Nimejipa jukumu la kuiombea CHADEMA katika kipindi hiki kigumu wanachopitia, bila upinzani imara CCM itayumba

Nimejipa jukumu la kuiombea CHADEMA katika kipindi hiki kigumu wanachopitia, bila upinzani imara CCM itayumba

Hizi sarakasi za watawala zinaongeza umaarufu wa vyama vya upinzani vinavyolengwa. Hivyo vyama vya siasa vinavyosaidiwa ili kuja kuwa wapinzani rasmi vinahatarisha uhai wao. Watanzania wanataka vyama vinavyoshindana kwa hoja na siyo vyama vinavyounga mkono juhudi za watawala. Wanasiasa wanaodiriki kutumia njia haramu na rasilmali za umma kuhujuma umma kwa maslahi yao binafsi ni wasaliti na muda utakaporuhusu lazima watajibu mashtaka ya uhaini.
 
Tenda wema uende zako Jo... Niliichangia NCCR-MAGEUZI, Nilimchangia Mrema. Nilimchangia Lamwai... Yalikuwa ni mahitaji ya nyakati SIJUTI..
Usiumbe CHUKI na CHADEMA eti kwakuwa tu kuna nguvu yako pale ulichangia

Jr[emoji769]
Wkt huo alikuwa anatamba huyu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nami naùngana na wote wanao iombea cdm katika wakati huu wanapopitia magumu,machungu na misukosuko ya kila aina. Mungu ni mwema atatoa njia 7 za kutokea na hatimaye watavuka salama .
 
ili maombi yako yapokelewe kwanza mbowe arudishe bilioni 8.9 alizopeleka uswiss.
mbowe aseme azory gwanda alipo.
mbowe atubu dhambi ya mauwaji ya diwani wa chadema morogoro.
mbowe aseme kwanini alitaka kumdhuru lisu,na atubu
mbowe kwanini mtu atakaetaka uwenyekiti wa chadema anawatisha kuwauwa kwa kuwaambia sumu ailambwi.atubu dhambi
 
Nakujua vema Jo una CHUKI isiyoisha na CHADEMA

Jr[emoji769]
Bwashee mimi siyo kama Lijualikali.......ninaikubali Chadema katika mambo kadhaa ikiwe!o kuandaa vijana kuwa viongozi ndio hawa akina Zitto. Prof Kitila, Kafulila, Juliana Shonza, JJ Mnyika nk

Kadhalika naipinga Chadema inaposhindwa kujidhihirisha kama ni chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa sababu " imepungukiwa" vyote hakina maendeleo wala demokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mungu naomba nipe maisha marefu zaidi ili niione siku ambayo vyama makini vyote vya upinzani "vimefutwa" ama kwa njia ziliandikwa vitabuni (zimazojulikana kisheria) ama zisizoandikwa (za kihuni, mkono wa chuma au zozote zile za kishenzi) nipate kushuhudia maisha yetu ambao hatuwapendi na hatutaki mfumo wa vyama vingi nchini!

Kwa sie walau tuliouona mfumo wa chama kimoja wakati wa ujana wetu, hatutamani kurudi huko hata kama kwamba kwa sasa tunafaidika na hali ya kisiasa sasa hivi kiuchumi binafsi.

Vijana wengi humu kina Bia yetu wanatamani sana kupotea kwa kioo cha chama chetu CCM (CHADEMA).

Wanaamini kwamba hata kioo hiki tukikivunja bado tunaweza kujiona namna tulivyojipaka mafuta usoni kupitia Maji yaliyotulia kwenye pipa bila kujali usumbufu tutakaoupata kwenda nje kujichungulia ndani ya pipa, wakati kioo tuliweza kukitumia hata tukiwa tumajilaza kitandani!

Naiombea siku hiyo ifike niishuhudie!

Nishuhudie kufa kwa forum kama hii JF ambayo unapata nafasi ya kubishana kwa hoja na mtu bila kumfahamu huku ukiwa unajifunza mengi kutoka kwa "wapinzani" wako kiitikadi. Je baada ya Upinzani kufa, watapata "wapinzani" wa kujengeana hoja?
 
Back
Top Bottom