UPO
Huo ndio mtihani mweyezi mungu kakupatia,
Nimeishi miaka 8 bila mtoto ndani ya ndoa,mke wangu akaniambia yeye Hana historia ya kupata mimba tangu ubinti wake hivyo hivyo nitafute mwanamke mmoja anizalie watoto wa kurithi jina langu Kwa sharti watoto wakiwa na umri wa miaka 2 anawachukua na kuwalea yeye kwa kua jambo lilikua na baraka za mke wangu kipenzi sikuchelewa kupata mwanamke,saivi Nina watoto 4 na mke wangu anawalea na kuwasomesha Kwa kuwa ana kipato.
Jambo hili usilifanye bila kuongea na mkeo Kama unahitaji kupata watoto nje
Miaka 8 bila mtoto ndani ya ndoa yangu lakini mapenzi hayakupungua Kwa mke wangu nikampenda zaidi asiwe mnyonge siku Moja tukiwa katika stori akasema unaonaje utafute Binti umuoe azae watoto wataorithi jina lako nikamwambia haiwezekani nakupe da sana Lakini moyoni najisemea na iwe kweli akazidi kuniambia Ilo suala mwisho I nikakubali nikatafuta mwanamke nikaoa Kwa sharti watoto wakiwa na umri wa miaka 2 anawachukua na kuwalea yeye kwa kua alikua na kipato kizuri aliwalea na kuwasomesha nilifanikiwa kupata watoto 4, Nina ndoa nzuri na watoto nashukuru kuwa na mke huyu japo hajanipa mtoto lakini ni baraka sana kwangu
SawaAchana na specialist,huyo si zaidi ya uhalisia,
Basi kama.huamini acha baki hivyo tu,siku ukiacha nae atazaa kwa mwingine na utafedheheka
Story nzuri Sana mkuuPO
Huo ndio mtihani mweyezi mungu kakupatia,
Nimeishi miaka 8 bila mtoto ndani ya ndoa,mke wangu akaniambia yeye Hana historia ya kupata mimba tangu ubinti wake hivyo hivyo nitafute mwanamke mmoja anizalie watoto wa kurithi jina langu Kwa sharti watoto wakiwa na umri wa miaka 2 anawachukua na kuwalea yeye kwa kua jambo lilikua na baraka za mke wangu kipenzi sikuchelewa kupata mwanamke,saivi Nina watoto 4 na mke wangu anawalea na kuwasomesha Kwa kuwa ana kipato.
Jambo hili usilifanye bila kuoN
Miaka 8 bila mtoto ndani ya ndoa yangu lakini mapenzi hayakupungua Kwa mke wangu nikampenda zaidi asiwe mnyonge siku Moja tukiwa katika stori akasema unaonaje utafute Binti umuoe azae watoto wataorithi jina lako nikamwambia haiwezekani nakupe da sana Lakini moyoni najisemea na iwe kweli akazidi kuniambia Ilo suala mwisho I nikakubali nikatafuta mwanamke nikaoa Kwa sharti watoto wakiwa na umri wa miaka 2 anawachukua na kuwalea yeye kwa kua alikua na kipato kizuri aliwalea na kuwasomesha nilifanikiwa kupata watoto 4, Nina ndoa nzuri na watoto nashukuru kuwa na mke huyu japo hajanipa mtoto lakini ni baraka sana kwangu
Sawa mkuuHakuna uchawi, ni akili yako tu imekosa majibu kwa matatizo yanayokusibu kwa hiyo inahangaika kujaza majawabu yoyote.
Kwa kifupi sana sijasoma maelezo yotee nimesoma heading TU.Nimekuja hapa JamiiForums kuomba ushauri na msaada Kwa namna moja au nyingine, hapa nimekuwa nikisoma tu nyuzi za watu nilikuwa sina account na mimi nimeona nijiunge nitoe yanayonisibu labda nitapata msaada, hapa naamini ni sehemu sahihi japo kuna ambao sometimes wanaleta masikhara.
Ishu inayonisumbua ni kwamba nimekaa na mwanamke kwasasa takriban Miaka mi3 hatujafanikiwa kupata mtoto.
