzo kila mwezi yanaongezeka au yanashuka? kama yako palepale au yanashuka then biashara hiyo ni mbaya, meaning ulikua na traction mwanzoni tu imekata mapema, yaweza kua sababu ya covid pia ila inabidi kua makini, kama inapanda basi angalia utafanyeje kuaccelerate hiyo faida, unachotengeneza kwa miezi mitatu ukitengeneze kwa mwezi moja, then igeuke kua in two weeks, then one, ikiwezekana igeuke kua in a day. Sijui biashara yako ni ipi ila liangalie hili

2. Hiyo 333k kwa mwezi, is it worth your time? au ungeweza fanya kitu kingine ukaingiza hela zaidi ya hiyo? Ni muhimu sana kuvalue muda wako, muda ni kitu ambacho kikiondoka hakirudi tena, so inabidi utumie effectively.

All the best, entrepreneurship inaanzia hukohuko then mtu anazidi kukua, inafika muda hiyo 1m haikupi hata mawazo, zipo nyingi tu kwenye account zimejaa wakati wote.
 
sasa kama una wivu hivyo mkeo akiwa mjamzito akapelekwa hospital si utazimia kabisa kue wanaingizwa mikono mzee wanachunguliwa nyuchi bila huruma,na bahat mbaya kila wodi ya wazazi madaktar wanaume wamejaa kibao.
 
Kaza mwendo kamanda,ujasiriamali hua ni lonely journey, usitafute mtu wa kukutia moyo wala nini.Wewe endelea na mapambano.

Uko kwenye right track.
INANIPAGA NGUVU YA KUSONGA MBELE
 
Mkuu si vibaya ukatuwekea picha ya dula lako tuone lilivyosheheni huenda likatupa motisha wengine wengi tunaofikiri labda mpaka tuwe na mamilion
 
Kwahiyo kipindi unapiga haya mahesabu, mzigo ulio nao ulikua una thamani gani?
 
Unakwenda vizuri sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nimebobea pia kwenye biashara/ ujasiriamali. Pia na MBA (Master of Business Administration).Ili nikupe ushauri, naomba screenshot ya income statement yako.
 
UPDATE

From JANUARY TO MARCH

Hiki ndicho nilichokivuna 747,050/=

Habarini wana jamvi wengi walitamani kusikia mambo yapoje baada ya miezi mitatu mingine. Kiukweli biashara ni ngumu lakini Mungu ni mwema hicho ndicho nilichovuna
Najua wapo watakao beza Karibuni

Picha naleta soon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…