Nimejifunza kitu kutoka kwa Zelensky

Sasa wewe ambae huwezi hata kuongoza familia yako ya watu hawazidi 10 tena katika Ulimwengu wa tatu unawezaje kumdharau Zelensiky [emoji3]
 
Kwani US iliichukua Iraq kwa siku moja?,hebu jibu kwanza hili sio kuleta ushabiki tu hapa
Hawakuchukua muda mrefu hivi ilikuwa ni wiki tatu tu walikuwa tayari wameshaiteka Baghdad na Saddam alikuwa na nguvu Ukraine ni cha mtoto.

Russia bado sana hawezi kupambana hata na UK, France au Israel, atachakazwa vibaya sana hadi atakimbilia nyuklia.
 
Nchi inazidi kuteketezwa na Mvamizi hilo halina ubishi, lakini ukweli unabaki pale kwamba Zelensky ni jasiri na kadri vita inavyoendelea usishangae mwisho akaibuka kidedea. [emoji120]
Kuna watu hapa wanamfokea Zelensiky wakati wao jana Panya Road wamefanya yao mtaani kwao na wamebaki kuufyata na kujificha vyumbani kwao wakicomment kumzodoa Zelensiky [emoji3]
 
1)Ni vitu viwili kufananisha vita ya Iraq na vita ya ukraine.saddam ndani kwake tu alikuwa na upinzani mpaka na wananchi wake.alikuwa anaongoza nchi kwa mkono wa chuma.kuna baadhi ya maeneo vikosi vya ushirika havikupigana kabisa maana walikuwa washafanya makubaliano na wakuu wa vikosi.

2) Nchi 30 vs Iraq isiyopata msaadq kutoka sehemu yoyote ile kwq sababu alikuwa na maadui kila sehemu

3)Ukraine anasaidiwa karibu na dunia nzima
 
bila NATO Kyiv ingekuwa mikononi mwa jeshi la Putin ila Putin nae siku nyingine ajipange vizuri kabla ya kuanzisha vita maana anatukatisha sana tamaa team Kiba
Ali Kiba hawezi kushangilia wapuuzi wa Russia
 
Kuna watu hapa wanamfokea Zelensiky wakati wao jana Panya Road wamefanya yao mtaani kwao na wamebaki kuufyata na kujificha vyumbani kwao wakicomment kumzodoa Zelensiky [emoji3]
Ni bora wakajitofautisha na Zelensky. Wajue kwamba huyu Zelensky sio sawa na wanaume wa Dar ambao vitoto vidogo vidume na vijike eti vimebeba mapanga halafu wanaume wanajificha kwa hofu na vinaumiza au kujeruhi watu na kupora mali na fedha huku wamanaume wanavikenulia meno. Zelensky ni jasiri wa kupigiwa Upatu. Sasa hivi Putin, kama sio kukaza shingo kwa ajili ya kuchelea aibu mbele ya Mataifa, angekuwa kesha omba puu. 🤣
 
Mkuu tena hawa Wanaume wa Dar Pro Putin ndiyo wanashangaza sana,yani Panya Road wamewalaza saa tatu usiku,halafu wana guts za kumkejeli mwanaume wa shoka anaepambana kulinda himaya yake.Kuna mmoja tunafahamiana in person jana nilimwambia nitashangaa sana kukuona unamkejeli Zelensiky baada ya kusimulia alichokumbana nacho Kunduchi kwa panya Road.Namsubiria hapa aweke comment yake,naona bado ana wenge la Panya Road [emoji3][emoji3]
 
Teh,teh,teh 🤣 🤣 🤣
 
Sasa wewe ambae huwezi hata kuongoza familia yako ya watu hawazidi 10 tena katika Ulimwengu wa tatu unawezaje kumdharau Zelensiky [emoji3]
Zelensiky ni raisi mjinga kutokea duniani,..Leo Urusi imeruhusu wale walikojificha kwenye kiwanda kuondoka,wengine kawachukua Urusi ..

Baada ya dakika kadhaa ameanza kushambulia kiwanda...Urusi imeshachukua nusu ya mashariki ya Ukraine..

