Nimekagua Gari sita Yard siku ya leo, majanga ni makubwa.

Nimekagua Gari sita Yard siku ya leo, majanga ni makubwa.

Mbona iliyopo hapo sio Actual distance (sio Odometer readings). Ukiona kuna herufi A au B hiyo ni setting distance (trip distance), actual distance kunakuwa na herufi ODO maana yake Odometer reading.
Hiyo haibadiliki mkuu
Madmax amekujibu na yuko sahihi kabisa, odo ni hiyo unayoiona kwa chini hapo hiyo ya juu ni mileage
 
View attachment 3099763

Mfano hiyo hapo juu ni actual mileage inayonekana kwenye gari.

View attachment 3099769
Hii ni mileage inayoonekana kwenye website ya EAA.

Gari imeshushwa 120,000Km

sasa hiyo ina uafadhali ila zipo ambazo ni worst kuliko hiyo.

inaonekana kununua gari na kuja kuuza na actual Kilometers watu hawataki kununua, kwa hiyo mwendo kwa sasa ni huo.

Zipo gari nimekuta zimetembea 200,000Km ila dashboard ina 55,000Km,.

Hapo sijagusia Diagnostic Reports ni majanga matupu, Gari nyingi hapo zilikuwa na faults kuanzia 8 mpaka 20.

Tumeanza kusema siku nyingi usinunue gari kwa Km, tafuta gari nzima hata kama ina 300000Km tulia humo.
Ndiyo lengo la dpw kufanya tanzania na africa kuwa dampo ...kwasasa tz hatuna kiongozi nchini
 
Mi nadhani ukitaka kilichonyooka agiza mpya. 0km. Hizi used zetu ukianza kuzikagua sana yatakushinda. Kikubwa angalia yenye unafuu, lipia kavimbe huko.
Lengo la kukagua ni kuona kama unaweza kuyabeba madhaifu utayokutana nayo si kukimbia, hizo gari zote tumekagua jamaa kafikia hatua ya kuchukua gari ambayo ina 127000km japo dash yake iliandika 56000Km.

angalau ndio gari iliyokuwa na least problems
 
Back
Top Bottom