Ndugu matatizo yapo kikubwa usikate tamaa.
1. Mimi mke wangu ameondoka this December kaacha watoto watatu, hatukuwa na house helper ikabidi niombe siku kadhaa job niangalie namna watoto watabaki.
2. Feb 16 nimefiwa na baba mzazi, tunamaliza kuzika, kinakaa kikao cha familia kaka zangu wanajimilikisha mashamba na mali za mzee zote, nikakausha kwa vile nina maisha yangu mbali na huo mkoa.
3. Nimetoka msibani na watoto tunarudi home tunakuta mama yao alikuja na fuso akasafisha nyumba.
Lakini sikuteteleka, kwa kuwa nilirudi na msaidizi wa kazi, niliomba mkeka kwa jirani wakalala. Kesho nikanunua godoro dogo kwa ajili ya watoto na yule binti maisha yakaanza. Kurudi job kwa wema tu boss akaniongeza siku 14 ikabidi sasa nizitumie kuweka mambo sawa.
Moral of the story, changamoto za maisha zisikukatishe tamaa.