Nimejipa jukumu la kuiombea CHADEMA katika kipindi hiki kigumu wanachopitia, bila upinzani imara CCM itayumba

Endeleeni kusingizia vyombo vya dola, nenda field ufanye research

Ccm ya sasa inakubalika sana kwa Wananchi

Nakuambia tu

Field ipi unayoongelea, tupo mtaani kila siku. Au hiyo hofu mliyopandikiza kwa wananchi ndio unadhani ni kukubalika? Kama mngekuwa mnakubalika, kipi kinawafanya mlazimishe kupita bila kupingwa?
 
Mleta mada atakuwa anapoteza muda kwanza wenyewe hawakubali kama wanahari ngumu ya kuhitaji maombi yeye kajuaje. CDM wanasema hata leo uchaguzi ukiwa huru kama wa 2015 wanachukua nchi kwani kwa sasa wamekubalika sana kwa sera zao sasa iweje wewe uturushe katika maombi, jamaavipi
Kwa sasa uhai wa Chadema umeshikiliwa na Dr Mashinji wa CCM!
 
Field ipi unayoongelea, tupo mtaani kila siku. Au hiyo hofu mliyopandikiza kwa wananchi ndio unadhani ni kukubalika? Kama mngekuwa mnakubalika, kipi kinawafanya mlazimishe kupita bila kupingwa?
Uchaguzi wa serikali za mitaa si mlisusia?
 
Kwa mtazamo wako Upinzani ni nini? Isije kuwa upo nje ya key
Elewa tu Nccr mageuzi hakuna mpinzani katiba yao ya asili walimuuzia Mzee Mtei.....wao wakabaki kama wanaharakati.

Ndio maana Nyerere alimshangaa mwanawe Makongoro alipojiunga nao.

Na hata mpinzani wa ukweli mzee Lyatonga Mrema aliwashtukia na kwenda zake TLP!
 
Endeleeni kusingizia vyombo vya dola, nenda field ufanye research

Ccm ya sasa inakubalika sana kwa Wananchi

Nakuambia tu

Field ipi unaoongelea, tupo mtaani kila siku. Au hiyo hofu mliyopandikiza kwa wananchi ndio unadhani ni kukubalika? Kama mngekuwa mnakubalika, kipi kinawafanya mlazimishe kupita bila kupingwa?
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa si mlisusia?

Yes, maana hatuko tayari kubariki uhuni. Na hatuna wasi wasi eti kuwa chama kitakufa kwa kukosa kiti hata kimoja kwa uhayawani. Iwapo tutaingia kwenye uchaguzi kisha tukose kura hapo tutajua kweli chama kimekataliwa na watu. Hii tunahesabia ni kama nchi iko chini ya serikali iliyopinduliwa.
 
Ukiwa juu ya siasa za vyama utaona wazi namna wananchi watakavyoihitaji Chadema kuliko makamanda wa Ufipa wanavyowahitaji.

Kwa kuwa chama kikuu cha upinzani kinapita katika wakati mgumu na mimi naamini kwamba Siasa siyo uadui, basi kwa hiyari yangu mimi Yohana nimejipa mzigo wa kuiombea Chadema iweze kuvuka salama.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu Yohana, pamoja dhamira yako ya maombi, ambayo hujaweka wazi yatapelekwa kwa nani, lkn ni lazima utambue ya kuwa magumu ambayo CDM inayapitia ni kutokana na kukiukwa kwa makusudi kwa masharti ya katiba na sheria zilizopo. Na pia uwepo wa utovu wa kimaadili, upendeleo wa wazi wa kitaasisi, vyombo vya dola, mahakama na hata bunge kwa chama tawala, huku kwa makusudi kabisa vyote kwa pamoja vikishindana kukandamiza haki za uwepo wa vyama makini ya upinzani.

Kwa hiyo basi maombi yako ni lazima uyaainishe utayapeleka kwa nani. Lakini ktk hali ya kawaida maombi hayo yanafaa kupelekwa kwa Shetani ili mapenzi yake yatimizwe. Kwa kuwa ktk hali yoyote ile, haiwezekani ukiukwaji mkuu na wa makusudi wa viapo vilivyotolewa kupitia imani za kidini na tena kwa kuapa kwa kushika vitabu vya kiimani, kunaweza kukawa na haja ya kuleta maombi ya kukumbushana kutenda haki na kutimiza wajibu wa kiuongozi.
 
Ukiwa juu ya siasa za vyama utaona wazi namna wananchi watakavyoihitaji Chadema kuliko makamanda wa Ufipa wanavyowahitaji.

Kwa kuwa chama kikuu cha upinzani kinapita katika wakati mgumu na mimi naamini kwamba Siasa siyo uadui, basi kwa hiyari yangu mimi Yohana nimejipa mzigo wa kuiombea Chadema iweze kuvuka salama.

