Mwezi watano katika mihangaiko yangu nikakutana na mdada mmoja nikamwelewa tukayajenga mwisho tukakubaliana kuishi pamoja.
Alinieleza changamoto zinazomkabili huku akiwa na mimba ya miezi 2 anasema baba wa mtoto wamepotezana ni watu waliokutana katika kudanga hivyo hajui namna ya kumpata.
Hivyo basi nikajitoa kwa nia ya kumpata mke na kutoa msaada. Tukakubaliana itakuwa ni siri yetu na nikimuoa mtoto atatambulika ni wangu kawaida.
Sasa basi tukakaa pamoja kama miezi miwili akaniambia nimtambulishe kwa wazazi nikafanya hivyo nikampeleka Kwa wazazi wakamwona na wakampenda.
Sasa baada yakurudi mjini akaanza dharau ananidharau mpaka aibu Kwa majirani Yani ananifokea kama mtoto.
Kibaya zaidi anafanya kosa nikimweleza anakuwa mkali huku akisema kwa sauti "unafanya hivi kwasababu sio damu yako" ameshatangaza Kwa majirani wote kuwa mimba sio yangu.
Mwisho ameamuwa kuongea maneno mengi ya aibu na dharau kisha akaondoka mwenyewe. Ikumbukwe kwamba ameshataka kuondoka zaidi ya mara tatu nikamzuia akaona kama namng'angania akazidisha jeuri na dharau.
Sasa alipoamuwa kuondoka alisema hatarudi nyuma kwanza kwangu palikuwa panamtesa analishwa vyakula ambavyo hataki kwani yeye anataka ale chipsi Kila siku. Akafikia hatua ya kuniambia mimi sio mwanaume.
Mimi nikamuacha akakusanya virago vyake akaondoka zake mwenyewe. Sasa cha kushangaza kesho yake tu anaanza kuomba kurudi nikamwambia mimi ndio sirudi nyuma nenda kakae huko huko Kwa walio wanaume.
Akaenda akapangisha jirani na hapa napoishi mimi kisha ananisumbua sana anasema anateseka anaomba msamaha lakini mimi simtaki tena lakini kwaupande mwingine mimi roho inaniuma mimba sio yangu lakini Kuna roho ya huruma ninayo juu yake.
Ukizingatia mimba imefika miezi 8 ananiambia anataka vifaa vya kujifungulia na analala njaa hana chakula na analala kwenye mkeka.
Naomba ushauri nifanyaje nashindwa nitawaelezaje nyumbani kuhusu hili suala.