Nimejifunza kitu kutoka kwa Zelensky

Nimejifunza kitu kutoka kwa Zelensky

Kabisa mkuu..
Ule msafara wa Putin ulikuwa unatisha hata watazamaji wa nchi za mbali wa kwenye TV, imagine mlengwa mkuu Zelensky ndani ya Kyiv.. Huyu rais siyo wa mchezo bhana, ni jasiri mnoo!
Kuna uungu ndani yake.
Mungu hajawahi kumuacha Israel kabisa...japo wao humuacha lakini huwa anakumbuka agano na kuwarehemu.
 
Sasa putin na NATO nani mwanaume.

Nato ni kikundi cha malaya walijiunga pamoja kwa uoga dhidi ya mwanamme Russia
Jipe moyo anakuita...cc Bathelomayo kipofu
 
Kuna Rais wa zamani wa Ukraine naye huwa namuona akihojiwa yupo front kapiga kombati na ana silaha anapambana.

Hawa jamaa wana spirit ya ajabu kuipigania nchi yao.
Nilimuona akirejea nchini
 
Mkuu; Ulitaka kumaanisha: Kwani amewamaliza Warusi kwa kutumia jeshi la Ukraine ambalo kimwonekano ni dogo na dhaifu? au vp? Fafanua kidogo mkuu.
Mkuu nimetumia utenzi tu kama Miriam alivyoimba baada ya kuvuka bahari ya shamu na kuwaua Farao na jeshi lake.
 
Tukiachana na taarifa za CNN, BBC kule hali no mbaya sana ktk Majimbo yote na wanasema bora wangelipindua Serikari kuliko kinachojiri Muda huu. Ukraine INACHAKAZWA miundombinu yake ya kijamii na kijeshi akiwa anashuhudia na rafiki zake wa Magharibi. Kukimbia hawezi maana hawana Muda nae.
Kimsingi hakuna anayejua malengo ya Mvamizi yenye usiri mkubwa.
 
Kuna Rais wa zamani wa Ukraine naye huwa namuona akihojiwa yupo front kapiga kombati na ana silaha anapambana.

Hawa jamaa wana spirit ya ajabu kuipigania nchi yao.
Ni Petro Poroshenko aliyeshindwa uchaguzi wa marudio na Zelensky. Hata viongozi wakuu wa serikali ya Poroshenko wanashiriki mapigano mtu pekee ambaye namuona yuko kimya ni Alseniy Yatsenyuk aliyekuwa Waziri Mkuu kwa muda mfupi pale Viktor Yanukovich alipokimbia ile 2014.

Kitu nilichozidi kuamini katika vita hii ni kwamba nchi nyingi duniani hasa za uchumi wa kati na wa chini zinaongozwa na watu wasio na sifa na bahati mbaya raia hawaamini hilo. Wanasiasa na viongozi unakuta ni wale waliolelewa bungeni, serikalini, mashirika ya serikali na kujipendekeza kwingi kwenye media ila uwezo wa kuongoza wanazidiwa sana na underground wengi nchini

Volodymir Zelensky alikuwa mchekeshaji amekaa kama hana uwezo. Akaigiza kipindi kimoja cha TV akionesha udikteta, rushwa na ubadhirifu akawa anasema kitu kilekile kinachotokea nchini kwake ila kwa kisingizio cha kuigiza. Mwishowe akagombea na mwanzo hawakumuamini ila kumpa nafasi ya kumsikiliza na kutoa hoja zake akaonekana kumbe ukiachana na kuchekesha in real life anajua.

Uchaguzi akamshinda Poroshenko kwa margin ndogo. Hata jeshi kamchagua Commander in Chief umri mdogo General Zaluzhnyi ana miaka 48 hata cheo cha General wa 4 star kapewa vita imeshaanza. Jeshini kulikuwepo na majenerali wakuu wasiokidhi kivile.

Kiujumla nchi zikipata shida hubadilisha uongozi kwa sababu most of the time huwa zinakuwa na watu hopeless ambao wanaishi kwa bahati. Nchi zenye changamoto all the time kama Israel hawawezi chagua kiongozi mbovu
 
Kwa hiyo majeshi ya Ukraine ndio yalimfukuza Urusi kuendelea kufanya operation kuelekea Kiev au sio??.
Kumbe western media zilitudanganya kuwa Kiev,imeomba Urusi asiendelee na operation kuelekea Kiev ili kupisha mazungumzo.
 
Hizo zilikuwa ni propaganda za kivita ili Jamaa Mbabe ajichanganye zaidi.
 
Tukiachana na taarifa za CNN, BBC kule hali no mbaya sana ktk Majimbo yote na wanasema bora wangelipindua Serikari kuliko kinachojiri Muda huu. Ukraine INACHAKAZWA miundombinu yake ya kijamii na kijeshi akiwa anashuhudia na rafiki zake wa Magharibi. Kukimbia hawezi maana hawana Muda nae.
Kimsingi hakuna anayejua malengo ya Mvamizi yenye usiri mkubwa.
Kitaeleweka tu mkuu. Muda ndio utakaosema. Huyo Mbabe nionavyo mimi ni kwamba sasa anapiga, anaua, anabomoa n.k. (kicks of the dying horse) yaani yy ni kufanya kila aina ya uharibifu awezavyo kana kwamba ni kama mwendawazimu fulani hv ili mwisho wa siku kuwepo na ulazima wa UN kuweka majeshi kati ya kuwatenganisha Urusi - Ukraine na hapo huyo Mbabe aweze kuificha aibu yake kwa maneno ya kwamba "shukuru sana wee ngurumbili(Ukraine) ......kama sio UN kuingilia kati huu mtifuano, wallah-billah, ww Dogo (Ukraine/Zelensky) ungenitambua kuwa mm ni nani" Lakini ki-ukweli Mbabe huyu (Putin) ameshaigeuza hii kitu(Vita) na kuwa sio vita tena kama tuijuavyo vita bali ni Maangamizi ya makusudi ya Urusi dhidi ya Taifa la Ukraine. Yan afadhali hata KickBoxing ina ka-Utaratibu na Refa huwa anakuwepo ila sio Iilivyo kwa hili la Putin dhidi ya wana-Ukraine. 🏃‍♂️ 🏃‍♂️
 
Kuna Rais wa zamani wa Ukraine naye huwa namuona akihojiwa yupo front kapiga kombati na ana silaha anapambana.

Hawa jamaa wana spirit ya ajabu kuipigania nchi yao.
... lingekuwa lile zalendo la kusadikika na vibaraka wake wangekuwa wamejichimbia kusikojulikana. Uzarendo; my foot!
 
Kabisa mkuu..
Ule msafara wa Putin ulikuwa unatisha hata watazamaji wa nchi za mbali wa kwenye TV, imagine mlengwa mkuu Zelensky ndani ya Kyiv.. Huyu rais siyo wa mchezo bhana, ni jasiri mnoo!
... mimi binafsi uliniogofya sana; naona kama ndoto hadi leo sijaamini kama lilikuwa jeshi la kweli! Hollywood wakiamua kutengenezea picha litauzika sana!
 
Tukiachana na taarifa za CNN, BBC kule hali no mbaya sana ktk Majimbo yote na wanasema bora wangelipindua Serikari kuliko kinachojiri Muda huu. Ukraine INACHAKAZWA miundombinu yake ya kijamii na kijeshi akiwa anashuhudia na rafiki zake wa Magharibi. Kukimbia hawezi maana hawana Muda nae.
Kimsingi hakuna anayejua malengo ya Mvamizi yenye usiri mkubwa.
Putin alitoa maagizo ya kijeuri mapema kabisa. Kwamba wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe immediately; hataki kuona jeshi nchini Ukraine na serikali yote ya Ukraine ijisalimishe mapema mara majeshi yake yatakapoingia huko. Hakuna siri kwamba alitaka kukabidhiwa nchi ya Ukraine kwenye kisahani. Sasa ameshajua kuwa itakuwa vita ya muda mrefu na Ukraine wako tayari kufa kwa ajili ya nchi yao (kama waTaliban) huku wakipigwa tafu na NATO kwa silaha na teknolojia.

Putin ajue hii itakuwa vita ya "attrition" inayolenga kummaliza nguvu mvamizi asiwe na jeuri ya kuanzisha vita kwingine bila kupiga hesabu kamili. Amewapa fursa Marekani kutengua uwezo wake taratibu hadi ajikute chali. Ukraine itajengwa upya, pesa si suala kwa matajiri. Wazungu wakiamua kupigania haki na utu wao, hawaogopi kufa. Watu wanashangaa kwamba Putin anaua ndugu zao Warusi badala ya kuwafuata NATO kwao.
 
Kwa hiyo majeshi ya Ukraine ndio yalimfukuza Urusi kuendelea kufanya operation kuelekea Kiev au sio??.
Kumbe western media zilitudanganya kuwa Kiev,imeomba Urusi asiendelee na operation kuelekea Kiev ili kupisha mazungumzo.
Na akili zako unaamini hoja kuwa Urusi aliombwa asiendelee na vita Kyiv kisa mazungumzo ?
 
Back
Top Bottom