Tulishakwenda hospitali kupima wote tukaonekana tupo sawa hatuna shida (hospitali special za uzazi) pia mimi kwenye pita pita zangu maisha ya nyuma huko nishawahi kutia sana wanawake mimba.
Harakati zetu za kutafuta mtoto zilianza baada ya kukaa Kwa mwaka mzima bila mwanamke kupata ujauzito, ndio akaanza na dawa za kupevusha mayai na za hormone imbalance (hii ni baada ya kupima hospitali kuambiwa hatuna shida akashauriwa atumie hizo), baada ya kuona mwaka wa pili unaingia bilabila ikabidi tuhamie kwenye dawa za kienyeji za chango, kanywa Sana Lakini hatukupata matokeo.
Tukahamia Kwenye kuombewa, manabii, wachungaji wa madhehebu karibia YOTE ya kikristo ashaombewa, ilifika kipindi maji ya kunywa na mafuta ya kupikia tulikua tunachukulia Kwa mwamposa.
ikabidi sasa nitafute mtaalamu japokuwa hayo sio mambo yangu, nijaribu kuchekiwa(ramli) ili nijue Kwa upande wa pili kama kuna shida yoyote.
Hapa sasa ndio nikaja kuamini kuwa uchawi upo, niliwasiliana na mtaalamu wa kwanza (namba zake nilipewa na mshkaji wangu), nikamtumia majina yetu wote watatu ili aangalie nani ana shida, nilipomtumia baada ya nusu saa akanipigia akaniambia kaangalia kwa upande wangu hakuna shida ila tatizo lipo Kwa mwanamke amefungwa, akanielezea kama kuna ndoto anaota usiku nikamwambia ndio, akaniambia ana kitu cha kichawi kimefunga uzazi.
Kwakweli sikuamini, nikahisi labda huyo Mtu ananichezea akili, huyo anakaa mikoa ya kaskazini ikabidi nitafute mwingine wa mkoa tofauti kabisa (Mimi nakaa Dar).
Nilipotafuta mwingine wa mkoa tofauti, maajabu ni kwamba ALINIAMBIA KITU KILEKILE KAMA HUYO WA KWANZA😳, nilishangaa Sana nikahisi hawa watu wanajuana wanaambiana au?! Lakini mbona ni watu hawajuani kabisa??! Na wanakaa mikoa ya tofauti kabisa??
Sikuridhika na majibu ya hao wawili japo yanafanana, NIKATAFUTA MWINGINE WA TATU kutoka mkoa mwingine (wote hawa ni wale wanatibu kiarabu, masheikh)
Huyu wa tatu nae alinipa majibu yaleyale kama ya wale wawili wa mwanzo, hapo ndio nikaamini, nikachukue hatua ya kwenda kwa yule wa kwanza ili huyu mwanamke atibiwe.
Kufupisha story, baada ya kwenda kutibiwa Kwa huyo wa kwanza, akapata nafuu Kwa kutokuota ndoto mbaya Kwa miezi mitatu tuu lakini mimba haikushika, baada ya miezi mitatu ndio ikawa kama tumechokoza kwani alikuwa akiota ndoto za kutisha mara nyingine anaota anaingiliwa.
Nilienda Kwa wote hao lakini HATUKUFANIKIWA, na pia nilienda Kwa wataalamu wengine nao wakaniambia amefungwa, tukajaribu na huko lakini hatujafanikiwa mpaka sasa.
Nikiwaza nimuache roho inakua nzito kwani ni Mwanamke alietulia Hana mambo mengi ya kimjinimjini (nilitoka nae mkoani), nawaza kurudi tena kutafuta alietulia kama huyu inaweza kuwa kazi ngumu sana kwa maisha ya sasa hivi.
Naombeni msaada wenu, najua hii kitu wapo waliopitia ambao wapo hapa JF, kwa ambao mlishawahi kupitia hili mkatoboa nakaribisha ushauri.
Tokea nimeanza kuhangaikia hii ishu nimecalculate nimetumia zaidi ya millioni 5 Kwa nauli za kwenda mikoani na kulipa wataalamu.