Zelensiky angelikaa tu mezani na Putin yaishe kidemorasia
 
Mwanaume wa shoka ni yule anaelinda himaya yake kwa gharama yoyoye ile,hata Putin angevamiwa angefanya kile kile anachokifanya Zelensiky,nnje ya hapo huyo atakuwa kama wanaume wa Dar wale wanaokimbizwa na Panya Road tu [emoji3]
 
Zelensiky alikuwa na maneno ya kunya,Kila siku alikuwa anamtishia Putin, eti Ukraine itajiunga na NATO,..

Angekubalina na Putini kuwa Ukraine itabaki kuwa nchi Neutral haya yanayotokea sasa Ukraine yasengelitokea..

Wako wapi NATO?kabakia peke yake anawauwa Waukraine wasio na hatia..
 
Utakuwa haupo serious wewe,unauliza kweli NATO wako wapi? Muulize Putin NATO walipo aliyepanic hadi akatishia Nuklia.
 
Silaha ya kwanza kushinda vita ni kukubalika na wananchi wako. Jamaa anakubalika kiasi kwamba wanawake kwa waume wako tayar kufa kwa ajili ya nchi yao.
 
Mwanaume wa shoka ni yule anaelidna himaya yake kwa gharama yoyoye ile,hata Putin amgevamiwa angefanya kile kile anachokifanya Zelensiky,nnje ya hapo huyo atakuwa kama wanaume wa Dar wale wanaokimbizwa na Panya Road tu [emoji3]
Kweli,lakini angelitafuta njia nyengine ya kuilinda nchi na watu wake sio kwa staili hii..

mashariki ya Ukraine yote iko chini ya Urusi,Bahari ya black sea yote sasa iko chini ya Urusi isipokuwa Crimea tu,Na huo mji wa Crimea mwanamme kaanza kushambulia kwa long range rocket..

Zelensiky imekuwa kwake,..
 
Wewe ulitaka zelensky achukuwe maamuzi gani baada ya Russia kuishmbulia Ukraine? Yaani ulitaka Ukraine ikubali kufanya lolote kutoka Russia? Kuna uwezekano mkubwa wazee wetu waliouzwa Kama watumwa walikua na akili Kama zako.
 
Utakuwa haupo serious wewe,unauliza kweli NATO wako wapi? Muulize Putin NATO walipo aliyepanic hadi akatishia Nuklia.
Putin katishia Nuke pale vita vilipoanza,Katishia Sweden na Finland kama na wao wataleta chochoko za kujiunga na NATO watakiona cha moto..

Kidume hakina masihara,Juzi kasema Urusi ina silaha kama ikizitumia dunia itashangaa..


NATO waneufyata
 
Wewe ulitaka zelensky achukuwe maamuzi gani baada ya Russia kuishmbulia Ukraine? Yaani ulitaka Ukraine ikubali kufanya lolote kutoka Russia? Kuna uwezekano mkubwa wazee wetu waliouzwa Kama watumwa walikua na akili Kama zako.
Zelensiky alitakiwa kukubaliana na Putin kabla vita havijaanza ili kunusuru nchi yake na watu wake..

Nchi imekuwa magofu,Waukraine milioni 5 wakimbizi,Ulaya haijawahi kushuhudia kitu kama hicho tangu vita vya pili vya Dunia

Zelensiky ni Raisi mjinga na mpumbavu..
 
Maoni yako nayaunga mkono 99%. Na hujabahatisha ili uandike hivi ni lazima uwe unajua sio kuotea
 
Kutaka kujiunga na NATO ndio maneno ya kunya? Kila siku tunawaambia nyinyi ambao vita mmeanza kufuatilia February 2022 kwamba Russia aliichukua Crimea, akachochea Donetsk na Luhansk kujitenga na akavunja makubaliano ya mwaka 1991 ambayo waliwekeana Ukraine, Russia na Marekani kwamba Ukraine waharibu silaha zao za nyuklia na return yake hawatojiunga na NATO na wakati huo Russia haitowavamia. Russia ikaivamia tangu 2014, kuna haja gani Ukraine kuacha kujiunga na NATO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…