Maendeleo hayana vyama!
Naona umehisi harufu ya kukosa kazi Bwashee wangu. Yote haya kina Bia yetu , USSR , Magonjwa Mtambuka na wengine kaliba yenu mnayafanya na kuonekana kwasababu ya CHADEMA. So ikifa mjue hata familia zenu zitateseka kidogo maana kama hakuna wa kumtukana na kzi yenu itaisha. Hata kina Ndugai na kina Mwambe watapotea sana. So salama yao na yenu ni CHADEMA imara tu.
 
Endeleeni kusingizia vyombo vya dola, nenda field ufanye research

Ccm ya sasa inakubalika sana kwa Wananchi

Nakuambia tu
Bia yetu kumbuka unaonekana na kuyaandika haya kwasababu ya CHADEMA. Mwenzako kaona mbali so usimpuuze ndugu. Utakufa njaa CHADEMA ikifa.
 
Naona umehisi harufu ya kukosa kazi Bwashee wangu. Yote haya kina Bia yetu , USSR , Magonjwa Mtambuka na wengine kaliba yenu mnayafanya na kuonekana kwasababu ya CHADEMA. So ikifa mjue hata familia zenu zitateseka kidogo maana kama hakuna wa kumtukana na kzi yenu itaisha. Hata kina Ndugai na kina Mwambe watapotea sana. So salama yao na yenu ni CHADEMA imara tu.
Kwani ACT wazalendo haipo bwashee?

Naiombea Chadema kwa sababu tumetoka nayo mbali.

Niliwahi kukata kadi ya Chadema mwaka 1993 pale mtaa wa majamati Kisutu kwenye ofisi za muda za Chadema.
 
Ukiwa juu ya siasa za vyama utaona wazi namna wananchi watakavyoihitaji Chadema kuliko makamanda wa Ufipa wanavyowahitaji.

Kwa kuwa chama kikuu cha upinzani kinapita katika wakati mgumu na mimi naamini kwamba Siasa siyo uadui, basi kwa hiyari yangu mimi Yohana nimejipa mzigo wa kuiombea Chadema iweze kuvuka salama.

Maendeleo hayana vyama!
Mnafiki we kibwengu
 
Kwani ACT wazalendo haipo bwashee?

Naiombea Chadema kwa sababu tumetoka nayo mbali.

Niliwahi kukata kadi ya Chadema mwaka 1993 pale mtaa wa majamati Kisutu kwenye ofisi za muda za Chadema.
Ndomaana hujaiombea ACT bwashee. Hata porini fisi wapo ila usipoona simba bado hujaona mwindaji makini.
 
Ukiwa juu ya siasa za vyama utaona wazi namna wananchi watakavyoihitaji Chadema kuliko makamanda wa Ufipa wanavyowahitaji.

Kwa kuwa chama kikuu cha upinzani kinapita katika wakati mgumu na mimi naamini kwamba Siasa siyo uadui, basi kwa hiyari yangu mimi Yohana nimejipa mzigo wa kuiombea Chadema iweze kuvuka salama.

Maendeleo hayana vyama!
Hatutaki dua ya wakala wa Shetani , kwanini usimuombee kiongozi wako Mangula aliyetiliwa sumu ndani ya vikao vya ccm ?
 
[SiQUOTE="Bana likasi, post: 35506042, member: 580950"]
Hata haya angalau ccm imeyafanya ni sababu ya upinzani.Ccm bila upinzani haiendi ni lzm ipigwe na nyundo ili iende.Upinzani ni nyundo ccm ni tindo,tindo bila nyundo haiwezekani
[/QUOTE]sio kweli kwan mwanzo kabla ya vyama vingi ccm ilikuwa haiendi? Hayo ni mawazo yako tu kumbuka ccm tangia 77 ipo upinzani umekuja jana tuu
 
Swala sio ccm kuyumba. Hiko chama kimeshakaa madarakani zaidi ya nusu karne, kinaongozwa na wazee wenye akili za mwaka 47 waliosoma kipindi cha Nyerere na sera za ujamaa na kujitegemea.
Kwa kifupi ni kwamba ccm imeishiwa pumzi.
Bado kina sera za kizamani sasa unategemea kuna jambo gani jipya linaweZa kufanyika chini ya ccm
hivi lowasa angeshinda angekuja na lipi jipya?!
 
Ukiwa juu ya siasa za vyama utaona wazi namna wananchi watakavyoihitaji Chadema kuliko makamanda wa Ufipa wanavyowahitaji.

Kwa kuwa chama kikuu cha upinzani kinapita katika wakati mgumu na mimi naamini kwamba Siasa siyo uadui, basi kwa hiyari yangu mimi Yohana nimejipa mzigo wa kuiombea Chadema iweze kuvuka salama.

Maendeleo hayana vyama!
Mnafique

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom