Nimekataa kurudiana naye, sasa anataka kuvujisha picha mtandaoni alizonipiga kwa Siri. Sijui Nifanyaje?
Wanajukwaa, nina jambo langu nataka niwashirikishe. Kwa muda mrefu limekuwa likinisumbua, naona linaweza kuhatarisha vitu vingi kwenye maisha yangu. Naombeni mnisaidie.
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume fulani. Siku moja nilipokuwa nimelala kwake, alinipiga kwa siri picha za faragha bila mimi kujua. Baadaye mahusiano yetu yakavunjika na kila mmoja akaendelea na maisha yake kwa takribani miaka miwili.
Mara kadhaa amekuwa akinifuata akitaka turudiane, lakini kwangu imekuwa usumbufu. Nilipokataa, alianza kunitishia kuwa atazisambaza picha hizo mtandaoni na kuwatumia watu ninaofahamiana nao, hata watu wa ofisini.
Sijui nifanye nini, kwa sababu tayari amenitumia baadhi ya picha hizo kuthibitisha kuwa bado anazo.