Nimekataa kulipa Pesa ya Taka na ulinzi kama hawatanipa risiti za EFD. Nimepewa barua ya wito serikali za mitaa

Nimekataa kulipa Pesa ya Taka na ulinzi kama hawatanipa risiti za EFD. Nimepewa barua ya wito serikali za mitaa

Rob Pole na changamoto, kimsingi una haki ya kudai risiti ya efd kwenye taka kwa sababu kampuni zinazozoa zinatakiwa kuwa na efd machine, ulinzi mtaani hawana efd sijajua upo mkoa gani ila pia ipo shida kubwa ya upatikanaji wa hizo efd machine, imagine kata ina mitaa labda 7 ina efd moja, mara mtandao upo down, mara imeharibika na mengine mengi
Mjinga mpe cheo rob
Huwa wanazitoa kabisa, wanakua na hizo risiti kibwena.
Ukilipa risiti yako inaandikwa jina kwa mkono pale juu..

Hiyo kua na mashine moja wala sio excuse.

Unadhani kwenye masoko huwa wanadanyaje?? Njia ni hiyo hiyo, zikibaki na wewe mtumishi sio mjanja zitakudodea.
 
Kila mwezi huwa nalipa 2000, ya uzoaji Taka, sababu kazi wanayofanya inaonekana, kila wiki hupita na gari lao kukusanya taka.

Si sawa kupingana na walio wengi, katika mtaa wako, hata kamaa kuna mahala hawako sawa (hii ndio busara).

Ndio unahoja ya msingi unataka risiti za EFD, lakini ulitakiwa kwanza kutoa ushirikiano lipa kiasi husika, Then fuatilia serikali za mtaa kupata ufafanuzi au mwongozo kwanini hujapewa risiti unayohitaji.
Uko sahihi binafsi namshangaa mleta mada
Mambo ya ulinzi na kuzoa taka mitaani sio mambo ya TRA hayo

Mtu aweza soma lakini akawa mpumbavu aishiye mtaani.Wanajua ana akili huko kazini kwake lakini mtaani ni hopeless kabisa Sababu unakuta hahudhurii hata vikao vya serikali ya mtaa vikiitishwa yeye ni ndani ya nyumba yake tu na kwenye gari kwenda kazini na kurudi tu ndani ya nyumba

Hajui kinachoendelea mtaani na hajui hata kazi ya serikali ya mtaa ni nini?
 
Rob Pole na changamoto, kimsingi una haki ya kudai risiti ya efd kwenye taka kwa sababu kampuni zinazozoa zinatakiwa kuwa na efd machine, ulinzi mtaani hawana efd sijajua upo mkoa gani ila pia ipo shida kubwa ya upatikanaji wa hizo efd machine, imagine kata ina mitaa labda 7 ina efd moja, mara mtandao upo down, mara imeharibika na mengine mengi
Mjinga mpe cheo rob

Hiyo ibaki kuwa changamoto Kwa serikali
 
Ukitoa huduma toa risiti.
Ukipata huduma dai risiti.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Nyie watibeli wabishi sana tatizo 😂👊🏾
 
Back
Top Bottom