Nimejuta: Sitatamani tena binti kupitia Social Media!

Nimejuta: Sitatamani tena binti kupitia Social Media!

Hapa nilipo nimeghafirika sana,hata dinner niliyopanga kupata naye imebidi tu nilipie 1 drink na msosi wake halafu nizuge nimepata dharura!
Yaani huyo binti nilimDM insta baada ya kuona picha zake,daaah nikasema mashalaaa!Aliporespond,tukabadilishana mawasiliano na tukaanza kuongea!
Bahati nzuri wote tuko kwa jiji,basi tukapanga leo tukutane Catalunya pale opposite na Mlimani city!
Lahaula,yaani mpaka anafika sijamjua kama ni yeye!Mpaka aliposhika simu na kupiga,simu yangu ilipoita ndio nikajivunga kumpungia mkono!
Nilikaa tu kuzuga kama dk 15 then nikazuga kupokea simu ya dharura!Nimemuahidi narudi ila ndio mazimaaaa!!!!

Wadada punguzeni filters!
Kuna post imeletwa leo jalibu kuitatuta uone watu wanavyotililika....pole my bro[emoji23]
 
Acheni roho mbaya na husda.
Sasa mnataka sie wenye sura za baba tupendwe na akina nani?

Kwani wewe unataka sura au mnato?
Acheni ulimbukeni na ushamba.

Na bado, mtatujua mpaka akina Rihanna tunaoongea kiswahili sanifu na kihaya.
Shubaamit!!!!
Sasa si muweke sura zenu bila kuziedit na maphotoshop kibao?
 
Wamitandao ni hatari,FILTERS zinawapandisha chati ila kiuhalisia wengine ni sivyo walivyo.
 
Halafu sijui kwann hawajishtukii!!!Au wakijiangalia kwenye kioo,huwa hawaoni tofauti na mapicha picha wanayotupia insta?
wengi huimagine ni wazuri kwahiyo picha ya kwamba wao ni wazuri hujijenga vichwani mwao na hukomaa!
 
Nyie tatizo mnataka demu wenye chura au mwenye chuchu konzi.
Ila all in all...unataka sura au mnato?
Kama ni mnato,mbona wanawake wa sinza wana bei kuliko wa buguruni?
 
Back
Top Bottom