Kwa upande wa Imani Sisi ni wakristo na yeye anazingatia maombi hata Mimi kumpeleka Kwa wataalamu ilikuwa mbinde kwani alikua haamini hayo mambo, ikumbukwe ashaombewa sana, kwa manabii na wachungaji pia tulishaenda sana tulipooona hamna suluhisho ndio tukaanza kwenda upande wa pili.
Kama kuna Mtu atanipatia suluhisho la kunipa connection ya mtaalamu wa uhakika ambae atamtibia akishapona ndio tunalipa nitashukuru Sana, atakaenipa hiyo connection kama akitibika kweli nitampatia hata 500K ya maji.
Mambo haya yanaumiza, hapa nilipo Niko makazi mapya, tulipokua tunakaa mwanzo tuliondoka kwasababu ya maneno ya watu.
Haya mambo yanaumiza vibaya mno, kunajirani yangu alishawahi Kukaa Miaka 10 ndio wakafanikiwa, kuzaa nnje ya ndoa ndio kitu sijakifiria kabisa.
NATAMANI WAJITOKEZE WATU AMBAO WASHAPITIA HUU MSOTO TUPEANE EXPERIENCE NA NAMNA WALIVYOJINASUA.
Achana na watoto wa shirki/ watoto wa dawa za kiganga Huwa wanashida.Connection Kaka naomba kama unao manguli unaowajua
Hapa ndo matatizo yalipoanzia, ushauri wangu achana na ramli, rudi kwa Mungu wako kwani yeye atajibu kwa wakati ufaao.Kiukweli ujana mbaya, nilikua nazitoa sasahiv najuta
Sawa mkuu nitashukuru nasubiri nondo hizo ukituliaKwa kifupi sana sijasoma maelezo yotee nimesoma heading TU.
Mimi nikiwa kama mdau wa afya mwandamizii senior nilipitia hiyo hali tulifunga ndoa na tukakaa miaka miwili net
Usipende kwa waganga wa kienyeji labda uende kwa mwamposa
Sijakushauri chochote cha kitaalamu baadae badae mchana nikitulia ntakupa madini na njia tulizo tumia Mimi na wife.
Kwa Sasa nakuitia kaka yangu wa dhatii kabisa akupe ushaurii Mimi pia Kuna madini alinipa Gily Gru kaka msaada wako ni muhimu SANAAAAAA hapa sema neno kaka.
Asante sanaPole mkuu
Sawa mkuu asanteHapa ndo matatizo yalipoanzia, ushauri wangu achana na ramli, rudi kwa Mungu wako kwani yeye atajibu kwa wakati ufaao.
Usiwaamini waganga ipo siku mke wako anaweza kupata mimba kumbe mimba ya mganga, na huyo mtoto akizaliwa ni shida tupu.
Ukweli ni kwamba uchawi upo, ila cha msingi fanya toba ya kweli kwa mimba ulizotoa, pia fanya toba kwa kupotoka na kwenda kwa miungu wengine (waganga) na zaidi kumbuka kiapo cha ndoa yenu kuwa mtavumiliana katika shida na raha, katika afya na katika magonjwa. Sasa ndo wakati wa kuonesha ukomavu wenu wa kuishi hicho kiapo kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Pia kupitia kusali ndipo mtaweza kuvishinda hivo vifungo vya kichawi, Kuna wakati unatakiwa ujiombee mwenyewe ukiwa na Imani thabiti. Usitegemee sana kuombewa.
Nashukuru Sana nitalifanyia kaziFanya consult na professional herbalist(sio madaktari wa kisunna) kama Unaweza kupata,
Red Raspberry leaves, Uva ursi, cramp bark, St.john's wart, Blue vervain, Cinnamon, Blessed thistle.
Hizi herbs Unaweza kupata Amazon.com
Hii combo ita target mambo ya Fertility na spiritual ,hii ni kutokana na maelezo yako ikiwa Kuna uchawi ndani yake.
Akipenda M/Mungu watoto utapata.
SawaJaribu kuwatafuta siri za asili tiktok dawa zao ni nzuri