DOKEZO Nimekata tiketi VIP basi la Happy Nation, lakini halina huduma hadhi ya VIP. Naweza kulalamika wapi?

DOKEZO Nimekata tiketi VIP basi la Happy Nation, lakini halina huduma hadhi ya VIP. Naweza kulalamika wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Baaasi shida ipo kwenye kabila na aina ya ticket ulokata kwa nini huwa mnapenda kujikweza?
Wew ndo una matatizo...

Na akili hiz ndo zinatufanya Tanzania tuwe maskini wa kutupwa hadi leo..

Na sioni kama tutaendelea soon
 
Nimepanda Happy Nation( BUSINESS CLASS) la saa 10:00 kutoka Bukoba to Dsm kwa NAULI ya 120,000/.

Hilo basi halina AC na pia CHOO chake haki flush tunalazimishwa kuchimba dawa kwa KUJILIPIA hiyo huduma. Konda hana jibu la malalamiko yetu yote, likiwemo la kurudishiwa nauli inayobebwa na hiyo business class. Nani mhusika kwa sakata hii?

View attachment 2861202

Nijulishe na namba yake tafadhali.
Kama shabiby wapo route hiyo ungepanda hao wengine ni wababaishaji
 
Biashara ya mabasi ni biashara ya kitapeli sana.

Enzi zile kuna darlux wakawa wanasema gari ina wifi hivyo watu wakawa wanalipishwa bei ya luxury ila ukiingia ndani kila siku mtaambiwa kwamba kifaa cha wifi kina matatizo.

Mbaya zaidi wakawa kama unatokea dar wanaenda kusimama kwenye kihoteli kimoja kiko bahi, mshikaji wangu alikula pale wali aliharisha nusu afe.

Vile nilikua mteja wao siku moja nikawaambia huu Uswahili wenu ipo siku hii kampuni itakufa, kweli Uswahili ukaiua darlux.

Maisha yamebadilika kidogo sasa long safari yoyote kama sijaenda na gari binafsi basi ni flight tu. Mabadi ni waswahili sana.
Bongo utapeli kila sehem.
 
Bm pia sandhill tatizo, unalipa nauki ya Dar Moshi 45k bus la luxury but unapandishwa mkweche
 
Kwa hapa Tanzania,heri Shabiby anajitahidi
Hata kama hatoi huduma zote ila angalau gari lake ndani seat ni pana
1×2,,upande wa seat mbili Kuna nafasi na zimetenganishwa , kiasi kwamba jirani Yako hawezi kukubugudhi

Free wifi ni kwa ajili ya movies tu walizirecommend..iwe utatumia simu Yako, ama Tablet yao
Utaangalia movies tu walizoziweka mule,na vinyimbonyimbo,,nje na hapo hakuna kingine.



Vip nyingine usijikoroge kutupa pesa,
Hakuna chochote cha maana.
ABC wanaojiita VIP, labda choo na AC ..seat zimebanana hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nia yako ulikua unye ndani ya gari! Konda alikusoma mapema Sana ndio maana akafunga choo. Magufuli alisemaje kuhusu kunya?
 
Happy Nation ni mabasi ya hovyo. Unakata basi unaambiwa jipya namba E unaletewa mkangafu basi limechoka halitamaniki halafu bovu. Halafu wana kiburi hawajali. Nadhani wamekua kwa haraka sana na wameelemewa.
 
VIP ya Bongo ni Gari kuwa na milango miwili, siti 1x2, biskuti, pipi, maji na juisi(hivi hupewi vyote, vinatolewa viwili kati ya hivi)

Mimi huwa napanda daraja la kawaida au la kati tu kulingana na ninakoenda ambapo nauli inakuwa ni minimum recommended
kwan vip lina huduma gani kwan mpaka useme hakuna tz nzima


msikariri
 
Back
Top Bottom